Rais Kikwete kupangua Baraza la Mawaziri

Rais Kikwete kupangua Baraza la Mawaziri

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,507
IMEELEZWA kuwa Rais Jakaya Kikwete wakati wowote kuanzia Desemba 15, mwaka huu atafanya mabadiliko makubwa ya Baraza lake la Mawaziri. Hatua ya kwanza ya mabadiliko hayo imeanza kwa kumteua Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge wa Viti Maalumu na kwamba huo ni mkakati wa kumkabidhi mama huyo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi inayoshikiliwa na Dk. Shukuru Kawambwa.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, zimeeleza kuwa hatua hiyo ya rais imekuja kufuatia uwepo wa shinikizo la ndani na nje ya chama chake la kuwataka baadhi ya mawaziri wake kujiuzulu kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Imeelezwa kuwa Wizara ya Elimu inaonekana kusuasua na mtu pekee anayetajwa kuimudu wizara hiyo kwa sasa ni Dk. Migiro ambaye pia alishawahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Uteuzi wa ubunge wa Dk. Migiro ulitangazwa jana na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Florens Turuka ambaye alisema uteuzi huo umeanza jana.

Dk. Migiro ambaye pia anatajwa kuwa chaguo la kwanza la baadhi ya wakubwa wa CCM kwenye kinyang'anyiro cha urais kwenye uchaguzi ujao, amekuwa katika ziara za chama hicho zinazoendelea, jambo ambalo linatafsiriwa kuwa ni mikakati ya kumtambulisha mama huyo kwa wananchi.

Kabla ya kwenda UN, Dk. Migiro alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, nafasi aliyoonekana kuitumikia vema.

Aidha uteuzi wa Dk. Migiro umekuja katika kipindi ambacho joto la mabadiliko ya baraza la mawaziri likizidi kupamba moto, kutokana na udhaifu wa baadhi ya mawaziri kiutendaji.

Dk. Migiro ambaye amekuwa akitajwa kuwa mwanamke shupavu kiutendaji, wachambuzi wa masuala ya kisiasa na wasomi, wamekuwa wakimwona kama mtu anayefaa kuongoza wizara yoyote kwa maslahi ya taifa.

Akizungumzia uteuzi huo wa ubunge, Dk. Migiro alisema kuwa ameupokea kwa unyeyekevu na kwamba anamshukuru Rais Kikwete kwa kuonesha imani kubwa kwa wanawake na kwamba ataitumikia nafasi yake hiyo kwa weledi.

Baadhi ya mawaziri ambao wamekuwa wakipatiwa shinikizo la kujiuzulu ni pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Kawambwa na Naibu wake, Philip Mulugo, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Naibu wake, Adam Malima pamoja na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.

Kinana amekuwa akiwaandama mawaziri hao, huku akishinikiza kuwashughulikia ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho kwa kile alichodai wanakiangusha chama chao kwa kushindwa kutatua kero za wananchi ambao wanazidi kupoteza imani na CCM.

Kutokana na dhana hiyo, imeonekana wazi kumshtua Rais Kikwete katika kuonesha dalili za kufanya mabadiliko ya baraza hilo la mawaziri, ili kuweka sawa upepo wa kisiasa ndani ya chama chake.

Hali kama hiyo ilitokea pia Mei mwaka jana, ambapo Rais Kikwete aliwateua wabunge watatu wapya ambao ni James Mbatia, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Janeth Mbene.

Taarifa za uhakika zimebainisha kuwa mabadiliko ya mawaziri yatafanyika mara baada ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM kukutana mjini Dodoma wiki ijayo.

Kwa hisani ya Mtanzania.
 
Waswahili wanasema ukiona mawingu yanatanda hiyo itakuwa ni dalili ya mvua.

Historia inatueleza kuwa unapoona Rais Kikwete anaanza kumpa Mtanzania mkao wa kula basi lazima kuna jambo anataka kumkabidhi kulifanya. Hata juzi juzi alifanya kwa Prof. Muhongo na matokeo yake tuliyaona.

Hatuna budi pia kusema inaelekea Dr. Migiro anataka kukabidhiwa jambo la kisiasa kulifanya baada ya kupelekwa bungeni. Hongera yake!.

