Rais Magufuli afuta safari ya UN General Assembly

Kutokana na janga la tetemeko la ardhi, kwa mara nyingine Mheshimiwa Rais wetu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania analazimika "kuvunja" safari ya kwenda kuhudhuria Mkutano wa 71 wa Umoja Mataifa ambao unaanza kesho tarehe 20.09.2016 hadi 30.09.2016

Kwa mujibu wa Ms. Mindi Kasiga aliyehojiwa na gazeti la The Citizen Mheshimiwa Rais amelazimika kutoenda kuhudhuria mkutano huo ili kushughulika na matokeo ya maafa ya tetemeko hilo lililochukua maisha ya Watanzania wenzetu takribani 19 huku wengine takribani 200 wakiachwa majeruhi.

NOTE: Mada mbalimbali zitajadiliwa kwenye mkutano huo lakini moja ya mada ambayo inatarajiwa kuwa na msisimko ni ile itakayozungumzia wimbi la Wakimbizi na Wahamiaji duniani. Kwa mujibu wa tovuti ya Umoja wa Mataifa, hii ni mara ya kwanza Mkutano Mkuu wa UN kukutanisha wakuu wa nchi kujadili suala hilo.

Pamoja na hilo la Wakimbizi na Wahamiaji, pia kutakuwa na kikao muhimu sana ambacho kitachukua takribani 70% ya mkutano wote kutokana na umuhimu wake. Huu ni mdahalo unaolenga kuzungumzia malengo ya maendeleo endelevu na nafasi yetu katika kusukuma mabadiliko ya kufikia malengo hayo.

United Nations

View attachment 402894
Mmm, this is now too much!
 
Safari ya pili hii mkuu anaihairisha, ya kwanza ilikuwa kwenda nchi jirani wiki iliyopita. lakini mkuu aliihairisha sababu ya tetemeko kagera.

Hakika tumepata Rais wa wanyonge na hili tetemeko inaonekana ni jinsi gani limemgusa. Ila tu najiuliza kughairi safari, kwa sababu ya tetemeko halafu kwenye tetemeko huendi, Hapa ndiyo naamini siyo kila swali lina jibu.
 
Mkuu Chige, kuna kujali kwa aina nyingi, wengine kujali kwao ni kwa huruma na compassionately kwa kuwatembelea waathirika na kutoa pole
Kuwafariji hata kama huna msaada wowote kwao, na wengine kujali kwetu ni kuguswa na kuhitaji kusaidia hivyo hatutembelei waathirika wala hatutoi pole, bali ndio watu tuko bize kusaidia mambo yaende. Kama waathirika watakula pole na watalalia hizo pole, wapeni pole nyingi za kutosha hadi kujengea nyumba zao! . Sisi tutajifungia ofisini tukipokea simu za michango hivyo tukija eneo la tukio, hatuji kutoa pole wala kufariji bali kuangalia kile ambacho tumesaidia tena tunataka kulinganisha hizo pole zenu zimefanya nini na sisi misaada yetu imesaidia nini!.
Pasco
Kwa kweli sijui huko kwenu lakini huku kwetu; wallah tuna kautamaduni ketu huenda ka peke yetu!! Tukisikia kilio tutaacha kila kilicho chetu na kukimbilia kilioni... na kama ulivyoeleza hapo juu; ukija na mkono ulionyooka basi Inshallah na ukija na mkono uliokunja basi alhamdullilah! Shughuli watu ati na watu sharti wahudumiwe!

Hayo tuyaache!

Fanya kumfikiria jirani wa mtaa 3 na yule wa mtaa wa 7. Kikisikika kilio tu nyumba ya jirani, yule wa mtaa wa 7 atafanya hima hima hadi kilioni! Anawahi kufika huku akihema na akiwa hana japo thumuni wala kibaba mkononi! Siku ya kwanza, ya pili; tunae! Siku zote hizo tunalia nae!! Huyu tutakuwa nae hadi siku jamvi la mwisho linaanuliwa. Kwa siku zote hizo; jirani huyu hakupitwa na uji wa shughuli wala mlo wa jioni ingawaje hakuja na hiki wala kile! Lakini si tulikuwa nae?! Si tumelia nae huyu?!

