Rais Kikwete safarini Marekani

Rais Kikwete safarini Marekani

source ni ikulu wametangaza na kwenye taarifa ya habari ya saa saba mchana chanel TEN kuwa mkuu wa nchi amekwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake USA hii imekaaje wakuu
 
Rais Kikwete amewasili Dubai usiku jana akiwa njiani kwenda marekani kwa ajili ya matibabu na kufanya check up ya afya yake.

Maafisa wa ikulu wamethibitisha kuwa safari hii ni kwa ajili ya matibabu tu ingawa haijasemwa anasumbuliwa na nini

Ni vema wamekumbuka kumjaza mafuta mapema coz papaaaaa mkulu fast jet alikuwa anaonekana kazidiwa /kalevya na uchovu wa safari za juu kwaju kila kuchao kama popo .. Hongera kina "ulimboka" wake kumtizama afya yake "dhaifu".
 
source ni ikulu wametangaza na kwenye taarifa ya habari ya saa saba mchana chanel TEN kuwa mkuu wa nchi amekwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake USA hii imekaaje wakuu

Hii imekaa vizuri sana. Ni vema kufanya mara kwa mara uchunguzi wa afya ya kiroho na kimwili hata kama haujisikii vibaya.
 
Rais Kikwete amewasili Dubai usiku jana akiwa njiani kwenda marekani kwa ajili ya matibabu na kufanya check up ya afya yake.

Maafisa wa ikulu wamethibitisha kuwa safari hii ni kwa ajili ya matibabu tu ingawa haijasemwa anasumbuliwa na nini

Ni kawaida kwa binadamu kuangalia afya kila wakati, tumwache rais acheki afya yake.cha msingi hapa ni kumwomba Mh Rais kuendelea kuziboresha hosptal zetu,ili huduma nzuri ziweze kupatikana na kupunguza safari za viongozi wetu nje ya Tanzania,hii itasaidia kuwa na huduma nzuri za kiafya hapa nchini kama ilivyo kwa afrika ya kusini
 
Imekaa vibaya kwanini hizo hospitali zisijengwe hapa Nyumbani? kama ni mzalendo angeanza kuunga foleni pale Muhimbili.
 
jK mwenyewe aliwahi kusema kuna watu wanachuki hata ukifanya jambo gani zuri,lkn wao watakuchukia tu,leo ndo nimeamini.
 
Ni kawaida kwa binadamu kuangalia afya kila wakati, tumwache rais acheki afya yake.cha msingi hapa ni kumwomba Mh Rais kuendelea kuziboresha hosptal zetu,ili huduma nzuri ziweze kupatikana na kupunguza safari za viongozi wetu nje ya Tanzania,hii itasaidia kuwa na huduma nzuri za kiafya hapa nchini kama ilivyo kwa afrika ya kusini

Hili ndilo jambo la msingi sana. Tuboreshe hospitali zetu ili na viongozi wetu watibiwe hapahapa Tanzania na sio kutumia gharama kubwa kumsafirisha kwenda kutibiwa Marekani na msafara wa watu 20!
 
Nyerere Miaka 24 Ikulu safari 66 nje ya TZ
JK miaka 8 Ikulu safari 361 nje ya TZ

Anayetetea safari za JK nje ya nchi ana matatizo ya kufikiri!!
Kwenye hilo bandiko la Barubaru imebidi nimgongee 'like', sio kwa kupenda bali kwa machungu ya jinsi baadhi yetu tunavyoichukulia nchi hii. Kwa hakika kusonga mbele itakuwa kazi ngumu.

Sijapendezwa kufananisha matibabu ya South Africa na Tanzania. SA ni ulaya nyingine
 
Anasumbuliwa na S&T allowances!! Ndani ya week mbili tu ................. RSA x2, Kenya, sasa UAE na kesho USA!! Kama kweli ni matibabu kulikuwa na haja gani ya kupitia huko Dubai. Au anataka kudai ana save pesa za walipa kodi kwa cheap tickets za Emirates!!??
Kwa kuwa alikuwa RSA, kwa nini hakufanya hiyo check-up pale Millipark alikolazwa Mgimwa na kuokoa kiasi kikubwa cha pesa ya walala hoi?
 
Hivi kwann tusijenge ikulu nyingine marekani huyu mzururaji akakae huko?

wiki moja trip zaidi ya tano?

Hivi marekani hawana sera ya kukamata wazururaji kama hawa?
hahahahahahahaha JF kweli kiboko!!!
 
mandela alikuwa mjanja hakwenda Ulaya au Marekani kutibiwa
alijua akienda huko hatarudi kama Nyerere,,,

alichofanya ni kuhakikisha kuna hudua bora za afya nchini mwake
JK watu unaowaongoza nao wakachekiwe afya zao wapi?Ulaya au Marekani?
serikali ya CCM inatakiwa kuboresha huduma za afya kila kata
wekezeni kwenye afya na elimu..
Mmeshindwa kujenga Apolo Moja Tanzania???

Zile fedha walizowekeza mafisadi uswizi kwanini wasijenge
hospitali kubwa na ya kisasa na ikaajiri madaktari wa Kitanzania na wa nje?
uwezo wa madaktari wetu ni mkubwa tatizo vifaaa....

Je ni halali kwa rais kama kiongozi kutumia kodi yetu kutibiwa nje
huku akiwaacha wananchi wake wakiwa na huduma duni za afya???
Kiwango anachokitumia kwa wiki nzima huko na aliofuatana nao kingejega zahanati ngapi?

nani katuloga tukakosa upeo wa kufikiria?
bora hata Ikulu wasingetangaza hii habari wangekaa kimya.
wazungu wanatucheka kwa vile tumekosea upeo wa kufikiri,
viongozi wametutelekeza, hata kuchekiwa afya lazima iwe nje?? terrible
KAZI TUNAYO.. inaniuma sana kwa sisi walalahoi
 
Ivi nako marekani anapokelewa kiheshima au washamzoea wanahisi a nigger in the next street!!
 
Nyie pro-Chadema najua mna chuki sana na rais wetu JK hata kama anakwenda kutibiwa tatizo lipo wapi acheni unafiki basi, juzi hapa kiongozi wenu Dr.Slaa kaongozana na girlfriend wake Josephine kwenda Ujerumani kuangaliwa afya mlishangilia sana leo JK mnaanza kuponda acheni siasa za makengengeza.
Why US, while UDOM and MMC can perform blood exchange at (the) fraction of the costs ???
 
Rais Kikwete amewasili Dubai usiku jana akiwa njiani kwenda marekani kwa ajili ya matibabu na kufanya check up ya afya yake.

Maafisa wa ikulu wamethibitisha kuwa safari hii ni kwa ajili ya matibabu tu ingawa haijasemwa anasumbuliwa na nini

Mara zote anazoenda kutibiwa haisemwi!!!!
 
Kwa kuwa alikuwa RSA, kwa nini hakufanya hiyo check-up pale Millipark alikolazwa Mgimwa na kuokoa kiasi kikubwa cha pesa ya walala hoi?
Wengine huwa wanasema 'ningekugongea likes 1m'. Hoja yako ni ya msingi sana katika suala zima la uzalendo maana Afrika Kusini hawajafikia USA lakini wanawakaribia kwa matibabu. Huenda suala sio check-up ila kuna kingine lakini wanatudanganyia hiyo.
Kwa wale watakaokuwa wanalalamikia hili suala basi wataweza kupozwa endapo wataambiwa anagharamia hii safari mwenyewe lakini kama ni pesa za kodi za Watanzania basi kuna haki na haki na haja ya kuhoji.

Back
Top Bottom