Rais Kikwete na safari za nje

Rais Kikwete na safari za nje

Hivi ameshaondoka U.A.E...En route to U of ES EI

AU is footing the bill!

Kula Breki!!!
 
This time nafikiri anasababu ya msingi maana ametoka huko two weeks tu zimepita. provided nchi haiingii gharama ya safari hii hakuna tatizo pamoja na kuwa anaacha mambo nyumbani sio mazuri na kwenda huko.
 
Rais Kikwete aenda New York, atahutubia Baraza Kuu UN

2008-09-21 11:34:39
Na Mwandishi Wetu

Rais Jakaya Kikwete ameondoka nchini jana kwenda New York, Marekani, ambako atahudhuria na kuhutubia kikao cha mwaka huu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN).

Rais amepangiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne ijayo, Septemba 23, 2008 katika nafasi yake pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

Mbali na kuhutubia Baraza Kuu, Rais Kikwete amepangiwa kuhudhuria mikutano mingine muhimu kuanzia ule ambao utaangalia Mahitaji ya Maendeleo ya Afrika.

Mkutano huo, utajadili ahadi za nchi tajiri kwa Afrika na Maendeleo ya Bara hilo, na kuona ahadi hizo zinatekelezwa namna gani.

Rais pia atahutubia kikao cha ufunguzi cha viongozi ambao watajadili maendeleo ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG\'s).

Baada ya kuwa amehutubia kikao hicho, Rais atashiriki katika mijadala kuhusu afya ya Mama na Mtoto, na pia mjadala kuhusu ugonjwa wa Malaria, masuala yote mawili yakiwa sehemu muhimu ya MDG`s.

Ijumaa, Septemba 26, Rais atakwenda mjini Washington, ambako atatoa hotuba muhimu ya ufunguzi kwenye Kikao cha Mwaka cha Wabunge Wenye Asili ya Afrika katika Bunge la Marekani, na pia kuhutubia mkutano wa viongozi wa shughuli za biashara katika Marekani.

Mbali na mikutano ambayo amepangiwa kuhutubia ama kushiriki, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wengi wa shughuli za kisiasa, kibiashara na kiuchumi duniani na katika Marekani.

Miongoni mwa viongozi ambao Rais Kikwete atakutana nao na kufanya mazungumzo nao ni pamoja na Rais wa Iran, Mheshimiwa Ahmedinajad; Katibu Mkuu wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Mheshimiwa Javier Solana; na mfanyabiashara maarufu duniani wa shughuli za kompyuta na teknolojia ya mawasiliano, Bill Gates.

Rais Kikwete pia atakutana na Waziri Mkuu wa Denmark, Mheshimiwa Anders Fogh Rasmussen; na Katibu Mkuu wa Shirika la Kazi Dunia (ILO), Juan Somavia.

Rais Kikwete pia atafanya kikao cha pamoja kati yake, Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki Moon na Makamu wa Rais wa Sudan, Ustaz. Ali Osman kuzungumzia mgogoro wa eneo la Darfur nchini Sudan.

Wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili katika Sudan mwanzoni mwa mwezi huu, Mwenyekiti huyo wa AU, alimwahidi Rais Omar El Bashir wa Sudan kuwa angefanya kikao kati yake, Katibu Mkuu wa UN, na mwakilishi wa Sudan kuhusu hali ya Darfur wakati wa Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu.

Kikao hicho kitaangalia jinsi gani ya kuharakisha zoezi la kupeleka askari wa kulinda amani wa UN na AU katika Darfur, na pia jinsi ya kuahirisha, kwa angalau mwaka mmoja, hati ya kukamatwa kwa Rais Bashir iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uharifu (ICC).
  • SOURCE: Nipashe
 
Huo ni uzushi!Umesikia wapi?shirikisha chanzo cha habari!

ni kweli kikwete amesafiri, nakumbuka nimesoma kwenye gazeti na pamoja na kuhudhuria huo mkutano vile vile ataonana na Bill Gates!

this president of urs is 2 much!
 
Nakuunga mkono ka hilo na kwa kuongezea tu, si safari hii tu, safari zote za JK zina maana kwa nchi yetu na nadhani wengi wanalijuwa hilo.

Safari zote za Rais zina maana, may yes lakini za JK zinawalakini fulani Kama mmja ya kazi za rais ni kusafiri then JK hii anaiweza vizuri sana lakini kilio cha wananchi ndiyo kashindwa kukifanyia kazi. Nafikiri kisha gundua akiwa nje anapumzuika kidogo maana ngoma ni zito hajui kuicheza. Alifikiri urais ni rahisi sasa hajui cha kufanya. Mimi simjui raisi yeyeto zaid ya JK ambaye ansafiri kuliko mawaziri wake. Nafikiri hata Ma-PS amewazidi pia.
 