Lakini kuna huyu wa mtaa wa 3 sasa... labda ni kv maridadi au mnatashati sana! Au huenda ni kibri tu na majivuno ya kuzaliwa, usomi, au chochote kile kasoro ya maradhi! Huyu katu hana muda wa kuja akihema kukimbilia kilioni! Inawezekana kabisa akiwa huko kwake nae analia pamoja nasi; lakini nani ajue! Inawezekana kabisa vilio vya majirani huwa vinamgusa sana na hivyo huamua kujifungia chumbani siku kadhaa akilia peke yake; lakini kama ni kilio si yatupasa tulie pamoja?! Lakini pamoja na yote hayo si kwamba hatatokea kabisa; abadani! Si ajabu siku ya pili tu, hamadi, huyu hapa! Atapepesa macho huku, atapepesa macho kule, kabla hamjakaa sawa; minoti hiyooo! Ndiyo minoti; ataacha minoti hapo kisha huyooooo; anatoa hudhuru anataka kuwahi bandarini!!

Atafanya hivyo kwenye kilio cha kwanza, kisha cha pili, kisha tatu na cha nne, na cha tano hatimae inatosha kwa majirani kufahamu kwamba jirani wa mtaa wa 3 si wa kulia nae kilio bali ni wa kuja kumwaga noti na kuondoka!

Kwa huku kwetu tulivyo, jirani mtaa wa 3 na minoti noti yake yote hiyo anayotumwagia lakini tunamhesabu si mwenzetu! Si kwa lengo la kulipiza wala kukomoa! Nawe yakikukuta, haidhuru hata kwa kukopa, majirani watamiminika kwa wakati wao na kukumwagia noti kama ufanyavyo; kisha haooo! We kwako mtaji si pesa bwana!

Hakika sie mwenzetu ni yule wa mtaa wa 7 anayefanya hima kuwahi kilioni, kisha tunalia nae pamoja kipindi ambacho machozi yatumwagika mithili ya bomba la mvua! Huyu wa mtaa wa 7 ndie mwenzetu manake ndie anamsaidia baba au mama mwenye nyumba kumfuta machozi kwa siku zote hizo! Haidhuru amekuja kilioni pasi na pishi ya mchele wala kibaba cha uwele... lakini huyu ndo mwenzetu!! Aliyefanya hima kuacha kitanda chake hata kama ni cha teremka tukaze lakini akaja kufarijiana na walio msibani wakati chozi bado linatiririka!!
 
Kitu gani hasa kimemzuia asiende huko UN?
Ukisikia ufukunyuku ndio huu sasa!!! E bhana eh, narudia: Mheshimiwa Mtukufu Daktari wa Hisabati na Kemia; masomo magumu kuliko yote duniani; amefuta safari ya kwenda UN ili ashughulikie maafa ya tetemeko la ardhi!

Ukihoji kama ndivyo mbona sijui wapi sijui mbona hata kukanyanga kwenyewe hajakanyaga; wallah nakuripoti!! We twende tu....
 
Uyoo ndo Magufuli.

Magufuli anahitaji mtu wa kumcontrol lasi hivyoo utasikia mengi sana mpaka ifike 2020 utakuwa hutaki kusikia habari zake.
Ndugu kwani Magufuli ni rais wa UN au Tanzania? Mwacheni awatumikie Watanzania. Mnataka akatumbue mifedha kama yule?
 
Bora ungekaa kimyaa.

Wewe mbona unatokaga kwenda kutafuta riziki ungekaa ndani uwatumikie watoto wako. Na wewe ni baba wa wapi wa mtaani au nyumban kwako?
 
Kwenye maisha hasa ya kisiasa lazima uwe very smart upstairs na usifanye kila kitu to the xtreme always soma mchezo ili uweze kuwaacha maadui zako kisiasa mdomo wazi halafu merits zote zije kwako!
Daima fanya uwezavyo kuficha uhalisia wako hapo adui atahangaika sana kukupata kwenye lolote
Wa kwanza alisafiri sana akatoa nafasi ya kujulikana hulka yake
Huyu hataki kabisa kusafiri anaanza kujianika
JK pamoja na kelele zote hakuwahi kujibu bali ndio kwanza alizidisha safari[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Huyu kama hasafiri asitoe sababu zozote! Hasafiri! Hasafiri full stop...Visingizio sio vizuri
Nadhani kwenye hili Magufuli yuko sahihi...