Ninaamini Dr. Migiro ANA uwezo wa kuvaa viatu vya Uwaziri hasa katika eneo la utaalamu wake kielimu na uzoefu lakini pia ninaamini HANA uwezo wa kuvaa viatu vya Urais wa "Tanganyika" au Tanzania kulingana na changamoto zilizopo na zitakazokuwepo baada ya 2015 hasa ikichukuliwa kuwa Tanzania kwa sasa katika macho ya walafi wa malighafi duniani inashambuliwa katika motto wa 'scramble for Tanzania'.

Tanzania ya baada ya 2015 itahitaji Rais ambaye ni firm but fair. Rais ambaye anafahamu na pia anaguswa na umasikini wa Watanzania unaochagizwa na ruswa, ukabila na udini. Rais mwenye uwezo wa kupambana na hayo mambo makuu manne. Someone talks the talk and walks the walk.

Kwa mtazamo na fikra zangu, sioni kama Dr. Migiro ana huo uwezo na kama kweli CCM machinery wako kwenye mchakato wa kumsimamisha kugombea, basi watakuwa hawawatendea haki wanaCCM na Watanzania kwa ujumla hasa ikichukuliwa kuwa, kwa political climate iliyopo, mgombea wa CCM bado ana nafasi kubwa sana kushinda Uchaguzi Mkuu.

Lazima CCM watambue pia kuwa, kushindwa kukidhi haja na kuwaletea Watanzania mtu ambaye HANA uwezo kwa next General Election, basi wanaweza wakasema potelea mbali, mgombea wa CCM siyo baba wala mama yetu.
 
CCM inakufa ....mbona anawaondoa watu kwenye baraza la Mawaziri? ......
 
Angalia pia miundombinu inarudisha nyuma uchumi, natoka kimara kwenda posta ktk jiji la Dar kwa masaa 3-4!. Do needful for Dar residence
 

Attachments

Hali ni mbaya sana apangue tu maana ukweli
huwezi kuulinganisha na uongo kamwe
Wananchi wamekosa matumaini pia inaonekana kama nchi ya wachache.


Viongozi hasa hao mawaziri viburi vimewajaa
sana km vile wanawatukia watu wasiowachagua
kwenye nafasi za Ubunge wao.
 
Huyu si alishindwa kule ambako kuna resources zooooote za dunia hii sasa huku tunakoaminishwa na chama cha kilaghai maccm kuwa tu masikini ataweza???!!! lakini kwa muda mfupi tutajua yu dhaifu kwa kiasi gani!
 
CCM inakufa ....mbona anawaondoa watu kwenye baraza la Mawaziri? ......
Huo ni mtazamo wako na inawezekana ikawa ni kweli.

Hata hivyo hufahamu kuwa katika nchi zilizoendelea Baraza la Mawaziri huwa linakuwa na muda fulani ambao Waziri Mkuu au Rais huwa analipangua ili kuongeza ufanisi na kuondokana na dhana ya kufanya kazi kwa mazoea inayosababishwa sana na kukaa kwenye position ya kiuongozi na kiutawala kwa muda mrefu.

Kwa nchi nyingi za Kiafrika na Tanzania ikiwemo, kuna baadhi ya mawaziri wanaweza kukaa katika nafasi moja kwa kipindi chote cha utawala wa Waziri Mkuu au Rais kama vile wanakuwa wamemilikishwa hiyo position.

Mabadiliko katika Baraza la Mawaziri siyo lazima iwe ni kwa sababu ya kushindwa majukumu bali vile vile huwa kwa sababu ya political tactical reason ili kuongeza ufanisi zaidi kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Ndiyo maana waliotuletea demokrasia wameweka kikomo kwenye kiti cha Rais ili kupisha mwingine bila kujalisha kama bado aliyepo anapendwa na kuchagulika tena.

REFRESHING, REFRESHING, REFRESHING.
 
