Rais Magufuli aagiza daraja la Busisi limalizike kwa miaka 3 na sio 4. Awataka Wananchi kuongeza kulima

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,382
2,000
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewataka Watanzania kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kulima mazao ya biashara ili kuweza kuziuzia nchi zinazokabiliwa na janga la Corona, huku akimtaka mkandarasi wa daraja la Kigongo Busisi kuimaliza kazi hiyo ndani ya miaka mitatu na sio miaka minne.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumatatu, Desemba 28, 2020 wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika daraja hilo linalotarajia kukamilika kwa gharama ya bilioni 700.

“Watanzania tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na janga la Corona na tulime kwa nguvu zote ili kukuza uchumi wa nchi na watu kwa ujumla,mazao mtakayolima tutaziuzia nchi zinazokabiliwa na Corona maana watu wao hawafanyi kazi wapo kwenye karantini,” amesema Magufuli.

Amesema wananchi walime sana maana mwakani nchi inaweza kukabiliwa na janga la njaa,kutokana na nchi nyingi zitahitaji chakula kutoka Tanzania.

Aidha, Magufuli amemtaka mkandarasi wanayejenga daraja la Kigogo Busisi wa Kampuni ya China Civil Engineering Group Limited kwa gharama ya Tsh. bilioni 700, kujenga miradi huo usiku na mchana ili kukamilisha ndani ya miaka mitatu, maana ilitakiwa iishie.kwa muda wa miaka minne.

Daraja hilo la Magufuli lenye urefu wa kilo mita 3.2 na barabara unganishi 1.66 kilo mita, ambalo ni la kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwa kukuza uchumi wao.
 

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
802
1,000
Ingawa sina hakika kama daraja hilo kwa urefu huo ni potential kiasi hicho hadi litumie pesa nyingi kiasi hicho wakati bado kuna changamoto nyingi sana sekta ya afya na elimu ambazo ni potential zaidi.

Nadhani Mh. Anapambana kuacha historia yenye kuvunja record.
 

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,445
2,000
Hivi kwa kuwaharakisha haiwezi kuleta athari hasi kwenye ufanisi na ubora wa kazi?
Ndo nawaza hapa. Kwanini wapewe kandarasi ya miaka minne halafu wao watumie mitatu? Hii nchi hii!!!

Halafu hili suala la Corona natamani akae kimya aachane na kulisemea semea. Watu wanaumwa sana na wengine wanakufa sana tena ghafla ghafla tu na ushahidi upo ila yeye kusema kila siku haipo.
 

skillers

Member
Dec 18, 2020
59
125
Unadhani hatumii wataalamu? Hiyo ni idara aliyo kaa na kuiweza kwa miaka,hata mkandarasi atakua anajua miaka mi3 ni mingi iwapo kila kitu kipo kwa nini apoteze muda
Na kwanini wakati wa kusaini kandarasi walikubaliana miaka minne ilhali walijua ni possible kukamilika kwa miaka mitatu?
 

skillers

Member
Dec 18, 2020
59
125
Ndo nawaza hapa. Kwanini wapewe kandarasi ya miaka minne halafu wao watumie mitatu? Hii nchi hii!!!
Halafu hili suala la Corona natamani akae kimya aachane na kulisemea semea. Watu wanaumwa sana na wengine wanakufa sana tena ghafla ghafla tu na ushahidi upo ila yeye kusema kila siku haipo.
Kwa kweli hapo lugha gongana tu

Hilo la corona unaweza kulitolea ufafanuzi vizuri mkuu?
 

skillers

Member
Dec 18, 2020
59
125
Mkataba unasemaje? Kubadili unilaterally terms & conditions za mkataba baada ya ku sign ni halali? Je, hakutakuwa na athari ya kifedha, ubora wa kazi?
Good question, ngoja tusubiri wajuvi watufafanulie
 

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
802
1,000
Ingawa sina hakika kama daraja hilo kwa urefu huo ni potential kiasi hicho hadi litumie pesa nyingi kiasi hicho wakati bado kuna changamoto nyingi sana sekta ya afya na elimu ambazo ni potential zaid.

Nadhani Mh. Anapambana kuacha historia yenye kuvunja record.
 

share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
5,600
2,000
Kama namuona maalim seif naye akipiga makofi huko alipo Ikulu Zanzibar.
 

Mromboo

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,445
2,000
Ufipa hamna jema!
Jema kwenu huko Lumumba ni kuharakisha miradi ya miaka minne ijengwe kwa miaka mitatu bila kujali muda uliowekwa ni makusudi ili kulinda ubora wake. Au mmekosa chakuzindua mnawashwawashwa. Ila alisema akitoka madarakani kabla halijamalizika akija mwingine linaachwa. Anajua kabisa ni mradi ambao hauna tija tofauti na kuchezea hela za walipa kodi.
 

Kibereko

JF-Expert Member
Sep 26, 2018
248
1,000
JK aliomba suma JKT kupendekeza kujengwa nyumba aliyotakiwa kukabidhiwa taratibu isije ikaja kubomoka. Aliona mbali. Nimekumbuka pia zile hostel za chuo kikuu dar.
Bado kuna zile Kota za magomeni zinazijengwa na hao Suma JKT, nina mashaka sana na ubora wake .
 

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
802
1,000
Ufipa hamna jema!
Hili la daraja hapana hata mimi napingana nalo hakuna potentialities zozote kwenye daraja hili na hasa kwa ukubwa wake na gharama zake za ujenzi , maana kwa hesabu ya kawaida serikali inatumia pesa nyingi sana kwenye daraja hili wakati sio daraja la kibiashara hivyo halita kuwa na return kiuchumi badala yake kupelekwa kivuko ambacho kingechangia sana pato la taifa

ni sawa tu na daraja la kigamboni , hayo yote hayakuwa na ulazima sana wa kuyajenga kabla ya kutatua kwanza changamoto ambazo zipo sekta nyeti kama maji , afya, na elimu ikibidi huko kungepelekwa vivuko tu ambavyo bado vingeendelea kukuza pato la taifa huku vikijiendesha vyenyewe wakati tunasawazisha kwanza huku kwenye maji na afya na baada ya kuweka mambo sawa huko ndio turud sasa kwenye madaraja hayo.
 

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
802
1,000
Jema kwenu huko Lumumba ni kuharakisha miradi ya miaka minne ijengwe kwa miaka mitatu bila kujali muda uliowekwa ni makusudi ili kulinda ubora wake. Au mmekosa chakuzindua mnawashwawashwa. Ila alisema akitoka madarakani kabla halijamalizika akija mwingine linaachwa. Anajua kabisa ni mradi ambao hauna tija tofauti na kuchezea hela za walipa kodi.
Kitu ambacho huwa kinanisikistisha wakati wote ni watawala kutumia pesa za umma kukidhi matamanio yao badala ya kushuhulika na vipaumbele na changamoto zinazo wakabili wananchi moja kwa moja katika mazingira yao.
 

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
492
500
Ingawa sina hakika kama daraja hilo kwa urefu huo ni potential kiasi hicho hadi litumie pesa nyingi kiasi hicho wakati bado kuna changamoto nyingi sana sekta ya afya na elimu ambazo ni potential zaid.

Nadhani Mh. Anapambana kuacha historia yenye kuvunja record.
Dkt John Pombe Magufuli anaacha rekodi kubwa kuwahi kutokea - sasa sekta binafsi zione umuhimu wa kutumia miundombinu hiyo kwa ajili ya kukuza uchumi

Daraja la Busisi ni muhimu na limejengwa kwa ndogo sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom