Rais Kikwete kupangua Baraza la Mawaziri

Rais Kikwete kupangua Baraza la Mawaziri

Sijui vyuo vya Tanzania lakini vyuo vya nje ukifanya rejea (reference) ya wikipendia utafeli hilo somo
Hatuko shuleni undosha akili ya kiuanafunzi. Yale ni maneno ya Ban Ki-moon juu ya uchapa kazi wa Asha Rose Migiro kwenye New York Times yana ukweli kuliko maneno ya majungu ya kutunga ya Subira Ramadhan kwenye blog ya bongo ya blog Vox media.
 
Wewe umpendaye utuambie fanikio moja to alilolifanyia UN. Ushahidi wa kushindwa kwake ni huu hapa:
Kwa vile wewe umejikita kwenye tabia yetu Watanzania ya copy & paste bila kujiuliza mlengo , maudhui na kusudio la hiyo habari na mleta habari katika media za mataifa ya magharibi basi na mimi naona niongee lugha unayoifahamu vizuri ya copy & paste.

Umeelewa nini kwenye hii sentesi ambayo nimeitoa kwenye bandiko lako,
understanding the politics at the world body and creating alliances

Hizo politics zinazosemwa za hapo ofisini (majungu) zina mahusiano gani na utendaji wa kazi za kila siku. Kwa hiyo kama hawezi kuyaelewa majungu ambayo ndiyo jadi kwenye hizo ofisi basi hata kazi nayo itakuwa imemshinda!.
 
Mkuu wangu hilo neno ukilisikiliza kwa undani utafahamu nini maana yake na nini kinatafutwa kupitia jinsia yake kama ilivyokuwa kwa Mama Spika wetu.

Nchi zetu bado ni Men's World bila kujalisha kama wanawake wana elimu na uwezo. Hata yeye anafahamu kabisa kuwa anaandaliwa kufika sehemu fulani kwa kutumia chapuo la jinsia yake pamoja na kwamba ana elimu na uwezo.

Huo ndiyo ukweli na Mama yetu ametoa shukrani kwa sababu hiyo!.

Kwahiyo hii ni shukrani ya 'ukike' mola aliyompa Asha-Rose hapa hakuna elimu wala taaluma.
Like Makinda like Asha-R.
Like Sam like Edo.
 
Ng'wamapalala, hii kauli (kama kweli imetolewa na Dr Migiro), inaleta ukakasi sana. Yaani kwa masomi kama huyu na kwa uwezo alionao bado anaamini kuwa amechaguliwa kwa sababu ya jinsia yake?

Hiyo ndio turufu yake anayotaka kuitumia kupata URAIS; anaamini kuwa kwa vile statistics zinaonesha kuwa wanawake ni zaidi ya nusu ya population ya nchi ,hivyo akiweza kupata kura zao anaweza kuufumania URAIS!!! Unfortunately, yeye kuwa pendekezo la Kikwete is a liability na vile vile historia is against wale wote wanaopigiwa debe na incumbent president!!!! I do not have to substatiate.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Waswahili wanasema ukiona mawingu yanatanda hiyo itakuwa ni dalili ya mvua.

Historia inatueleza kuwa unapoona Rais Kikwete anaanza kumpa Mtanzania mkao wa kula basi lazima kuna jambo anataka kumkabidhi kulifanya. Hata juzi juzi alifanya kwa Prof. Muhongo na matokeo yake tuliyaona.

Hatuna budi pia kusema inaelekea Dr. Migiro anataka kukabidhiwa jambo la kisiasa kulifanya baada ya kupelekwa bungeni. Hongera yake!.

Ninaamini Dr. Migiro ANA uwezo wa kuvaa viatu vya Uwaziri hasa katika eneo la utaalamu wake kielimu na uzoefu lakini pia ninaamini HANA uwezo wa kuvaa viatu vya Urais wa "Tanganyika" au Tanzania kulingana na changamoto zilizopo na zitakazokuwepo baada ya 2015 hasa ikichukuliwa kuwa Tanzania kwa sasa katika macho ya walafi wa malighafi duniani inashambuliwa katika motto wa 'scramble for Tanzania'.

