Rais Kikwete; Watanzania tukukumbuke kwa lipi ulilotufanyia?

Rais aliyewadharau walimu kupita kiasi,mwenye kutumia cheo kufunga wanamuziki,anayeogopa kwenda Mby,mbinafsi,anayependelea,hashauriki,muongo,muoga,aliiba pesa za EPA,aliyeangusha uchumi,anayejaza ndg zake NEC kwa uchache tu.
 
Kuifanya Tanzania kuwa kituo kikubwa cha madawa ya kulevya"
 
hili swali Kikwete aliulizwa na Fm kibonde pale Serena wakati wa uchaguzi 2010, " unataka watanzania wakukumbuke kwa lipi?"
mh. akajibu "nimewatoa hapa nimewapeleka pale"
binafsi nilishtuka saana, yeye mwenyewe hana chochote cha kujivunia, ww utakaye msifia utamsifu kwa lipi. nyambafu....

Umenifanya nicheke kweli, duu! Anyway, mi pia nitamkumbuka kwa kuufanya urais wa Tanzania kila mtu anauweza cause hata yakitokea matatizo we unaweza kua nje ya nchi na yakaisha by Auto!
 
Mi nitamkumbuka kwa tabasamu lake zuri lisilo na mipaka.....hadi msibani anatabasamu tu!!!!!!!!!
 
Chuo kikuu dodoma
Cha mkopo kutoka kutoka mashirika ya mafao ya uzeeni ya wafanyakazi. Pesa ambayo serikali haielewi italipa vipi. Wakati huo huo inamwaga mihela kwenye mikataba ya hovyo hovyo km. DOWANS, IPTL, Meremeta etc!
 
Tembea utaona Mh.Jakaya Kikwete aliyoyafanya..wewe umekaa tu ukiamka ubungo kariakoo hadi unamaliza mwaka...tatizo lenu mnadhani nchi ipo Dar es salaam peke yake..tembeeni muone Kikwete aliyoyafanya nchi hii.Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni banaa!!
 
Kaka wewe ndio unaleta propaganda, sisi tuliopo Kigoma tunamshukuru kwa kutuletea lami, mojawapo toka Mnanila hadi Kigoma mjini. Tushukuru jamani tusiwe wabishi kwa itikadi zetu, tuseme ukweli.
Hivi kumbe Kigoma siku hizi ni lami?? Labda lami za huko huko ndani kwa ndani kwenda Burundi...

Pia ujenzi wa barabara umechukua miaka 55 na hivyo kuwafanya muwe nyuma sana kimaendeleo, kama ungekuwa na akili kama watu wa Kigoma walivyo ungeyalaumu sana haya MaCCM kwa kuchelewesha miundombinu kwa miaka 55

By the way kama unalipa kodi hutakiwi kuishukuru serikali kwa kutimiza wajibu, labda kwa kuwa Kigoma ni miongoni mwa mikoa inayotumia hela nyingi za bajeti kuliko makusanyo kutoka kwenye vyanzo vya huko
 
Tembea utaona Mh.Jakaya Kikwete aliyoyafanya..wewe umekaa tu ukiamka ubungo kariakoo hadi unamaliza mwaka...tatizo lenu mnadhani nchi ipo Dar es salaam peke yake..tembeeni muone Kikwete aliyoyafanya nchi hii.Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni banaa!!
Acha uongo wako,,, hapa sio Dar es salaam...

View attachment 85651

Ni maendeleo hayo au mateso kwa hawa watoto. Karne hii walitakiwa wawe wanawaza Playstation au Nintendo Wii baada ya kutoka shule. Nyie MaCCM mnawafanya wawaze watakula nini na Kikwete wenu
 
Rais pekee aliyetoa uhuru wa kila mwananchi kuongea na kusema atakacho.Hili limetusaidia kujua kua watanzania tukipewa uhuru tunalewa
 
1. Rais mwoga kufanya maamuzi kuliko wote waliowahi kuwepo
2. Rais asiye na job description hivyo kumkosesha kujua vipaumbele vyake ni nini
3. Rais ambaye kila kona ya nchi ukipita utaambiwa huyu ni mtoto wa "..."
4. Rais aliyevunja record ya kuanguka anguka majukwaani kwenye kampeni zake zote za Urais
5. Rais mtalii zaidi duniani
6. Rais aliyemilikisha mali za nchi kwa familia yake
7. Rais ambaye kila mwanafamilia wake ni mwanasiasa wa CCM na NEC imejaa ndugu na jamaa zake akiwemo mke na mtoto
8.

8.kupiga picha na wasanii.
9.udini (kutekeleza mkakati wa kuteua waislam wazake)
10.Anayecheza cheza hovyo mbele za watu
 
Huu uzi hapa JF ni kama gazeti la mwanahalisi na ile habari ya Ramadhan Ighondu wa TISS.
 
yapo mazuri ya kumkumbuka. yapo. kama tukiwa wakweli wa nafsi zetu, sio kwa chuki yoyote, yapo ya kumkumbuka tena mazuri. lakini kama shilingi yenye pande mbili, yapo mabaya pia ya kumkumbuka. ili upate hayo lazima uwe objective na sio subjective katika kufanya analysis. ukisema hakuna alilolifanya wewe utakuwa muongo na na mnafiki na dhambi hiyo iatakutafuna mpaka kaburini. ukisema kwa kumsifia kana kwamba ni malaika, wewe pia utakuwa mwongo, mnafiki unaejipendekeza na dhambi hiyo itakuandama mapka kaburini. fanya utaffiti wa kisayansi afu ndipo useme.
 
Tembea utaona Mh.Jakaya Kikwete aliyoyafanya..wewe umekaa tu ukiamka ubungo kariakoo hadi unamaliza mwaka...tatizo lenu mnadhani nchi ipo Dar es salaam peke yake..tembeeni muone Kikwete aliyoyafanya nchi hii.Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni banaa!!

wewe cc tunaijua tz zaidi yako+kikwete wako,amefanya nini kama si kuwa nyuma ya udini unao itesa nchi leo???? Serikali ya mauaji ya raia? safari za nje wakati taifa liko kwenye majonz makubwa? serikali ya kishikaji ? Mikataba ya dowans na richmond? Mgawo wa umeme? Mass failure form four? Ufisadi na wizi wa nyara za serikali mchana kweupe? Madaraka ya kiundugu ? Ukandamizaji wa demokrasia? 8 bits thinking capacity? 1 KB reasoning and argumentation? POOR KIKWETE ...POOR CCM.
 
Back
Top Bottom