Rais Kikwete; Watanzania tukukumbuke kwa lipi ulilotufanyia?

Kwa kutuondolea jembe mpiganaji wetu mzalendo aliyekuwa katibu mkuu wa wafanyakazi wa reli Sylivester Rwegasira,hakika wazalendo wetu hawana chao kwa J.K

R.I.P kamanda Rwegasira!
 
Tanzania haijawai kupata rais mzuri kama Kikwete.
1.Ametuunganisha na nchi kama USA.Brazil na China 2.Ameendeleza michezo na kuirudisha mashuleni 3.Wananchi waliopata matatizo kama gongo la mboto wamesaidiwa haijawai tokea 4.Umeme na hospitali vimeongezeka kupatikana kwa kila raia 5.Vyuo vikuu vimeongezeka ata wanafunzi kusoma bure huko vyuo vikuu 6.Mishahara wafanyakazi wanapata mizuri tena kwa wakati 7.Ajira njenje kama ualimu,polisi,jeshi etc 8. Amegawa tractors na powertiller,mbolea ya ruzuku duh kweli Kikwete tutakulilia ukiondoka natamani tubadirishe katiba.
 
tutamkumbuka sana,maisha bora kwa kila mtanzania au mumesahau wanajf?tutamkumbuka kuwa rais pekee aliyeahidi ahadi nyingi kuliko marais wote waliostaaaaaaaaaafu
 
Mimi nta mkumbuka kama raisi aliye shindwa kuongoza nchi, kama wakati anaingia madarakani deni la taifa ni trillion 5, leo ni trillion21,kama kiwango cha ufaulu kili kuwa zaidi ya asilimia themanini leo kipo arobaini na, je na wewe utamkumbuka kwa lipi?
 
Mimi nta mkumbuka kama raisi aliye shindwa kuongoza nchi, kama wakati anaingia madarakani deni la taifa ni bill 5, leo ni bill21,kama kiwango cha ufaulu kili kuwa zaidi ya asilimia themanini leo kipo arobaini na, je na wewe utamkumbuka kwa lipi?

Mkuu ni vyema ukasahihisha tread yako kabla hasira hazipanda, deni la taifa limefikia TRILLION 21 na siyo Billion 21 kama unavyo jaribu kupindisha ukweli. Usishtuke mkuu hiyo ndo habari ya mjini na Waziri wa fedha ametangaza rasmi wadanganyika tusiwe na wasi wasi bado tunakopesheka.
 
Mimi nta mkumbuka kama raisi aliye shindwa kuongoza nchi, kama wakati anaingia madarakani deni la taifa ni bill 5, leo ni bill21,kama kiwango cha ufaulu kili kuwa zaidi ya asilimia themanini leo kipo arobaini na, je na wewe utamkumbuka kwa lipi?
Mimi nitamkumbuka kwa kuigawa nchi kwa misingi ya udini na kuuwa msingi wa mshikamano aliouanzisha Mwalimu Nyerere, nitamkumbuka pia kwa kushindwa kumfukuza kazi Edward Hosea hata pale alipomuanika mbele ya majasusi wa kimarekani kwamba hana ubavu wowote wa kupiga vita rushwa! Nitamkumbuka pia kwa kuwa rais anayependa ujiko sana...eti Doctor Kikwete...[pampaf kabisa!
 
Back
Top Bottom