Rais Magufuli aagiza daraja la Busisi limalizike kwa miaka 3 na sio 4. Awataka Wananchi kuongeza kulima

Kwani ni kosa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwenda nyumbani kwao/kwake kusherehekea sikukuu za Krismass na Mwaka mpya kwa wazazi wake? .. au ni kosa kwa watu mfano hao mnaowaita "wa Kaskazini" kurudi kwao mwishoni wa mwaka kula sikukuu?!
Take it easy mzee. Sio kila kitu upayuke
 
inaweza kuwa km Hostel za UDOM expanded joint
ghorofa ikijengwa zile nguzo na beam huwa zinakaa miezi 6 kukauka na kumwagiliwa
sasa km usiku na mchana muda wa kukauka ni ule ule
Hivi daraja la Ubungo, stand ya Mbezi ile barabra ya Kimara Kibaha walikovunjiwa nako muda umepungua au umeongezeka sijasikia kufunguliwa, au epansion joint haziungi?
Maswali ni mengi hakika
 
Hosteli za udsm aliharakisha hivyohivyo na tuliona matokeo yake,Barabara alizojenga tuliona zilivyosumbua ukarabati. Subira ni muhimu tusiharakishe mambo yamsingi kutafuta sifa binafsi tatizo ni wasiwasi linaweza zinduliwa awamu ya sita ajikute kagawana sifa na huyo ajaye...
Alafu hamna cha mkakati hapo alikoswakoswa kuzama ndomana anajenga na kupotezea mabilioni yetu humo? angeyatumia kujenga hospitali au kwenye miradi ya maji angesaidia watu wengi sana! Hii nchi rais asiruhusiwe kujiamulia miradi mikubwa kuzidi bilioni 50 ambayo haijapitishwa bungeni (bunge lenyewe sasa...)
Labda atakuwa anajua analolizungumza kama watu wanavyo sema maana nae ni taaruma yake, japo kuwa inatilia shaka na kufikirisha sana
 
Hajawaharakisha, bali ameaagiza wafanye kazi usiku na mchana
Suala la kufanya kazi usiku na mchana ni kawaida sana kwa wakandarasi (kama umewahi kupitia construction site yoyote utakuwa umewahi kuona) tunacho hofia sio nguvu kazi kuongezeka kwa sababu hilo ni possible kabisa naliko ndani ya uwezo wetu hofu zilizopo ni hizi mbili mkuu

1. Hofu ya kuweza kuongezewa gharama tofaut na awali kwa sababu kuna mabadiliko kwenye mkataba ambao unatupa favor zaidi sisi

2. Kuna maswala kwenye ujenzi hayawezi kuharakishwa ni lazima yapewe muda (mfano muda wa nguzo kukauka).

Hapa ndipo swali lilipo jitokeza kwamba hayawezi kuathiri ubora wa kazi au kuongeza gharama.
 
Ingawa sina hakika kama daraja hilo kwa urefu huo ni potential kiasi hicho hadi litumie pesa nyingi kiasi hicho wakati bado kuna changamoto nyingi sana sekta ya afya na elimu ambazo ni potential zaidi.

Nadhani Mh. Anapambana kuacha historia yenye kuvunja record.
Huwezi jua kama hutumii hiyo njia
 
Hili la daraja hapana hata mimi napingana nalo hakuna potentialities zozote kwenye daraja hili na hasa kwa ukubwa wake na gharama zake za ujenzi , maana kwa hesabu ya kawaida serikali inatumia pesa nyingi sana kwenye daraja hili wakati sio daraja la kibiashara hivyo halita kuwa na return kiuchumi badala yake kupelekwa kivuko ambacho kingechangia sana pato la taifa

ni sawa tu na daraja la kigamboni , hayo yote hayakuwa na ulazima sana wa kuyajenga kabla ya kutatua kwanza changamoto ambazo zipo sekta nyeti kama maji , afya, na elimu ikibidi huko kungepelekwa vivuko tu ambavyo bado vingeendelea kukuza pato la taifa huku vikijiendesha vyenyewe wakati tunasawazisha kwanza huku kwenye maji na afya na baada ya kuweka mambo sawa huko ndio turud sasa kwenye madaraja hayo.
Daraja hili ni la kimkakati kiuchumi lina beba uchumi wa Burundi,Rwanda,Uganda, DRC na Kenya na kuunganisha na Tanzania. Huyo anayesema halina maana hajui.
 