Tanzania ya baada ya 2015 itahitaji Rais ambaye ni firm but fair. Rais ambaye anafahamu na pia anaguswa na umasikini wa Watanzania unaochagizwa na ruswa, ukabila na udini. Rais mwenye uwezo wa kupambana na hayo mambo makuu manne. Someone talks the talk and walks the walk.

Kwa mtazamo na fikra zangu, sioni kama Dr. Migiro ana huo uwezo na kama kweli CCM machinery wako kwenye mchakato wa kumsimamisha kugombea, basi watakuwa hawawatendea haki wanaCCM na Watanzania kwa ujumla hasa ikichukuliwa kuwa, kwa political climate iliyopo, mgombea wa CCM bado ana nafasi kubwa sana kushinda Uchaguzi Mkuu.

Lazima CCM watambue pia kuwa, kushindwa kukidhi haja na kuwaletea Watanzania mtu ambaye HANA uwezo kwa next General Election, basi wanaweza wakasema potelea mbali, mgombea wa CCM siyo baba wala mama yetu.

Lakini kaka umechambua vyema kabisa hii jambo..ila kinachofanyika na akina Nape ni kiini Macho tu. Mawaziri hawajashindwa kazi ila system nzima ya nchi ndiyo iliyoshindwa kutekeleza yote haya. Haikuwa na haja ya kuwaadhibu kwa kuwanyooshea vidole hawa mawaziri bali kurekebisha mfumo mzima kitu ambacho ni kigumu. CCM kuna vikao vya ndani kamati kuu ndio ingeweka mikakati ya jinsi ya kufanya kazi kuweza kukamilisha ILANI ya CHAMA na sio majungu. Kazi za CHADEMA, CUF, UDP, NCCR inafanywa na Sekreterieti ya CCM kwa nini. Vikao vya Chama ndio vingejadili haya na hawa (Mawaziri) wameyakuta sio waliyo yatengeneza. Wizara ni kitengo na sio MTU. Tunakazi sana kufikia malengo tusitafute kura kwa kujitekeny hadharani alafu tunajichekesha wenyewe.

Pathetic Party Secreteriate...
 
Mkuu Ng`wamapalala hivi Dr. Mgimwa ni Mbunge wa Kuchaguliwa au Kuteuliwa?:A S 39:
 
amfukuze kabisa membe maana kazi ya mambo ya nje mukulu anaipiga mwenyewe! Amebakiza nchi kidogo kumaliza dunia!
 
Kikwete anawatafutia watu ulaji tu,anaona si vibaya akiondoka madarakani awe amewaonjesha uwaziri,,,,ishu ya baraza la mawaziri kuwa mbulula ilishapigiwa sana kelele,,,akanyamaza kimyaaa,hivi ndani ya huu muda ataleta mabadiliko gani???halafu wadau ni muhim tukajua kuwa hizi wizara sometymz hazifanyi vizuri kwa sababu zinapewa pesa kidogo kwenye bajet zao,,,,hapa tusitegemee jipya kwa hawa mawaziri wapya,,,,viongoz wa nchi hii wanajua wafanyalo kwa maslah yao,tuendelee kufanya kaz kwa bidii tujiletee maendeleo,ila si kwa mawaziri
 
CCM inakufa ....mbona anawaondoa watu kwenye baraza la Mawaziri? ......

Mulugo inabidi wamuache naona ndani ya mda mfupi sana amejitahidi sana kuwabana walimu wenzake wanaochakachua mitihani kwa watoto.
 
Hizo politics zinazosemwa za hapo ofisini (majungu) zina mahusiano gani na utendaji wa kazi za kila siku. Kwa hiyo kama hawezi kuyaelewa majungu ambayo ndiyo jadi kwenye hizo ofisi basi hata kazi nayo itakuwa imemshinda!.

He copy nad paste ni dhambi kwani tuko kwenye mitihani hapa?