Kwa kuzingatia majukumu rais anayokwenda kutimiza katika safari hii inayojadiliwa hapa, ungependekeza kazi hizi akawakilishwe na PS au waziri gani? Kwa hiyo yeye rais abaki ikulu afanye hizo kazi za ma-PS na mawaziri?
 
Harufu ya Shombo Ikulu mchezo!! Lile soko la samaki pale nyuma haliwezi kuhamishiwa sehemu nyingine?
 
Mtu mzima mwenye afya tele ndiye mwenye uwezo wa kutimiza majukumu yake vema, yakiwamo yale yanayomtaka kusafiri. Ama ninyi mlitaka awe anakaa pale ikulu afanye kazi kwa remote control? Kumbe wapo wanaodhani tumemchagua rais ati awe "anakaa" nyumba ya magogoni? Si lazima mtu kuwa rais ndipo mtu "akae" ndani ya jengo hilo la ikulu, kule kuna wapishi, walinzi na wasaidizi kibao wote "wanakaa" huko. Kazi ya rais siyo "kukaa" ikulu, ni kutimiza majukumu ya urais popote anapohitajika, ndani ama nje ya nchi. Tumechagua rais achape kazi, siyo "kukaa ikulu"! Anastahili rais Kikwete kupewa hongera na pole kwa kazi, anachapa kazi huyu mtu. Kwa nini hatufikirii kuwa huko anakoenda anachoka kwa kuchapa kazi, badala yake watu mnawaza "matanuzi" tu, kumbe wengine mngepewa nafasi kama hiyo mngekuwa mnasafiri kwenda "kutanua" badala ya kuchapa kazi? Nimeshachoka kabisa na hizi blah blah za kuhoji kila safari anayofanya Kikwete, watu wanaendekeza ujuha na ulimbukeni, pengine hata na chuki binafsi zaidi kuliko masuala ya msingi. Upumbavu mtupu!

...Kwa hiyo uchapakazi wake ni lazima iwe trip za nje ya nchi siyo? Tumewawekea nini basi Mabalozi huko nchi za nje kumbe kila katripu kadogo tu ka 'kununua majani ya chai' Raisi anataka aende yeye? Hivi kulikuwa na ulazima gani wa yeye kwenda Marekani wiki mbili tu zilizopita na kumbe alijua kuwa wiki hii alitakiwa kuwa huko tena??Mara ya mwisho alitembelea lini vijiji kumi mfululizo vya nchi yake? Tutajie faida MOJA tu ambayo wewe kama KITHUKU unaamini kabisa kuwa imetokana na trip za nje zisizokwisha za mheshimiwa. MOJA tu na hatutaki bla bla.Halafu matusi ya nini? huna haja ya kuita unachopingana na wenzio kuwa ni ujuha, ulimbukeni na upumbavu. Mimi nadhani limbukeni ni yule mtu anayependa mtu ama kitu kitu mpaka haoni kasoro za wazi kabisa za kitu hicho na yuko tayari kutukana wenzake kwa hilo. Ni hayo tu mheshimiwa.
 
Sawa mkubwa. Na faida za kukaa ikulu ni zipi? Faida za kutembelea vijiji kumi mfululizo nchini ni zipi? Na katika faida hizo, ukilinganisha na zinazotokana na "trip za nje zisizokwisha", zipi faida kubwa au za maana zaidi kwa taifa? Kumbuka kueleza pia kipimo unachotumia katika kutathmini "faida" au "hasara" hizo.
 
mkuu, hizo ndio blah blah nilizosema. wewe umesema kuwa trip za mheshimiwa
za nje zina faida nyingi nikakuomba wewe kama KITHUKU utaje mojawapo tu ya faida hizo, bila longolongo wala nini. Jibu lako ni kuniuliza maswali zaidi. Nikuambie kitu. Raisi anapotembelea kijiji KIMOJA tu cha nchi, achilia mbali kumi, kwa siku ile wale wana kijiji wa kijiji kile achilia mbali ile faraja tu ya kumuona Raisi wao, lakini kwa jinsi tunavyoijua nchi yetu angalau watachongewa barabara ambayo isingechongwa daima dumu, kama kuna bomba lisilotoa maji angalau siku hiyo injinia wa mkoa hatalala mpaka maji yatoke kwenye kijiji kile na angalau mimi na wewe KITUHUKU tutafahamu kuwa kumbe ndani ya nchi kuna kijiji kinaitwa Ugagagigikokoni ambacho wala tulikuwa hatujui kuwa kipo. na tunaposema Raisi angalau atulie pale Magogoni kidogo afanye kazi za nchi hatuna maana kuwa akae kwenye kiti. tuna maana kuwa kuna masuala ambaop kauli yake tu inaweza kuwa ni ufumbuzi.
Hebu fikiria raisi akikaa pale halafu akaona baba na mama zetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakuja kumkalia getini wakitaka haki yao, raisi anaweza kuamrisha kuwa walipwe katika siku mbili tu na wale wote waliokuwa wanalikwaza hili waondoke!! Na Voila! ikawezekana. Oh Yes, He can!
 
