Rais Kikwete ateua wakuu wapya wa mikoa

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,076
7,786
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA MIKOA WAPYARAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa nchini.

Katika mabadiliko hayo, amewateua Wakuu wa Mikoa wapya 15, kuwabadilisha vituo vya kazi Wakuu wa Mikoa watano na wengine saba wamestaafu kwa mujibu wa taratibu. Mkuu wa Mkoa wa Singida amebaki kwenye kituo chake cha kazi wakati Wakuu wa Mikoa wengine wanne watapangiwa kazi nyingine.

Aidha, Wakuu wa Mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika watatangazwa baadaye.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Wakuu wa Wilaya 11 wamepandishwa Vyeo na kuwa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo: Bw. John Gabriel Tupa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara; Bw. Saidi Thabit Mwambungu (Ruvuma); Bi. Chiku S. Gallawa (Tanga); Bw. Leonidas T. Gama (Kilimanjaro); Dk. Rehema Nchimbi (Dodoma); Bw. Elaston Mbwillo (Manyara); Kanali Fabian Massawe (Kagera); na Bibi. Fatma Abubakar Mwassa (Tabora). Wakuu wa Wilaya wengine walioteuliwa ni Bw. Ali Nassoro Rufunga, (Lindi); Eng. Ernest Welle Ndikillo, (Mwanza); na Bw. Magesa Stanslaus Mulongo Mkuu wa Mkoa (Arusha).

Walioteuliwa nje ya nafasi hizo ni Eng. Stella Manyanya (Rukwa); Bibi Mwantumu Mahiza, (Pwani); Bw. Joel Nkaya Bendera (Morogoro) na Bw. Ludovick Mwananzila (Shinyanga).

Waliobadilishwa vituo vya kazi ni Bw. Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza; Bw. Said Mecki Sadiki anayekwenda Dar es Salaam akitokea Lindi; Bibi Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma; Lt. Kanali Issa Machibya anayekwenda Kigoma akitokea Morogoro; na Kanali Joseph Simbakalia anayekwenda Mtwara akitokea Kigoma. Dk. Parseko Ole Kone ataendelea kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Waliostaafu ni Bw. Mohammed Babu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera; Bw. Isidore Shirima aliyekuwa Arusha; Kanali (mst.) Anatory Tarimo aliyekuwa Mtwara; Bw. John Mwakipesile, aliyekuwa Mbeya. Wengine ni Kanali Enos Mfuru aliyekuwa Mara; Brig. Jen. Dk. Johanes Balele aliyekuwa Shinyanga; na Meja Jen. Mst. Said S. Kalembo aliyekuwa Tanga.

Wakuu wa Mikoa wanne waliostaafu ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi ni Bibi Amina Mrisho aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani; Dk. James Msekela aliyekuwa Dodoma; Bw. Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Bw. Daniel Ole Njoolay aliyekuwa Rukwa.

Wakuu wote wa Mikoa waliopo sasa wameagizwa kuandaa Hati za Makabidhiano (Handing Over Notes) katika muda wa siku 14 kuanzia siku ya kuapishwa kwa Wakuu wapya wa Mikoa. Aidha Wakuu wa Wilaya ambao wamepandishwa vyeo kuwa Wakuu wa Mikoa nao wanapaswa kufanya hivyo hivyo kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya watakaopangiwa vituo vitakavyokuwa vimeachwa wazi kutokana na uteuzi wao.

Wakuu wa Mikoa ile minne mipya na Wakuu wa Wilaya watakaoteuliwa hapo baadaye nao watatakiwa kuandaa Hati za Makabidhiano ndani ya siku 14 tangu kuapishwa.

Makabidhiano hayo lazima yahusishe pia kutembelea kwa pamoja baadhi ya maeneo na miradi ambayo ni muhimu kama sehemu ya makabidhiano yao.

Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa na Wakuu wa Mikoa minne mipya wakaoteuliwa pamoja na Wakuu wote wa Wilaya watakaoteuliwa baada ya zoezi kukamilika watatakiwa kuhudhuria mafunzo ya wiki tatu kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kiuongozi na kiutendaji.

Wakuu hao wapya wa mikoa wataapishwa siku ya Ijumaa, Septemba 16, 2011 saa 4.00 asubuhi kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wakuu hao wapya wa mikoa; vituo wanavyokwenda na vituo walivyotoka ni kama ifuatavyo:

Na.
JINA LA MKUU WA MKOA
KITUO AENDAKO
KITUO ATOKAKO
1.Bw. Saidi Mecki SadikiDAR ES SALAAMRC - Lindi
2.Bw. John Gabriel TupaMARADC - Dodoma
3.Bw. Saidi Thabit MwambunguRUVUMADC - Morogoro
4.Kanali Joseph SimbakaliaMTWARARC Kigoma
5.Bi. Chiku S. GallawaTANGADC - Temeke
6.Bw. Abbas KandoroMBEYARC Mwanza
7.Bw. Leonidas T. GamaKILIMANJARODC – Ilala
8.Dkt. Parseko Ole KoneSINGIDARC Singida
9.Eng. Stella ManyanyaRUKWAMbunge V/Maalum
10.Bibi Christine IshengomaIRINGARC Ruvuma
11.Dk. Rehema NchimbiDODOMADC - Newala
12.Bw. Elaston John MbwilloMANYARADC – Mtwara
13.Col. Fabian I. MassaweKAGERADC - Karagwe
14.Bibi. Mwantumu MahizaPWANIMbunge/NW Mstaafu
15.Bibi. Fatma A. MwassaTABORADC - Mvomero
16.Bw. Ali Nassoro RufungaLINDIDC - Manyoni
17.Eng. Ernest Welle NdikilloMWANZADC - Kilombero
18.Lt. Col. Issa MachibyaKIGOMARC Morogoro
19.Bw. Magesa S. MulongoARUSHADC - Bagamoyo
20.Bw. Joel Nkaya BenderaMOROGOROMbunge/NW Mstaafu
21.Bw. Ludovick MwananzilaSHINYANGAMbunge/NW MstaafuIMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM
JUMATANO, SEPTEMBA 14, 2011.