Labda nikuulize kwa nini alipigwa yeye majungu na sio bosi wake? understanding the politics at the world body and creating alliances sio UN peke yake hata wewe ukiajiriwa mahali hii ni principle ya muhimu sana. Huwezi kwenda kufanya kazi mahali kwa kuji isolate. Tatizo kubwa leteu Watanzania ni kubweteka na uteuzi na kuacha kuwajibika. Mtu akishapata cheo mwaka mzima anapokea hongera!

Na neno politics sio siasa unayoijuwa wewe!
 
Waswahili wanasema ukiona mawingu yanatanda hiyo itakuwa ni dalili ya mvua.

Historia inatueleza kuwa unapoona Rais Kikwete anaanza kumpa Mtanzania mkao wa kula basi lazima kuna jambo anataka kumkabidhi kulifanya. Hata juzi juzi alifanya kwa Prof. Muhongo na matokeo yake tuliyaona.

Hatuna budi pia kusema inaelekea Dr. Migiro anataka kukabidhiwa jambo la kisiasa kulifanya baada ya kupelekwa bungeni. Hongera yake!.

Ninaamini Dr. Migiro ANA uwezo wa kuvaa viatu vya Uwaziri hasa katika eneo la utaalamu wake kielimu na uzoefu lakini pia ninaamini HANA uwezo wa kuvaa viatu vya Urais wa "Tanganyika" au Tanzania kulingana na changamoto zilizopo na zitakazokuwepo baada ya 2015 hasa ikichukuliwa kuwa Tanzania kwa sasa katika macho ya walafi wa malighafi duniani inashambuliwa katika motto wa 'scramble for Tanzania'.

Tanzania ya baada ya 2015 itahitaji Rais ambaye ni firm but fair. Rais ambaye anafahamu na pia anaguswa na umasikini wa Watanzania unaochagizwa na ruswa, ukabila na udini. Rais mwenye uwezo wa kupambana na hayo mambo makuu manne. Someone talks the talk and walks the walk.

Kwa mtazamo na fikra zangu, sioni kama Dr. Migiro ana huo uwezo na kama kweli CCM machinery wako kwenye mchakato wa kumsimamisha kugombea, basi watakuwa hawawatendea haki wanaCCM na Watanzania kwa ujumla hasa ikichukuliwa kuwa, kwa political climate iliyopo, mgombea wa CCM bado ana nafasi kubwa sana kushinda Uchaguzi Mkuu.

Lazima CCM watambue pia kuwa, kushindwa kukidhi haja na kuwaletea Watanzania mtu ambaye HANA uwezo kwa next General Election, basi wanaweza wakasema potelea mbali, mgombea wa CCM siyo baba wala mama yetu.

Tumewachoka na liCCM lenu, hata mumpe uwaziri Barack Obama kwa mfumo wenu huu goigoi na uliokufa hakuna mtakachofanya. CCM haina mtu hata mmoja ambaye ni firm.
View attachment 124764
 
Asha Rose Migiro amechaguliwa ili kumdhibiti Tundu Lissu bungeni maana anamjua vilivyo kuwa ni kilaza darasani wakati anamfundisha UDSM.
 
Ni Bahati nasibu kila kukicha, bora siku zinaenda
 
Ni mchezo mbaya sana. Hivi wanaomtaka, wanamtaka kwa maslahi ya Taifa au ni kwa maslahi yao binafsi ama "makundi" yao? Au ni strategy tu ya kumkwepa na yule "jamaa" mwingine? Na kwa kuwa hili limeanza mapama hivi, kuna hatari kuwa sana kwa huyu mama....nina wasiwasi anaweza kuwa "eliminated" na hao mtandao wa huyu "jamaa".
Mimi naona wanamtaka huyu Mama kwa maslahi ya chama ambayo automatic yanagusa maslahi yao. Kwa maana nyingine, wanataka kupiga ndege wawili kwa jiwe moja bila kujua kuwa siasa za ndani ya CCM zinaweza zikashindwa kufurukuta kama vyama vya upinzani vikijipanga ipasavyo katika uchaguzi mkuu ujao.

Unafahamu Rais Kikwete ni mjanja sana katika kuzichanga karata za kisiasa.

