DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail:
ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENTS OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini leo,
Jumanne, Novemba 18, 2008 kwenda Libya na Ethiopia kwa ziara fupi za kikazi.
Nchini Libya, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa nchi hiyo,
Kanali Mummar Gaddafi juu ya jitihada za kupatanisha mgogoro kati ya nchi za Chad na
Sudan.
Libya pamoja na Congo (Brazzaville) ziliombwa na AU kuzipatanisha nchi jirani za
Chad na Sudan ambazo uhusiano wao umekuwa siyo mzuri kwa muda sasa. Nchi hizo mbili
zimekuwa na mzozo wa kisiasa unaotokana kwa upande mmoja na vita ya Darfur, lakini
pia kutokana na kila moja ya nchi hizo kumtuhumu mwenzake kwa madai ya kusaidia
waasi wa nchi nyingine.
Rais Kikwete ataondoka Libya kwenda Addis Ababa, Ethopia kuhudhuria Mkutano wa Pili
wa Kamisheni ya Afrika Kuhusu Ajira kwa Vijana iliyoanzishwa na Waziri Mkuu wa
Denmark, Bw. Fogh Ramussen. Waziri Mkuu huyo alimwomba Rais Kikwete kuwa mjumbe wa
Kamisheni hiyo inayoshughulikia masuala hayo ya ajira kwa vijana barani Afrika.
Mheshimiwa Rais alikubali kuwa mjumbe wa Kamisheni hiyo ambayo pia mwenyekiti wake
ni Mheshimiwa Rasmussen mwenyewe.
Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano
Ikulu.
Dar es Salaam.
18/11/2008
Mail From Ikulu.go.tz