Ahamie huko huko US bongo haimfai muungwana...Nchi amwachie Rostamu na Lowassa.

TUWE MAKINI NA MHESHIMIWA SANA ZA COMEDY

Ndugu wananchi mimi ninawasiwasi huyu jamaa atamuuzia Bush Ikulu yetu pale Dar halafu akajenge kasri jingine Chalinze (bagamoyo?), manake hizo safari za USA zimezidi, ikizingatiwa kuwa Bush alimpigapiga mgongoni siku zile alipokuja . Hivyo tuwe makini.
 
mkuu, hizo ndio blah blah nilizosema. wewe umesema kuwa trip za mheshimiwa
za nje zina faida nyingi

Hebu onesha mahali nilipotamka maneno hayo, vinginevyo kuwa tu mstaarabu unitake radhi!

Mimi nimekuchagiza ueleze ni kwa nini unadhani rais kutembelea vijiji kumi au kukaa ikulu ni bora zaidi ukilinganisha na "trip za nje zisizokwisha", na unapotoa maelezo hayo utaje kipimo unachotumia katika tathmini hiyo ili na sisi wengine tutathmini halafu tukitumie kipimo hicho tuone kama tutafikia conclusion kama yako. Ni hilo tu na bado hujanipa jibu. Asante mkuu
 
Hivi hamjajiuliza ni lini mara ya mwisho kwa Rais JK kukaa Ikulu for 2 weeks straight bila kuondoka kwenda mikoani au nje?
 
Hivi hamjajiuliza ni lini mara ya mwisho kwa Rais JK kukaa Ikulu for 2 weeks straight bila kuondoka kwenda mikoani au nje?

Hivi hiyo ndiyo kazi ya rais, "kukaa Ikulu for 2 weeks straight bila kuondoka kwenda mikoani au nje"? Hivi mnayo job description ya rais? Inasema akae ikulu siku ngapi, mikoani siku ngapi na safari za nje siku ngapi katika mwaka?
 
Hebu onesha mahali nilipotamka maneno hayo, vinginevyo kuwa tu mstaarabu unitake radhi!
Mimi nimekuchagiza ueleze ni kwa nini unadhani rais kutembelea vijiji kumi au kukaa ikulu ni bora zaidi ukilinganisha na "trip za nje zisizokwisha", na unapotoa maelezo hayo utaje kipimo unachotumia katika tathmini hiyo ili na sisi wengine tutathmini halafu tukitumie kipimo hicho tuone kama tutafikia conclusion kama yako. Ni hilo tu na bado hujanipa jibu. Asante mkuu

tuanze na hili la kuonyesha ulipotamka maneo ya faida ya safari za mheshimiwa. Sijapaona. Nakuomba radhi.

Nimeishakupa mfano wa hali inavyokuwa pale mheshimiwa anapotembelea kijiji kimoja tu japo zinaweza kuonekana ndogo mno. Kuhusu hili la kulinganisha na faida za trip za nje zisizokwisha naomba nikuambie hivi.

Kuna mambo mengine yanataka common sense tu na sio lazima kutunga msahafu kuyafafanua. Iwapo wewe Kithuku wakati mheshimiwa anaingia madarakani ulikuwa unapokea mshahara wa shilingi Alfu kwa mwezi na ukaweza kununua sukari kilo moja shilingi mia tano (n9i mfano tu, samahani!), raisi wa nchi yako anaposafiri nje mara nyingi zaidi kuliko anavyokaa nchini unategemea faida za safari hizo zijiakisi katika maisha yako ya kila siku kwa maana ya zitawezesha ile kilo ya sukari uinunue kwa shilingi mia nne ama basi ibaki ile ile mia tano.

lakini iwapo baada ya safari zote hizo, ile kilo ya sukari unainunua shilingi 700 huku thamani ya mshahara wako imekuwa ni shilingi mia nane na sio alfu unayopokea na kila kitu kimekuwa worse off than alipoingia madarakani, ni nini sasa faida ya kutembea kwake nje???