Ninafikiri utakubaliana na mimi ukiangalia kuanzia njia iliyomuwezesha kuifikia Ikulu na pia alivyoweza kuzichanga karata kuhusu Spika kutokana na makundi kinzani ndani ya CCM yalivyokuwa yanataka kutoana macho na vile vile pia kwenye mgogoro wa UVCCM ambao aliupangua mpaka umemwezesha Nape kufika pale alipo.

Hata kwenye Mkutano Mkuu wa CCM ulioisha, aliweza pia kupangua hoja za wale mahasimu waliotaka kuziachanisha kofia za Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais ili waweze kumuweka mtu wao na kumtandika Rais Kikwete kisiasa.

Kwa sababu CCM ni chama dola, ndiyo maana hatuoni kama kuna mgogoro, lakini kiuharisia, CCM ina mgogoro mkubwa sana ambao utahitaji busara na hekima za hali ya juu ili kipite kwenye uchaguzi mkuu ujao salama.

Hekima ya wazee wa CCM inahitajika sana katika uteuzi wa wagombea Urais 2015.
 
Kila siri iko nje maana upinzani uko kila mahali na hapa watu wanaangalia ni nani atateuliwa ili naye anemeeke.
Siri sasa hakuna na kama hali ndo hii na kweli akafanya mabadiliko basi nchi iko uchi kwa mambo yake ya siri maana teuzi siku zote zinatakiwa kuwa siri na bila hivyo utakuwa ni usanii wa kiuongozi
 
duh chadema bwana hivi rais atabadilisha mawaziri mara ngapi ndani ya utawala wake??
 
Asha Migiro hata UN hawataki kumsikia ni mtu ambaye alikuwa mzigo kwa Umoja leo Tanzania mnampa uwaziri ? Haya wacha tuone sasa .Mimi nangojea Desemba 16 nione maajabu hayo .
 
Nasikia Lema atakuwa waziri wa maandamano na vurugu

Huko ni kumkosea heshima Mh. Rais, maana wizara zote zinaundwa naye na ndiye anayeteua mawaziri.

Kwa kauli yako una maana ameona umuhimu wa kuanziisha wizara hiyo na kwamba waziri atakayefaa ni Mh. Lema.

Hii ni dharau kwa Rais ambaye ndiye anayeunda baraza la mawaziri, na ndiyye mwenye uwezo wa kupunguza au kuongeza wizara kwa kadri anavyoona inafaa.

Pima kauli zako kabla ya ku-post, sijui kama natambua kuwa umadharirisha sana kiongozi wa nchi.

Kwa kauli yako una maanisha rais ata-establish wizara ya maandamano na vurugu.

Fedheha sana kwa kiongozi wangu wa nchi!
 
He copy nad paste ni dhambi kwani tuko kwenye mitihani hapa?

Labda nikuulize kwa nini alipigwa yeye majungu na sio bosi wake? understanding the politics at the world body and creating alliances sio UN peke yake hata wewe ukiajiriwa mahali hii ni principle ya muhimu sana. Huwezi kwenda kufanya kazi mahali kwa kuji isolate. Tatizo kubwa leteu Watanzania ni kubweteka na uteuzi na kuacha kuwajibika. Mtu akishapata cheo mwaka mzima anapokea hongera!

Na neno politics sio siasa unayoijuwa wewe!
Boss wake anachaguliwa na siyo ajabu pia katika UN kwa Katibu Mkuu kupigwa panga la kisiasa kutokana na majungu pamoja na kwamba utendaji wa kazi yake ni mzuri kwa ujumla.

Kwani hufahamu kuwa Boutros Boutros-Ghali alipigwa panga mwaka 1996 na USA kwenye uchaguzi wa pili na ukawa ndiyo mwisho wake wa kukikalia kiti cha Katibu Mkuu pamoja na kuwa nchi za Kiafrika na zingine zilikuwa zinapenda aendelee kitu kilichopelekea Kofi Annan kuchaguliwa.

Kufanya kazi kwenye ofisi za UN ni zaidi ya tujuavyo kwa nje. Hizo ndizo zinazoitwa politics at the world body.
 
Back
Top Bottom