Rais Kikwete azuiliwa kuingia Denmark

Rais Kikwete azuiliwa kuingia Denmark

Rais Wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete amezuiliwa kuingia Denmark kutokana na vuguvugu la uchaguzi nchini humo baada ya kubainika kuwepo kwake kungempa nafasi zaidi ya kuonekana waziri mkuu Wa sasa kitendo kilichotafsirika Kama kumpigia kampeni.

RAIS Jakaya Kikwete ambaye amekuwa katika ziara za kuaga washirika wa mandeleo katika nchi za Scandinavia, amekataliwa kuingia Denmark kwa madai kuwa ziara yake itatumika kisiasa kumnufaisha Waziri Mkuu wa sasa wa Denmark.

Nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu wiki ijayo. Zuio hilo limekuja baada ya vyombo vya habari na vyama vya siasa kudai kuwa ziara hiyo ingetumika kumnufaisha Waziri Mkuu aliyepo kwa kumpa muda wa ziada mbele ya vyombo hivyo wakati huu wa kampeni.

Vyama vyote vya kisiasa vinapata muda sawa mbele ya vyombo vya habari na kwa hiyo uwepo wa Rais Kikwete nchini Denmark ungesababsha Waziri Mkuu aliyepo madarani kuonekana mara nyingi akimpokea mgeni wake.

Rais Kikwete hivi karibuni amefanya ziara katika nchi za Finland, Sweden, Uholanzi ikiwa ni sehemu ya kuaga kutokana na muda wake wa kuwa madarakani kufikia ukingoni.

MY TAKE:
Vyombo vya habari hapa kwetu vijifunze kutoka kwa Wenzetu viache ushabiki na viweke mizani sawa kwa wagombea na vyama vyote.....

Mkuu labda hiyo hisiwe Tanzania na li tbc lao.
 
Ushawishi kwenye lipi hasa? Mbona kashindwa kuwashawishi watoe trillion zao kusaidia bajeti ya 2014/2015 na 2015/2016!?

Jk anaushawishi mkubwa hata kwa wazungu
 
Mkuu Rais Wa nchi halazimiki kuwa na mwaliko pia ziara hii ni yeye ndo kajipeleka ati kuwaaga wahisani wetu....

So hakuitwa kaenda mwenyewe kwa mapenzi yake.....

Kwahiyo anatumia kodi zetu kwa kutembelea marafiki zake,tunawashukuru hao walio mpiga ban
 
Aisee nimevutiwa Sana na demokrasia za Wenzetu zilivyo na usawa....

ingekua hapa waziri mkuu au Rais aliyepo madarakani ambaye naye ni mgombea atafanya manyanga yote kwa kofia ya urais licha ya kwamba inampa favour kuliko wenzie....

Angalia TBC1 inavyotoa airtime kwa CCM kuliko vyama vingine ingawa inaendeshwa kwa kodi zetu sote....

Inasikitisha sana na hiyo uwe fundisho kwa serikali yetu iwache upendeleo
 
Huku watangaza nia wanaleta viongozi wa nchi jirani.

Si unakumbuka pia çcm waliwahi kumleta Mchina jukwaani

Duuu,sipati picha akirudi bongo hiyo aibu ataificha wapi!
 
Inasikitisha sana na hiyo uwe fundisho kwa serikali yetu iwache upendeleo

Hapa hawayawezi hayo... ni double standards kwakwenda mbele....

Kwenye ESCROW wengine wametoswa wengine wameachwa!!!

Kwenye kutia nia wengine wanapewa airtime wengine wananyimwa!!!

Double standards hizi zimetulemaza kiasi cha kudhani kote zipo matokeo yake ndo hayo....
 
Ifike mahali bunge lihoji matumizi mabaya ya IKULU na safari za mheshimiwa Rais, ni fedheha na aibu sana!!!!

Hiyo safari inaonekana alijiendea tu bila kupangwa Kama anaenda gulioni
 
Na hiyo gharama ndo hasara kwa taifa

Wakitoka huko hasira zao zote ni kulazimisha efd ili warudishe fedha walizotumia huko,hii nchi ni zaidi ya tuijuavyo.
 
Rais Wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete amezuiliwa kuingia Denmark kutokana na vuguvugu la uchaguzi nchini humo baada ya kubainika kuwepo kwake kungempa nafasi zaidi ya kuonekana waziri mkuu Wa sasa kitendo kilichotafsirika Kama kumpigia kampeni.

RAIS Jakaya Kikwete ambaye amekuwa katika ziara za kuaga washirika wa mandeleo katika nchi za Scandinavia, amekataliwa kuingia Denmark kwa madai kuwa ziara yake itatumika kisiasa kumnufaisha Waziri Mkuu wa sasa wa Denmark.

Nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu wiki ijayo. Zuio hilo limekuja baada ya vyombo vya habari na vyama vya siasa kudai kuwa ziara hiyo ingetumika kumnufaisha Waziri Mkuu aliyepo kwa kumpa muda wa ziada mbele ya vyombo hivyo wakati huu wa kampeni.

Vyama vyote vya kisiasa vinapata muda sawa mbele ya vyombo vya habari na kwa hiyo uwepo wa Rais Kikwete nchini Denmark ungesababsha Waziri Mkuu aliyepo madarani kuonekana mara nyingi akimpokea mgeni wake.

Rais Kikwete hivi karibuni amefanya ziara katika nchi za Finland, Sweden, Uholanzi ikiwa ni sehemu ya kuaga kutokana na muda wake wa kuwa madarakani kufikia ukingoni.

MY TAKE:
Vyombo vya habari hapa kwetu vijifunze kutoka kwa Wenzetu viache ushabiki na viweke mizani sawa kwa wagombea na vyama vyote.....

Ili Jakaya Kikwete azunguke dunia nzima kuaga kwamba anamaliza muda wake pesa za safari hizo zinatoka katika fungu gani??
 
Ili Jakaya Kikwete azunguke dunia nzima kuaga kwamba anamaliza muda wake pesa za safari hizo zinatoka katika fungu gani??

Mwaka jana nilisikia mabilioni yakitengwa bungeni kwaajili ya ishu hii japo wabunge walilalamika Sana!!!
 
wameshamchoka tayari hivi bado yupo nje au amesharudi nchini .
 
wewe kikongwe Mkwere kaisha timuliwa uko.Mkwere akui yeye anaona sifa kufuja kodi zetu.Hakika watu wa pwani ustaarabu sifuri

Huyo ajuza hakuelewi kitu hapo...
 
Back
Top Bottom