Huu ni mfano rahisi kabisa kuliko yote ninaoweza kutumia ili kufafanua hoja yangu. natumaini utauelewa!
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi basi tangu JK ateue Baraza lake jipya la mawaziri, baada ya Lowasa kung'atuka kumekuwa na kikao cha baraza la mawaziri mara moja tu!!!

Ndio maana mambo hayaendi kabisa, kila mtu anajiamua mambo yake kivyake, JK yuko bize na safari za nje, yaani kwa kifupi hakai ofisini kama alivyokuwa anafanya Mkapa.

Tunakwenda wapi? Mbona kila kitu shaghalabaghala tu???? At least Mkapa alikuwa mkali kwa mawaziri wake...Msije na issue ya EPA kwenye hili, kwani EPA zilikuwa ni pesa kwa ajili ya uchaguzi ila tu "watanzania wenye asili ya asia" wakaitumia hiyo nafasi kuchota pesa kupita kiasi!!!!
 
Nimeridhia mkuu, huu ndio ustaarabu, no grudge.

Ukisoma post zangu kuhusu hizi safari za muungwana, utaona ninachosema kimsingi ni kuwa safari hizo ni miongoni mwa majukumu yake kama rais. Sijapata yeyote aliyeweza kunithibitishia kuwa hayo si majukumu yake, ama anaingilia ya wengine, ama anatunga safari zisizo na msingi. Na kufanya kazi pale ikulu na mikoani pia ni majukumu yake kama rais. Lakini sijawahi kusikia kuwa kuna gauge inayoonesha kuwa katika majukumu yote ya rais ni yapi muhimu kuliko mengine, na ni yapi yenye msingi zaidi ama yasiyo na msingi. Ndiyo maana nasema rais anasafiri kutimiza majukumu yanayompasa, sasa kama yupo mwenye ushahidi kuwa anachofanya ni tofauti na hayo aweke hapa tuuchambue.

Kwenye tathmini ya mafanikio ya rais, kupanda ama kushuka kwa uchumi nk, bado hatuna tathmini huru inayoweka mahusiano (causal links) baina ya ufanisi wa kiuchumi na kazi mojamoja anayofanya rais, kwa mfano je alipotembelea Manyara au alipoteua makatibu tawala wapya imechangia kiasi gani kwenye uchumi, hatuna ripoti hizo kwa hiyo hatuwezi kuhukumu. Na hata atakapomaliza muda wake wa urais, ikatokea kuwa uchumi umepanda au umeshuka kuliko wakati alipoingia, bila tathmini huru hatutaweza kusema ni kipi hasa kilicholeta athari hiyo. Kwa hiyo kwa sasa tumwache rais afanye kazi yake, inapobidi tupige kelele pale anapokwenda kinyume na taratibu, sheria, kanuni na katiba ya nchi.
 
JK inaelekea hajafahamu kuwa uraisi ni sawa na kuwa CEO au meneja wa kampuni/kiwanda. Hajui kuwa anatakiwa aonyeshe faida na hasara ya uongozi wake. Nafikiri kwake uraisi ni kama u-priffect mkuu, ambapo kila kiranja anawajibika kivyake bila kuwajibishwa na kiranja mkuu, halafu kipindi chao cha uongozi kikipita wanaagwa tu na wengine kuingia.
  • Sidhani kama anakaa chini na kusoma ripoti na kupanga mwelekeo wa nchi.
  • Sidhani kama anaelewa yale yanayoendelea kwenye wizara zake au kila waziri ni sawa na raisi wa hiyo wizara.
  • Sidhani kama anayo plani yenye milestones za kupimia anakoipeleka nchi zaidi ya kufikiria kuwa kila mtu anajua manifesto ya CCM.
  • Sidhani kama anaelewa kuwa hakuna nchi itakayotupa maendeleo kutokana na misaada ingawa inaelekea kuzunguka kuomba-omba misaada ndio anachofikiria kuwa ndio kazi ya raisi.
  • Sidhani kama anajali kuwa hivi sasa inflation inakaribia 10% na nini kifanyike kuiokoa nchi.
  • Sidhani kama anajali kuwa matumizi makubwa ya safari zake, mkewe, mawaziri na viburudisho vyao vingine ni mzigo mkubwa kwa wananchi.
Ukweli ni wazi kuwa, Kikwete hakustahili kumrithi Mkapa kwani tumerudi nyuma zaidi licha ya mapungufu aliyokuwa nayo Mkapa. Kama walivyofanya ANC kwa kumtaka raisi wao ajiuzulu, au kama Gordon Brown anavyokabiliwa na uwezekano wa kutimuliwa, sijui ni kwa nini wanaokerwa na hali hii ndani na nje ya CCM hawamkabili huyu mkuu kwenye vikao vya CCM au hata maandamano ya wapinzani ili tu angalau ajue kuwa tumemchoka??
 