.....anamshukuru Rais Kikwete kwa kuonesha imani kubwa kwa wanawake .......
Ng'wamapalala, hii kauli (kama kweli imetolewa na Dr Migiro), inaleta ukakasi sana. Yaani kwa masomi kama huyu na kwa uwezo alionao bado anaamini kuwa amechaguliwa kwa sababu ya jinsia yake?
 
Last edited by a moderator:
Huyu si alishindwa kule ambako kuna resources zooooote za dunia hii sasa huku tunakoaminishwa na chama cha kilaghai maccm kuwa tu masikini ataweza???!!! lakini kwa muda mfupi tutajua yu dhaifu kwa kiasi gani!
Kushindwa UN hakuna maana kuwa anaweza hata akashindwa katika nchi.

Kuna watu wanasahau jinsi kazi za UN zilivyo na majungu kutokana na matamanio ya nchi mbali mbali kuweka watu wake na wafanyakazi within UN office kuzitaka nafasi hizo. Kwa mtu ambaye hawezi kuzichanga karata za majungu katika hizo ofisi, kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kukwamishwa na kushindwa katika majukumu yake.

Kwa jinsi alivyo Dr. Migiro, siyo ajabu hilo lilichangia kwa kiasi kikubwa katika kuikosa nafasi yake.

By the way. Ni kweli Dr. Migiro alishindwa kazi au ndiyo yaleyale ya Watanzania na habari zao za vijiweni.
 
Ng'wamapalala, hii kauli (kama kweli imetolewa na Dr Migiro), inaleta ukakasi sana. Yaani kwa masomi kama huyu na kwa uwezo alionao bado anaamini kuwa amechaguliwa kwa sababu ya jinsia yake?
Mkuu wangu hilo neno ukilisikiliza kwa undani utafahamu nini maana yake na nini kinatafutwa kupitia jinsia yake kama ilivyokuwa kwa Mama Spika wetu.

Nchi zetu bado ni Men's World bila kujalisha kama wanawake wana elimu na uwezo. Hata yeye anafahamu kabisa kuwa anaandaliwa kufika sehemu fulani kwa kutumia chapuo la jinsia yake pamoja na kwamba ana elimu na uwezo.

Huo ndiyo ukweli na Mama yetu ametoa shukrani kwa sababu hiyo!.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kushindwa UN hakuna maana kuwa anaweza hata akashindwa katika nchi.

Kuna watu wanasahau jinsi kazi za UN zilivyo na majungu kutokana na matamanio ya nchi mbali mbali kuweka watu wake na wafanyakazi within UN office kuzitaka nafasi hizo. Kwa mtu ambaye hawezi kuzichanga karata za majungu katika hizo ofisi, kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kukwamishwa na kushindwa katika majukumu yake.

Kwa jinsi alivyo Dr. Migiro, siyo ajabu hilo lilichangia kwa kiasi kikubwa katika kuikosa nafasi yake.

By the way. Ni kweli Dr. Migiro alishindwa kazi au ndiyo yaleyale ya Watanzania na habari zao za vijiweni.

Ushindwe UN halafu hapa TAnzania ndo upaweze!! Huyu ni mzigo mwingine kwa Taifa hili linaloaminishwa kuwa masikini!! Hao ambao huwa wanachaguliwa toka mataifa mengine mbona wanaweza!
 
Nasikia Lema atakuwa waziri wa maandamano na vurugu
nasikia na wewe umo kwenye list ya uteuzi wa wabunge viti maalum, hongera. Sasa tunasubiri sijui watakupa Wizara ipi, ngoja tuvute subira.
 
Angalizo dogo kwenye hiyo taarifa ya mtanzania. Mheshimiwa Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa ni mbunge wa jimbo la Kalenga na siyo mteuliwa na Rais.
 
Mhe. Raisi amefanya mengi mazuri kwa manufaa ya Watanzania wote. Na inaonyesha wazi anaipenda sana Nchi yake. Ni mzalendo wa kweli. Mungu Ibariki Tanzania. Mabadiliko sio kuwa waliotolewa au kuachwa walitenda dhambi au hawafai, bali ni kutafuta maendeleo au mafanikio kupitia kwa wengine. Mbona hata wacheza mpira upokezana kuingia uwanjani?.
 
Back
Top Bottom