naninibaraka
JF-Expert Member
- Oct 13, 2011
- 910
- 668
Mh. Rais wangu,nikupongeze kwa kuchaguliwa kumaliza awamu yako ya pili na ya mwisho kabla hujaanza kuitwa mstaafu,ni ahadi nyingi sana ulizotuahidi watanzania mwaka 2005 na baadaye 2010.
Kwa mtizamo wangu kipingi ulichokaa madarakani ni kirefu zaid kuliko kipindi ulichobakiza kumalizia mda wako.
Hoja yangu ni kuwa kama ni vigumu kwa muda uliobaki kufanya lolote la kukumbukwa na watanzania,watanzania tumekata tamaa ya maisha,hakuna wa kutuma matumaini kwa siku zijazo baba umekaa kimya,nchi imekatikatika kwa mijadala isiyoisha.
Mh. Rais, 10yrs bila maendeleo ni jambo gumu ambalo athari zake kwa jamii ni kubwa!,kwa madogo uliyofanya kama kwenye michezo tutakukumbuka daima!
Naomba kuwasilisha.
Kwa mtizamo wangu kipingi ulichokaa madarakani ni kirefu zaid kuliko kipindi ulichobakiza kumalizia mda wako.
Hoja yangu ni kuwa kama ni vigumu kwa muda uliobaki kufanya lolote la kukumbukwa na watanzania,watanzania tumekata tamaa ya maisha,hakuna wa kutuma matumaini kwa siku zijazo baba umekaa kimya,nchi imekatikatika kwa mijadala isiyoisha.
Mh. Rais, 10yrs bila maendeleo ni jambo gumu ambalo athari zake kwa jamii ni kubwa!,kwa madogo uliyofanya kama kwenye michezo tutakukumbuka daima!
Naomba kuwasilisha.
Jakaya Mrisho Kikwete mwana wa msoga anastaafu, -anaacha taasisi ya Urais anaacha Serikali na hatimae ataacha Chama...
Kama ilivyo Ada kuwa kila anayemaliza atakumbukwa nae tutamkumbuka. Kwa maana nae ataacha kumbukumbu iwe mbaya ama nzuri, wapo watakaolia kwa furaha kuondoka kwake na watakaolia kwa majonzi kwamba hawajui kesho yao...
Kikwete atakumbukwa kwa mambo makubwa na mazuri aliyowafanyia Watanzania lakini vilevile wapo wataomkumbuka kwa jinsi alivyowaangusha kwa kutenda kinyume cha ahadi zake na kaulimbiu zake za Ari mpya, Kasi Mpya na Nguvu mpya na ya Maisha bora kwa kila Mtanzania.
Watanzania wa kada mbalimbali wanazo sababu za kumkumbuka Rais Kikwete atakapong'atuka madarakani. Hii itatokana na jinsi walivyonufaika au kuumizwa kwa namna moja ama nyingine na utawala wake.
WANAWAKE:
Watamkumbuka Rais Kikwete kwa jinsi alivyothamini mchango wao na uwezo wao kiutendaji.
Ktk Awamu ya nne, Rais aliongeza kasi ya kuwaamini na akawateua kwa wingi baadhi yao kuingia kwenye vyombo vya uamuzi kama uwaziri, Ukuu wa mikoa na wilaya na nafasi za uwakilishi.
Ktk kipindi chake idadi ya majaji wanawake iliongezeka, ikiwamo hata kufanikisha Anne Makinda kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya juu ya Uspika wa Bunge.
Swali ninalojiuliza ni je.., atawaachia zawadi wanawake kwa kupendekeza mmoja wao kuwa mgombea urais..???
VIJANA:
Kundi hili nalo litakuwa na kila sababu ya kuhuzunika KIKWETE atakapoondoka madarakani. Hii ni kwa sababu kila alipofanya uteuzi, hakuwaacha vijana.
Tangu alipojitosa katika kinyang'anyiro cha urais kwa mara ya kwanza mwaka 1995, Mkakati wake ulikuwa kuwapa vijana fursa za uongozi na aliposhinda mwaka 2005 aliwateua bila hofu katika nyadhifa mbalimbali
WAZEE:
Mbali na kuendelea kuamini busara za wazee, kila alipotaka kutangaza jambo zito au kutoa hotuba ya mwisho ya mwezi iliyotikisa nchi, alikutana na wazee wa Dar es salaam au Dodoma. Lakini vile vile wazee wamo katika nafasi mbalimbali za uongozi, uwaziri, ukuu wa wilaya na Mikoa.
WAZANZIBARI:
Rais Kikwete alijitahidi kadri ya uwezo wake kupatanisha wananchi wa unguja na pemba waliotofautiana kwa misingi ya siasa.
Chini ya ushawishi wake Wazanzibari walikubali kuongoza nchi kwa ushirikiano, wakaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. UHASAMA uliondoka japokuwa kuna viashiria vya uhasama kurudi.
WASOMI
Hakuacha nyuma kundi la wasomi, kwani miongoni mwao ndio wanaoongoza wizara nyeti na taasisi mbalimbali. Aliwateua katika nafasi mbalimbali za uongozi japokuwa baadhi yao wamemwangusha.
Atakumbukwa alivyohamasisha ujenzi wa shule za Sekondari kukidhi ongezeko kubwa la wanaofaulu kutoka shule za msingi na alivyojenga chuo kikuu cha Dodoma, upanuzi wa Chuo Kikuu huria na vyuo vya kati.
WANACHAMA WA CCM.
Tofauti na vyama vingine vya siasa, CCm wanajivunia kumpata mtu aliyekuwa kete ya ushindi kwa vipindi viwili mfululizo 2005 - 2010 na 2010 - 2015.
Watamkumbuka alivyowabeba, alivyofanyia marekebisho katiba ya chama kuwa na wajumbe wa Halmshauri kuu kutoka Wilayani, alivyohuisha chama hadi kuwa na mvuto kuliko awali.
HOFU yao ni je, watampata mgombea ambaye atakuwa KETE ya USHINDI..???