Nimeridhia mkuu, huu ndio ustaarabu, no grudge.

Ukisoma post zangu kuhusu hizi safari za muungwana, utaona ninachosema kimsingi ni kuwa safari hizo ni miongoni mwa majukumu yake kama rais. Sijapata yeyote aliyeweza kunithibitishia kuwa hayo si majukumu yake, ama anaingilia ya wengine, ama anatunga safari zisizo na msingi. Na kufanya kazi pale ikulu na mikoani pia ni majukumu yake kama rais. Lakini sijawahi kusikia kuwa kuna gauge inayoonesha kuwa katika majukumu yote ya rais ni yapi muhimu kuliko mengine, na ni yapi yenye msingi zaidi ama yasiyo na msingi. Ndiyo maana nasema rais anasafiri kutimiza majukumu yanayompasa, sasa kama yupo mwenye ushahidi kuwa anachofanya ni tofauti na hayo aweke hapa tuuchambue.

Kwenye tathmini ya mafanikio ya rais, kupanda ama kushuka kwa uchumi nk, bado hatuna tathmini huru inayoweka mahusiano (causal links) baina ya ufanisi wa kiuchumi na kazi mojamoja anayofanya rais, kwa mfano je alipotembelea Manyara au alipoteua makatibu tawala wapya imechangia kiasi gani kwenye uchumi, hatuna ripoti hizo kwa hiyo hatuwezi kuhukumu. Na hata atakapomaliza muda wake wa urais, ikatokea kuwa uchumi umepanda au umeshuka kuliko wakati alipoingia, bila tathmini huru hatutaweza kusema ni kipi hasa kilicholeta athari hiyo. Kwa hiyo kwa sasa tumwache rais afanye kazi yake, inapobidi tupige kelele pale anapokwenda kinyume na taratibu, sheria, kanuni na katiba ya nchi.

Nisamehe, mkuu! si kwamba nataka ku-have the last word lakini naomba tu ni-rest my case kwa hili. Unasema kuwa hizi safari za muungwana ni moja ya majukumu yake kikazi, sawa kabisa. na kwamba pia hakuna gauge ya kupima umuhimu baina ya majukumu haya ya raisi, pia sawa kabisa. LAKINI, tunapomchagua raisi, pamoja na meengi atakayotuahidi kama yeye binafsi na pia kwa kutumia sera za chama chake, tunategemea pia awe na UPEO na UTASHI binafsi wa mambo unaoweza kumfanya aamue kuwa miezi hii miwili nimesafiri sana nje ya nchi kwa hiyo hii miezi miwili nitashughulikia mambo ya hapa nyumbani na zile safari za kwenda A na B nitamtuma Waziri Mkuu wangu aniwakilishe. Hii inahitaji common Sense tu.

Ben Mkapa na Alli Hassani Mwinyi pia walipata kuwa maraisi wetu. Yapo mengi tunayowakumbuka nayo. Mabaya kwa mazuri. Lakini hakuna mahali tunapowakumbuka kwa kuwa walisafiri mara nyingi nje ya nchi. Je hawa hawakuwa na majukumu yaliyowataka wasafiri nje ya nchi? Si inawezekana kuwa kuna baadhi ya safari waliamua tu kuacha kwenda kwa sababu hawakuona kama kuna ulazima wa wao kufanya hivyo? Na pamoja na hayo si tunakubaliana kuwa Ben Mkapa angalau alikusanya Kodi kwa ufanisi mkubwa na kwa hakika hakuwa na haja ya kusafiri sana nje ili kumudu hili?
Mwisho, mbali ya upeo na utashi tunategemea pia raisi kuwa na jeuri fulani hivi kiasi cha kutia watu hamu ya kukuona. ukiwa rahisi wa kukubali kila mualiko unaopewa utajikuta kuna siku unaalikwa kusimamia ubatizo wa mjukuu wa Condoleeza Rice, kama mkuu wa nchi na sio kama mtu binafsi. I rest my case.
 
Back
Top Bottom