Rais Kikwete ateua wakuu wapya wa mikoa

Nikupunguza nguvu ya Bunge kama wabunge zaidi ya 50 nis ehemu ya serikali (Mawaziri na naibu wao) sasa ukiongeza na wabunge wa kuteuliwa (10) na hao wanaoteuliwa kuwa RCs and DCs (5) ndani ya bunge rais anakuwa na wateule wake 65 katiya wabunge wote 360 hii ni sawa 19% kwa hiyo anahitaji 15% tu kuzuia 2/3 ya bunge lote
 
Wapi Papaa Lawrence Masha?
Wapi mamaa Dr. Batilda Buriani?

Na Dr Deodolus Kamala je????

May be wanasubiri mikoa mpya....Ameanza na wachache ili kuepuka kasheshe kama ile ya Jairo....Anakwenda mwendo wa kutoa single na kusikilizia kama itapewa air time ya kutosha!!
 
Du tunashukuru sana Invisible kwa taarifa za uhakika, I do appreciate, keep it up.
 
Lol..Kuna hiyo mipya bado..labda mheshimiwa atanikumbuka

Mahiza, Bendera na Mwananzila tayari wameula

mikoa mipya ya bishoo Masha, Batilda na UVCCM wasio kambi ya Lowasa

yoyote aliyeko kwenye kundi la awaniaye 2015 imekula kwake
 
Hiv ktk nchi hii kwel wamekosekana watu wengine na wenye sifa mpaka rais aamue kuwavisha baadh ya watu kofia mbil! Huu ni udhalilishaj kwa watanzania,haiwezekan hata siku moja watu wapeane vyeo tu kwa kuwa wanajuana,hii nchi itakuwa ya ukoo flan bas,just wait,tutaheshimiana 2015 tu.
 
Nikupunguza nguvu ya Bunge kama wabunge zaidi ya 50 nis ehemu ya serikali (Mawaziri na naibu wao) sasa ukiongeza na wabunge wa kuteuliwa (10) na hao wanaoteuliwa kuwa RCs and DCs (5) ndani ya bunge rais anakuwa na wateule wake 65 katiya wabunge wote 360 hii ni sawa 19% kwa hiyo anahitaji 15% tu kuzuia 2/3 ya bunge lote
Mkuu tafsiri yake kubwa ni kwamba Wabunge wengine wote waliobakia 295 wanategemea maendeleo ya sehemu zao kutoka kwa hawa wateule wa rais 65. Hivyo Bunge haliwezi kusimamisha muswada wa kutokuwa na imani na rais ikiwa asilimia kubwa ya wabunge wenyewe ni tegemezi.
 
Mbona ni wale wale tu..?, waliokosa ubunge n.k.,hivi kweli hakuna watu wengine wanaoweza kufanya hizo kazi?.,kama kila nafasi ili upewe ni lazima uwe mwanachama wa CCM na swahiba wa Kikwete hii nchi inapelekwa wapi?
 
Tatizo lenu bwana mnakomalia ishu hata hazina msingi wowowte sasa kuna ubaya gani mbunge kuwa mkuu wa mkoaacheni wivu wa kike au kwakuwa ni mwanamke mwenzenu kapewa shavu!!!
Mkuu wa mkoa/wilaya hawa si viongozi wa serikali?atatofautisha vp utendaji wake na siasa?kuwa mbunge ni mwanasiasa moja kwa moja, haya mambo ndiyo yanaturudisha nyuma na sio wivu. Atatumikia wapiga kura wake saa ngapi na mkoa wakati gani? Je demokrasia itafanya kazi ipasavyo?
 
iringa mbona wanapeleka wanawake mara nyingi? Kuna wilaya mkuu wa wilaya,mkurugenzi, na sasa mkuu wa mkoa wanawake! Yani ukifika mambo wanayoyafanya ni vituko tupu!
 
Ama kweli ukijifanya kuifagilia ccm hata kama inafanya pumba basi wewe utapendwa tu na mkuu mfano huyu mama Eng Manyanya anashobo na serikali hii mpaka basi
 
Heko watanzania nakupenda saana kueshimika kwa kuwa na kofia mbili au tatu.Hivi kweli mtu amestaafu kutoka JWTZ au Polisi alafu anapewa nafasi ya RC au DC,kweli huyu mtu anafikila za mageuzi au utendaji mwingine kuliko aliyo uzoea?Ebu tusubiri TANGANYIKA YETU 2015 na siyo hii Tanzania yenu.
 
Wakati wa Nyerere alikuwa anateua pia Wakuu Wa Mikoa Zanzibar; Nakumbuka Wazanzibari wengi tu walikuwa Wakuu Wa Mikoa Bara
 
Dr Slaa amewahribu sana!<br />
kila kitu mnaona ni ufisadi.<br />
Jamani tubadilike
<br />
<br />
kwani cc hatuoni vtu wanavyofanya? Ulipata birth asphyxia enzi hizo nn? We mtu anapata mishahara miwili unataka tukae kimya? Kuna wengine walivurunda awamu iliyopita wananchi wakawakataa,unadhani watafanya lolote kwenye hiyo mikoa? Waliostaafu wanaambiwa watapewa kazi nyingine, hakuna watu wengine?
 
Back
Top Bottom