Rais Magufuli aagiza daraja la Busisi limalizike kwa miaka 3 na sio 4. Awataka Wananchi kuongeza kulima

Unadhani hatumii wataalamu? Hiyo ni idara aliyo kaa na kuiweza kwa miaka,hata mkandarasi atakua anajua miaka mi3 ni mingi iwapo kila kitu kipo kwa nini apoteze muda
Hosteli za udsm aliharakisha hivyohivyo na tuliona matokeo yake,Barabara alizojenga tuliona zilivyosumbua ukarabati. Subira ni muhimu tusiharakishe mambo yamsingi kutafuta sifa binafsi tatizo ni wasiwasi linaweza zinduliwa awamu ya sita ajikute kagawana sifa na huyo ajaye...
Alafu hamna cha mkakati hapo alikoswakoswa kuzama ndomana anajenga na kupotezea mabilioni yetu humo? angeyatumia kujenga hospitali au kwenye miradi ya maji angesaidia watu wengi sana! Hii nchi rais asiruhusiwe kujiamulia miradi mikubwa kuzidi bilioni 50 ambayo haijapitishwa bungeni (bunge lenyewe sasa...)
 
Watanzania tututegemee ajira mpya za shifti ya usiku ili matarajio ya Mh.Rais yafanikiwe.
 
Kuongeza kasi ya kazi ni jambo linalowezekanacila ni gharama zaidi kuliko kufanya kazi kwa kawaida. Fikiria kufanya kazi ziwani usiku.
Unadhani hatumii wataalamu? Hiyo ni idara aliyo kaa na kuiweza kwa miaka,hata mkandarasi atakua anajua miaka mi3 ni mingi iwapo kila kitu kipo kwa nini apoteze muda
 
Hapana mkuu ni swala la kueleweshana tu, hakuna haja ya kuitana majina ya kejeli
inaweza kuwa km Hostel za UDOM expanded joint
ghorofa ikijengwa zile nguzo na beam huwa zinakaa miezi 6 kukauka na kumwagiliwa
sasa km usiku na mchana muda wa kukauka ni ule ule
Hivi daraja la Ubungo, stand ya Mbezi ile barabra ya Kimara Kibaha walikovunjiwa nako muda umepungua au umeongezeka sijasikia kufunguliwa, au epansion joint haziungi?
 
Sina shida na Daraja hilo ( hili ) Kujengwa bali nina shida na jinsi Rais wetu anavyolazimisha liwahishwe Kumalizika tofauti wa Wataalam wenyewe.
 
Unadhani hatumii wataalamu? Hiyo ni idara aliyo kaa na kuiweza kwa miaka,hata mkandarasi atakua anajua miaka mi3 ni mingi iwapo kila kitu kipo kwa nini apoteze muda
Unapo crash works program lazima gharama ipande,utalipa overtime nyingi,utaongeza resources..so construction costs zitakua juu na kuadhiri contract sum agreed!hizo additional costs nani atazibeba?? For me that was irrational instruction..
 
Yale maagizo aliyatoa tu kuwafurahisha wadanganyika lakini mkataba umempatia mkandarasi miaka minne na hilo linalindwa kisheria
Wanasiasa ifike muda muwe mnaheshimu Taaluma za Watu na msitake Sifa kwa Wafuasi wenu na baadae yakatokea Maafa yatakayowachafueni.
 
Ingawa sina hakika kama daraja hilo kwa urefu huo ni potential kiasi hicho hadi litumie pesa nyingi kiasi hicho wakati bado kuna changamoto nyingi sana sekta ya afya na elimu ambazo ni potential zaid.

Nadhani Mh. Anapambana kuacha historia yenye kuvunja record.
Hili la daraja hapana hata mimi napingana nalo hakuna potentialities zozote kwenye daraja hili na hasa kwa ukubwa wake na gharama zake za ujenzi , maana kwa hesabu ya kawaida serikali inatumia pesa nyingi sana kwenye daraja hili wakati sio daraja la kibiashara hivyo halita kuwa na return kiuchumi badala yake kupelekwa kivuko ambacho kingechangia sana pato la taifa

ni sawa tu na daraja la kigamboni , hayo yote hayakuwa na ulazima sana wa kuyajenga kabla ya kutatua kwanza changamoto ambazo zipo sekta nyeti kama maji , afya, na elimu ikibidi huko kungepelekwa vivuko tu ambavyo bado vingeendelea kukuza pato la taifa huku vikijiendesha vyenyewe wakati tunasawazisha kwanza huku kwenye maji na afya na baada ya kuweka mambo sawa huko ndio turud sasa kwenye madaraja hayo.
Mnaosema daraja hilo halina impact kiuchumi nina hakika hampafahamu Busisi na huenda hata Mwanza pia hamuifahamu and may be hata Geography pia kwenu ni changamoto; kwangu mimi daraja la Kigamboni ni la starehe Zaidi na kupendezesha mji wa Dar kuliko la Busisi. Iko hivi, ferry ya Busisi kama ilivyo ferry ya Kigamboni ni sehemu inayo unganisha mikoa, sio RAS kama ilivyo Kigamboni, Mwanza mjini inatenganishwa na ziwa, mikoa inatengwa na ziwa ni Geita, wilaya ya Sengerema, Kigoma, Kagera/Bukoba but again nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na hata Congo kwa kupitia Goma, Bukavu; hawa watu kama wanataka kuingia Tanzania kwa kupitia Mwanza ni LAZIMA wapite kivuko cha BUSISI; umbali huo wa kutoka ng'ambo ya Sengerema to Mwanza mji (Kigongo ferry to Busisi ) ndio hizo 3.12 km, sio sawa na magogoni to Kigamboni ambako sidhani kama zinazidi hata mita 200. Mikoa na nchi nilizozitaja, zinafanya sana biashara na Mwanza kwa saa 24; sometimes watu mnaweza kua mnampinga mhe Magufuli kwa kila kitu but sio kwa daraja, daraja lile litaimaisha uchumi wa Tanzania na nchi jirani. Nani asiyejua kule mwanza watu wanakwenda Uganda kila siku kufata bidhaa? Nani asiyejua kama Uganda, Rwanda, Burundi wankuja kuchukua mizigo mingi ikiwepo chakula Tanzania? Waganda, Rwanda na Burundi hawaendi Dar kufata chakula, wanakwenda Mwanza, Kigoma, Geita nk kufata chakula. Tutumie zaidi busara katika kujenga HOJA kuliko kujazana CHUKI. Elimu, afya nk vyote vina umuhimu but haitakuja kutokea duniani kote kwamba uachane na vitu vinavyo endeleza uchumi uka base kwenye elimu na afya pekee, Maisha mengine pia lazima yaendelee, hao Waganda, Rwanda, Burundi wakija Mwanza wataleta pesa, serikali itapata kodi na hiyo kodi itaendeleza elimu na afya.
 
Akianzaga route za huko utasikia ghafla yuko chattle kajificha. Tuendelee kunawa mikono kwa vitakasa
 
Akianzaga route za huko utasikia ghafla yuko chattle kajificha. Tuendelee kunawa mikono kwa vitakasa
Kwani ni kosa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwenda nyumbani kwao/kwake kusherehekea sikukuu za Krismass na Mwaka mpya kwa wazazi wake? .. au ni kosa kwa watu mfano hao mnaowaita "wa Kaskazini" kurudi kwao mwishoni wa mwaka kula sikukuu?!
 
Back
Top Bottom