Hakuna jipya la kumfanya aende...kuongelea suala ka wakimbizi na mazingira...Makamu wa rais ana kazi gani??

Nlichogundua...Magufuli ana akili sana..pengine kushinda watanzania wengi humu..ukiumiza kichwa kidogo utamuelewa. hahaha
 
Kwa kweli sijui huko kwenu lakini huku kwetu; wallah tuna kautamaduni ketu huenda ka peke yetu!! Tukisikia kilio tutaacha kila kilicho chetu na kukimbilia kilioni... na kama ulivyoeleza hapo juu; ukija na mkono ulionyooka basi Inshallah na ukija na mkono uliokunja basi alhamdullilah! Shughuli watu ati na watu sharti wahudumiwe!

Hayo tuyaache!

Fanya kumfikiria jirani wa mtaa 3 na yule wa mtaa wa 7. Kikisikika kilio tu nyumba ya jirani, yule wa mtaa wa 7 atafanya hima hima hadi kilioni! Anawahi kufika huku akihema na akiwa hana japo thumuni wala kibaba mkononi! Siku ya kwanza, ya pili; tunae! Siku zote hizo tunalia nae!! Huyu tutakuwa nae hadi siku jamvi la mwisho linaanuliwa. Kwa siku zote hizo; jirani huyu hakupitwa na uji wa shughuli wala mlo wa jioni ingawaje hakuja na hiki wala kile! Lakini si tulikuwa nae?! Si tumelia nae huyu?!

Lakini kuna huyu wa mtaa wa 3 sasa... labda ni kv maridadi au mnatashati sana! Au huenda ni kibri tu na majivuno ya kuzaliwa, usomi, au chochote kile kasoro ya maradhi! Huyu katu hana muda wa kuja akihema kukimbilia kilioni! Inawezekana kabisa akiwa huko kwake nae analia pamoja nasi; lakini nani ajue! Inawezekana kabisa vilio vya majirani huwa vinamgusa sana na hivyo huamua kujifungia chumbani siku kadhaa akilia peke yake; lakini kama ni kilio si yatupasa tulie pamoja?! Lakini pamoja na yote hayo si kwamba hatatokea kabisa; abadani! Si ajabu siku ya pili tu, hamadi, huyu hapa! Atapepesa macho huku, atapepesa macho kule, kabla hamjakaa sawa; minoti hiyooo! Ndiyo minoti; ataacha minoti hapo kisha huyooooo; anatoa hudhuru anataka kuwahi bandarini!!

Atafanya hivyo kwenye kilio cha kwanza, kisha cha pili, kisha tatu na cha nne, na cha tano hatimae inatosha kwa majirani kufahamu kwamba jirani wa mtaa wa 3 si wa kulia nae kilio bali ni wa kuja kumwaga noti na kuondoka!

Kwa huku kwetu tulivyo, jirani mtaa wa 3 na minoti noti yake yote hiyo anayotumwagia lakini tunamhesabu si mwenzetu! Si kwa lengo la kulipiza wala kukomoa! Nawe yakikukuta, haidhuru hata kwa kukopa, majirani watamiminika kwa wakati wao na kukumwagia noti kama ufanyavyo; kisha haooo! We kwako mtaji si pesa bwana!

Hakika sie mwenzetu ni yule wa mtaa wa 7 anayefanya hima kuwahi kilioni, kisha tunalia nae pamoja kipindi ambacho machozi yatumwagika mithili ya bomba la mvua! Huyu wa mtaa wa 7 ndie mwenzetu manake ndie anamsaidia baba au mama mwenye nyumba kumfuta machozi kwa siku zote hizo! Haidhuru amekuja kilioni pasi na pishi ya mchele wala kibaba cha uwele... lakini huyu ndo mwenzetu!! Aliyefanya hima kuacha kitanda chake hata kama ni cha teremka tukaze lakini akaja kufarijiana na walio msibani wakati chozi bado linatiririka!!
Mkuu Chige umenikumbusha mbali! ,enzi zile za kulala chini misibani, Tanga linaazimwa bure, mikeka Msikitini, kina mama kupiga na kula pamoja kwenye masinia na kupokezana jeneza hadi kusaidiana kufukia!.