Na kwanini wakati wa kusaini kandarasi walikubaliana miaka minne ilhali walijua ni possible kukamilika kwa miaka mitatu?
Miaka 4 ni maximum. Akiweza kukamilisha unjezi miaka 2 ni credit kwa huyo contractor na tungempa mradi mwingine. Miaka 2 inawezekana kabisa kama kazi ikafanyika mchana na usiku kwani kisio la miaka 4 lilikuwa ni la kufanya kazi mchana tu kama ilivyo kawaida. Haya mengine ya kufanya mchana na usiku ni ombi tu la rais kwa mkandrasi huu. Halazimiki kulikubali. Uzuri kalikubali baada ya kuhakishiwa pesa ipo. Hii ni biashara. Hata mimi au wewe ungalikuwa ni huyo mkandarasi si ungaliona ni neema hiyo. Ungalitaka ku mu- impress rais huyo kwa kuimaliza kazi hiyo kwa supersonic speed na kwa kiwango cha juu sana ili uendelee kupata kandrasi zingine nyingi kwenye nchi hiyo. Kumbuka mkandrasi anayejenga daraja hili ni huyo huyo anayejenga daraja la Tanzanite bridge aka Selender bridge huko DSM. Kumbuka kuwa hawa ma main contractors huwa wana uwezo wa kuweka ma sub contractors wa idadi ya kulingana na speed anayotaka ili mradi pesa iwepo.
 
Na kwanini wakati wa kusaini kandarasi walikubaliana miaka minne ilhali walijua ni possible kukamilika kwa miaka mitatu?
Kwa kuwa limepewa jina la mkuu itawezekana hata kwa miaka miwili...
 
Mnaosema daraja hilo halina impact kicuhumi nina hakika hampafahamu Busisi na huenda hata Mwanza pia hamuifahamu and may be hata Geography pia kwenu ni changamoto; kwangu mimi daraja la Kigamboni ni la starehe Zaidi na kupendezesha mji wa Dar kuliko la Busisi. Iko hivi, ferry ya Busisi kama ilivyo ferry ya Kigamboni ni sehemu inayo unganisha mikoa, sio RAS kama ilivyo Kigamboni, MWanza mjini inatenganisha na ziwa, mikoa inatengwa na ziwa ni Geita, wilaya ya Sengerema, Kigoma, Kagera/Bukoba but again nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na hata Congo kwa kupitia Goma, Bukavu; hawa watu kama wanataka kuingia Tanzania kwa kupitia Mwanza ni LAZIMA wapiti kivuko cha BUSISI; umbali huo wa kutoka ng'ambo ya Sengerema to Mwanza mji (Kigongo ferry to Busisi ) ndio hizo 3.12 km, sio sawa na magogoni to Kigamboni ambako sidhani kama zinazidi hata mita 200. Mikoa na nchi nilizozitaja, zinafanya sana biashara na Mwanza kwa saa 24; sometimes watu mnaweza kua mnampinga mhe Magufuli kwa kila kitu but sio kwa daraja, daraja lile litaimaisha uchumi wa Tanzania na nchi jirani. Nani asiyejua kule mwanza watu wanakwenda Uganda kila siku kufata bidhaa? Nani asiyejua kama Uganda, Rwanda, Burundi wankuja kuchukua mizigo mingi ikiwepo chakula Tanzania? Waganda, Rwanda na Burundi hawaendi Dar kufata chakula, wanakwenda MWanza, Kigoma, Geita nk kufata chakula. Tutumie Zaidi busara katika kujenga HOJA kuliko kujazana CHUKI. Elimu, afya nk vyote vina umuhimu but haitakuja kutokea duniani kote kwamba uachane na vitu vinavyo endeleza uchumi uka base kwenye elimu na afya pekee, Maisha mengine pia lazima yaendelee, hao Waganda, Rwanda, Burundi wakija Mwanza wataleta pesa, serikali itapata kodi na hiyo kodi itaendeleza elimu na afya.
Kwamba feli inazuia hizo biashara kufanyika au? Hebu onyesha kimahesabu badala ya hisia ku justify bln 700 kwa kudaraja hicho ukilinganisha na kutandaza lami kwa km 700 ,,hapo unazungumzia Kigoma- Tabora,, Kigoma-Kagera,,Kigoma-Katavi na Mbeya-Tabora au Songea-Ifakara-Mikumi

Sasa wewe kwa akili zako barabara maeneo niliyotaja hapo juu na hako kadaraja kipi ni potential kwako au unashabikia tuuu kwa vile ni kwenu? Hamna akili huko ccm ndio maana mumejenga maviwanja ya ndege mkoani yamebakia kuota nyasi
 
Daraja hili ni la kimkakati kiuchumi lina beba uchumi wa Burundi,Rwanda,Uganda, DRC na Kenya na kuunganisha na Tanzania. Huyo anayesema halina maana hajui.
Acha ujinga wewe kiazi,kwa hiyo kwa kutumia ferry kuvusha magari na mizigo nk huo uchumi umekwama? Hebu tueleze hasara inayopatikana kimahesabu basi

Wakati unawaza unatakiwa ujue kwamba hiyo bln 700 unajenga vituo vya afya vipya 1400,,km 800 za lami na unasambaza maji ya uhakika jiji zima la Dodoma au Unajenga plant ya Umeme wa maji 1 kama ile ambayo Rais wenu alikuwa abatembeza bakuli kwa Rais wa China nk nk

Sasa linganisha hayo niliyotaja hapo juu na hicho kidaraja kipi kinatija kubwa kiuchumi
 
Back
Top Bottom