Rais Kikwete kuhutubia Ijumaa

Rais Kikwete kuhutubia Ijumaa

Mnao fuatilia hizi hutuba zake huwa anaruhusu maswali kutoka kwa watu huru?

Aanze tu kuruhusu, labda mkubali kumwandikia maswali miezi 6 kabla ili ampe werema amjibie kisha yachapwe yawekwe kwenye auto cue aisome mara 60 kisha akihutubia yawe kwenye ile karatasi anayoisoma wakati auto cue unaendelea kuscroll ili incase akiamua kwa aibu kuangalia mbele basi asipoteze point...hana analoweza kusema mwenyewe. Hata hotuba ya tezi tu kaandikiwa sembuse maswali ya papo kwa papo!!
 
afanye maamuzi ya majibu ya escrow na kutangaza mawaziri wapya,hivi haoni wahisani wanazidi kukata misaada mpaka waone amewafanyia nini hao watu wa escrow?pesa za kujenga kituo cha mabasi nazo wamesitisha kwanza inazidi kula kwa ccm na serikali iliyoko madarakani.jk amua kitu cha maana wananchi wanakussikiliza jk fanya maamuzi wananchi wanakusikiliza kuwasimamisha wakurugenzi sio ishu,ishu ni kuwapiga chini gasia na wale waliotajwa kwenye escrow wote na mahakamani wapelekwe
 
"Tumempoteza mwanasheria mahiri kwa sababu zisizo na msingi alikuwa hodari sana kajiuzulu mzee wa watu----------------"

Tulimpoteza pia LOWASSA kwa uongozi wa huyu huyu.

Sikutaka koment kwa thread hii, ila post yako imenigusa.
 
Ni bora ataarifiwe mapema kwamba Watanzania hatutapenda kusikia hadithi za tezi dume, tuliyoyasikia kuhusu tezi dume katika hotuba yake aliyoitoa JKN Airport yanatosha.


Kamanda umeona mbali na ndicho atakachokifanya.. wait n see
 
Kikwete hana mapya..kazi yake akihutubia ni vijembe na mipasho.huyu baba hatumtaki amalize muda wake aende zake


Tatizo hata haka kamuda alikobakisha naona kama nikarefu sana..
Kwa nini tu asituachie nchi yetu na aondoke zake sijawahi kuona rais sampuli hiii jamani..
 
Historia ya Jk sio nzuri anapochagua hadhara ya wazee
pengine tusubiri kuona anahutubia kuhusu nini maana mtoa mada hajasema hotuba italenga nini kama anataka kuongea mambo ya fainali za uzeeni utamkataza kuchagua hadhira hiyo. ila kama anataka kuongelea escrow kwa kweli itakuwa shidaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa tuwe na subira
 
Ni bora ataarifiwe mapema kwamba Watanzania hatutapenda kusikia hadithi za tezi dume, tuliyoyasikia kuhusu tezi dume katika hotuba yake aliyoitoa JKN Airport yanatosha.

!
!
haswaaa na aache mambo yake ya kingese ya kuchekacheka hovyo katika mambo yaliyo serious.
 
Atahutubia taifa kupitia wazee wa dar es salaam Ijumaa wiki hii alasiri.
chanzo: ikulu

akumbuke kwamba mbali na ukimya juu ya Esrow bado anadaiwa atoe tamko juu ya mahakama ya Kadhi kama itaruhusiwa kwenye Bunge la mwezi wa pili, waislamu bado wanatilia maanani yaliyosemwa na waziri wake mkuu Pinda
 
Nategemea ataaga rasmi zile safari zake za nje ya nchi kila wiki mbili badala ya hii ya mwisho ya upasuaji wa Tezi dume, mbele yake saivi ni kuzito sana kutokana na hivi vikwazo vya hawa watu weupe.

Atarudia tena kama alivosema kule china nanukuu "Naomba Mungu muda wangu wa kustaafu ufike ili nikachunge ngombe wangu huwa nawanea huruma sana wale wanaotaka urais"

Na sasa tumekua na vita baina yetu na mataifa mengine kutuingilia kwenye maamuzi na masuala mbalimbali ya ndani yanayotuhusu sisi kwa kweli wazee wangu tufike mahali shida zetu tuziweze, paa..paa.. Paa. Makofi kidogo.
 
Kubwa atakalozungumzia ni namna hali yake inavyoendelea baada ya kufanyiwa upasuaji wa 'tezi dume'
 
Lini ataongea Na wazee wa kilimanjaro.

Wazee wa kanda ya ziwa lini nao hasa mikoa ya shy,mwanza,mara na kagera.
Amezoea hao wazee wa dar kwsbb ni wazee wa YES,anawadanganya anavyotaka kwsbb akili yao muda huo inakuwa inawaza ubwabwa wa ikulu. Na wale huwa ni wazee wa ccm wa dar,utaona watakavyoibuka na mijinguo yao ya chama.
 
Tulimpoteza pia LOWASSA kwa uongozi wa huyu huyu.

Sikutaka koment kwa thread hii, ila post yako imenigusa.

Wangekuwa watu makini wasingeruhusu ama kushadidia uhujumu wa uchumi na maovu yaliyokuwa yakitendeka mbele ya pua zao!
 
Nashauri siku moja ahutubia vijana wa Dar es salaam, why kili mara wazee wa Dar es Salaam kwani vijana hawastahili kumisikiliza raisi wao mpendwa..
 
Back
Top Bottom