Misiba ya siku hizi
Sare za kushonesha.
PA inakodishwa
MC anakotaka
Waimba kwaya wanakodiwa
Waliaji wenye sare wanakodiwa
Chakula ni catering
Mpambanaji wa kulipwa
Jeneza la gharama
Gari la maiti la kukodi
Kaburi la zege
Mashine ya kushusha jeneza
Maua ya kununua,
Padri /Shehe /Mchungaji analipwa
Ndugu walikuwa wanakuja na mahindi/mchele na Maharage, sasa ndugu wanakopa nauli na kumtegemea mfiwa!.
Zamani watu wanalala msibani, siku hizi ndugu tuu! .
Wanawake nywele tim tim ni mwendo wa kanga na mitandio, siku hizi wanaanzia saloon kisha suruali na vimini! .
Misiba ya kizamani unatangulia utu mshikamano na ushirikiano, misiba ya
kisasa inaongea pesa! .

Bora kabisa jamaa ajifungie tuu ndani afanye kazi ya mobilisation of resources kule ziende pesa na sio kupeleka utu! . Pesa ndio kila kitu, money can buy everything including love and happiness! .
Zamani mtu aliheshimiwa na kuthaminiwa kwa utu wake na sio mpaka awe na kitu! .
Sasa thamani ya mtu ni ana nini? ,gari, nyumba, Pesa etc na sio utu tena! .
Pasco
 
Nadhani kwenye hili Magufuli yuko sahihi...

Hakuna jipya la kumfanya aende...kuongelea suala ka wakimbizi na mazingira...Makamu wa rais ana kazi gani??

Nlichogundua...Magufuli ana akili sana..pengine kushinda watanzania wengi humu..ukiumiza kichwa kidogo utamuelewa. hahaha
Huu ni unafiki of the highest order. Watanzania mtadanganya nafsi zenu mpaka lini. Mficha maradhi kifo humuumbua. Ngoja tusubiri kifo.
 
Mkuu Chige umenikumbusha mbali! ,enzi zile za kulala chini misibani, Tanga linaazimwa bure, mikeka Msikitini, kina mama kupiga na kula pamoja kwenye masinia na kupokezana jeneza hadi kusaidiana kufukia!.

Misiba ya siku hizi
Sare za kushonesha.
PA inakodishwa
MC anakotaka
Waimba kwaya wanakodiwa
Waliaji wenye sare wanakodiwa
Chakula ni catering
Mpambanaji wa kulipwa
Jeneza la gharama
Gari la maiti la kukodi
Kaburi la zege
Mashine ya kushusha jeneza
Maua ya kununua,
Padri /Shehe /Mchungaji analipwa
Ndugu walikuwa wanakuja na mahindi/mchele na Maharage, sasa ndugu wanakopa nauli na kumtegemea mfiwa!.
Zamani watu wanalala msibani, siku hizi ndugu tuu! .
Wanawake nywele tim tim ni mwendo wa kanga na mitandio, siku hizi wanaanzia saloon kisha suruali na vimini! .
Misiba ya kizamani unatangulia utu mshikamano na ushirikiano, misiba ya
kisasa inaongea pesa! .

Bora kabisa jamaa ajifungie tuu ndani afanye kazi ya mobilisation of resources kule ziende pesa na sio kupeleka utu! . Pesa ndio kila kitu, money can buy everything including love and happiness! .
Zamani mtu aliheshimiwa na kuthaminiwa kwa utu wake na sio mpaka awe na kitu! .
Sasa thamani ya mtu ni ana nini? ,gari, nyumba, Pesa etc na sio utu tena! .
Pasco
Love bought by money is not love.
 
Bwna magu cdhani kama anaelewa jambo lolote la international politics n affairs
 
Kwa tabia hii kuna siku malaika atatutia aibu, tusubiri tu
 
Back
Top Bottom