 

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,602
788
Atakuwa kafanya jambo jema kama atafanya uteuzi wa kuzingatia vigezo na uwezo wa kila mmoja. Kingine itapendeza endapo huo uteuzi utakuwa umezingatia uelewa wao ktk maeneo waendayo kufanya kazi. Wakuu wa Mikoa makada wa chama ni matatizo!
 

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
868
219
Atakuwa kafanya jambo jema kama atafanya uteuzi wa kuzingatia vigezo na uwezo wa kila mmoja. Kingine itapendeza endapo huo uteuzi utakuwa umezingatia uelewa wao ktk maeneo waendayo kufanya kazi. Wakuu wa Mikoa makada wa chama ni matatizo!
Kaisha teuwa mkuu mambo ya vigezo too late wengi watakuwa wanawake na maswahiba waliokosa seats sehemu mbalimbali kikwete hana ubavu kuteuwa mtu mwadilifu itakula kwake
 

mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
554
Nilianza kuamini kaamua kuachana na post hizo za zenye mwelekeo wa kichama kuliko utendaji, kumbe alikuwa katulia tu. au alikuwa anachuja wanaohitaji "asante"/maswahiba awape na kutangaza?
 

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
939
57
Hapa ni kazi kweli, Mbona wanajeshi ni wengi ukuu wa mkoa? Je mtandao wa mpinzani wake umevunjika? Mbona singida hakuna mabadiliko au ndiye aliyeng'ara kiutendaji?
 

Sizinga

JF-Expert Member
Oct 30, 2007
8,825
5,291
Sidhani kama masharti na vigezo vimezingatiwa hapa sanasana ni kulipana fadhila kwa hawa wakulu wetu, haina haja ya kuanzisha mawilaya mingi kiasi hiki ilhali wilaya zilizopo hazijaboreshwa..miundo mbinu, maji, barabara, elimu nk.

Tumekaa muda mrefu bila wakuu wa mikoa wala wilaya, hata waliokaimu wameifanyia nini Tanzania??zaidi ya kula miposho na mamishahara na marupurupu na makandoro(maGX)...huyu ni ufisadi sana eeh tanzania yangu.
 

Entrepreneur

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
1,087
612
Hv hili suala la kofia mbili ni mpaka lini! Kuna haja gani kuteuwa mtu kuwa mkuu wa mkoa au wilaya wakati tayari ni mbunge?

Sasa hapo bunge litasimamia vipi utendaji wa serikali? Hata hivyo nchi hii ina watanzania zaidi ya milioni 40 na wengi hawana kazi halafu bado tunawaongezea wengine majukumu.

Nakumbuka PM aliwah kuulizwa na mtoto wa darasa la saba, kuhusu hizi kofia mbili, akashindwa kutoa jibu. Mpaka leo swali lile halijajibiwa
 

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,189
Kwa hiyo Stella Manyanya aliamua kukabidhi akili zake in exchange na ukuu wa Mkoa? Na je anakuwa mkuu wa mkoa maalum kusimamia uwekezeji wa Agrasal nyumbani kwa mtoto wa mkulima? Hata hivyo nikutakie kila heri, ika swali moja dogo la nyongeza. Hivi kati ya watanzani milioni 40 na ushee hakuna mtu anaweza kuwa mkuu wa mkoa badala ya kulimbikiziana vyeo? Stella Manyanya ni mbunge. sasa anakuwa mkuu wa mkoa! Ni lini tutaachana na hii kasumba mbaya?
 

Mfwatiliaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
1,325
64
ooh..sijui alikuwa rc mstaafu cum rc; sijui dc; sijui mbunge..bongo bana!! just recycling and recycling!! am out..always hakuna jipya, and this country will never change--unless magambas are out
 

Mwita Matteo

JF-Expert Member
May 16, 2010
216
55
Leo Mh. Raisi wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ameteua waku wa mikoa na kuwapandisha hadhi baadhi ya wakuu wa wilaya kuwa wakuu wa Mikoa. Mmoja wa wateule hao ni Mh. Eng. Stela Manyanya (MB). Mimi hapa ndipo ninapo hitaji ufafanuzi, hivi ni kwa nini Mbunge ateuliwe tena kuwa Mkuu wa Mkoa?? Najua huyu si wa kwanza kuna wengi walisha wahi kuwa wabunge na wakuu wa mikoa. Hapa tatizo ni nini? Je hatuna watendaji wakutosha serikalini au popote pale wasio kuwa wabunge au tatizo ni nini?? Tafadhali naomba kusaidiwa.

Nawasilisha,
 

Limbani

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
1,439
440
Mbona mikoa ya Tanzania Visiwani hawakuchaguliwa? au kule wanateuliwa na Rais wa SMZ!?
 

Biohazard

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
2,186
1,403
Duuu... sio mchezo naona magenerali,mabrigedia,mameja,makanali wanazidi kupungua. Basi sawa..!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

9 Reactions
Reply
Top Bottom