Rais Magufuli afuta safari ya UN General Assembly

Rais Magufuli afuta safari ya UN General Assembly

Hofu ya lugha ya malkia tu hiyo, mengine ni blah blah tu. Ina maana bila yeye kuwepo nchini hakuna kitakachofanyika Bukoba? Dalili zilianza kwenye mkutano wa AU, ikaja SADC, na sasa UN.
Kusema kweli taifa letu linadhalilika mno safari hii.
 
Mshana jr NINAKUUNGA mkono, awamu hii tuna tatizo kubwa sana katika mahusiano ya kimataifa, unajua mikutano kama hii huzaa matunda kwani maraisi hutumia kuonana na wenzao kando ya mikutano na kuzungumzia mahusiano ya kibiasha na yenye tija kwa nchi zao.
Naona raisi wetu anaendeleza visingizio visivyo na mashiko.
AMEKIRI
1. Haendi bukoba anawatu wa
kushughulikia tetemeko
2. Amesema wabukoba wachape
kazi, kwnn naye asichape enda
po wahanga wanachapa analipi
la kuomboleza?

Afundwe ktk hili, mbahili hapigagi hatua sawa na aliyepewa talanta moja akaificha mchangani
Very intelligent comment!
 
kaisha soma machale ahaaaaaa hivi kagera ameishaenda? te te te huku member states tulikuwa tumemsubiri mwenzetu jamani te te the embu niendelee kusoma hapa the UN charter.
 
Tetemeko ni vijisababu tu wanapata Masada ya wahanga wao wanagawa nusu kilo Mimi niko Bukoba hali nimbaya sana watu wanapewa kikombe kimoja cha unga na sukari alafu mnasema eti anashugulikia wahanga wa tetemeko? Mbona hana hofu ya Mungu? Nakuapia Taifa hili linashambuliwa kutokana na Magu kasome torati Daudi alizini na mke wa Uria lakini Mungu akadhibu Taifa zima mimi naamini majanga mengi yataendelea kutokea nawatu wataendelea kufa nakuteseka kutokana na uovu wa magu na kachama kake.
Acha kupotosha watu.. kasome vizuri hiyo habari ya daud
 
Si kweli kwamba viongozi wakuu wote wa nchi za dunia wanaudhuria mkutano huo wa UN, Nchi zingine wanawakilishwa na na viongozi wengine wakiwamo mabalozi wao walioko huko, Nchi zingine wapo na excuse kutokana na sababu mbalimbali na wanatuma contribution zao electronically, wengine wanashiriki remotely (Tukumbuke technologia - Dunia kama kijiji ) ..... Nchi zingine wanaenda kama wasikilizaji tu....
Bado ukweli unabaki kuwa G8 ndio mabingwa wa mikutano hiyo..... Asipoenda USA, Germany, France, Russia, China na wengine kama Brazil, SA.... unaweza question kwanini.....???
Nadhani viongozi wengi wangependa kuonana na Nyota hii ya Tanzania....... Record yake ipo Juu.... Viongozi wakuu wa dunia wanatambua nini anafanya katika Taifa lake na ni jambo zuri tu. Na ni mfano wa kiongozi bora anayeibukia katika karne hii ya ustaarabu Africa...... Utaratibu wa maisha lazima ufuatwe sio kuishi ishi tu bila mpangilio na ndio wengi wale wa maisha ya mikato hawataki na wanambeza....
Kwa wale members waliozoea maisha ya kushabikia kitu bila ya kuwa na critical thinkings, ubababishaji , usanii, wizi, mission town, utapeli na wenye chuki tu na kiongozi wetu huyu mwenye nia njema na nchi hii watanipinga.........Ila karibuni tuendelee kujadili bila matusi.
 
Tulimchagua kuwa rais wa watanzania hivyo matatizo ya watanzania inatakiwa iwe ni kipaumbele nambari moja kwa rais anayejitambua. Hongera Mh. Magufuli kwa kutambua fika jukumu lako kama rais. Watanzania wenzako wanahitaji msaada wa haraka hivyo safari kwa sasa zikome kwanza. Ukiendelea hivi ndugu rais hata hao UN na jamii ya nje watakuheshimu mara 100 na hawatakuletea fyokofyoko kwa sababu watatambua kuwa huna mchezo na unawajali wananchi wako kwa dhati na kwa vitendo.
 
Japo ngumu kumeza ila tuvumilie tuu, maana hamna namna nyingine
 
Back
Top Bottom