Rais Kikwete ateua wabunge wapya wawili

Rais Kikwete ateua wabunge wapya wawili

Rais Kikwete amemteua Dr Grace Pujah na Bw Innocent Seba kuwa wabunge wapya katika bunge la Muungano kuanzia tar 20 Machi.

Kufuatia uteuzi huo, sasa JK amemaliza orodha wa wabunge wote kumi wa kuteuliwa kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Katiba.

===========

Labda Watanzania sasa mtaamuka katoka kwenye usingizi wa PONO na kutambua kwamba hii katiba ya 1977, tuliyonayo ni MAJANGA MAKUBWA!

Nyerere Mwenyewe aliwahi kukiri kwamba hiyo Katiba inampa madaraka makubwa kiasi kwamba inaweza kumfanya awe DIKITETA.

Ninaomba Kikwete kabla ya kumaliza muhula wake aunde WIZARA ya kushughulikia kero za Wakwere na amteue Ridhwani Kikwete (MB) kuwa waziri wake, labda ndio Watanzania mtaamuka kutoka kwenye huo usingizi wa PONO. MAJINGA ndiyo yaliwayo!
 
Nadhani kuna sababu maalum kwa sababu watafanya nini wakati watahudhuria mkutano mmoja tu na bunge linavunjwa. ama sivo kama ni kutekeleza masharti ya sheria tu basi ni ajabu
 
Bado miezi miwili wabunge wapya wanateuliwa. Wana haki zifuatazo kama sikosei:
1. Mkopo wa gari (kiasi sawa na walichopewa wenzao mwaka 2010?)
2. Kiinua mgongo (sawa na wabunge waliotumikia miaka 4 na miezi 8?)
 
mwezi June bunge linavunjwa! Kateua marafiki KULA PESA TU
 
Haa haa tungekuwa na bunge makini ilipaswa kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais" huu ni ufujaji wa pesa za umma.
 
Hakika leo ndo nathibitisha kwamba huyu jamaa ni Dhaifu kupita maelezo...!!!! Khaaaaaaaa

Sasa hiyo miezi mitano iliyosalia (Kikao kimoja cha Bunge) Watafanya kazi gani hawa wabunge? Yaani watu wafanye kazi miezi mitano tu then wapewe masurufu juu....!!!

Huwa nawashangaa sana wanaodai ati hii nchi ni masikini haina hele...!!!! Haina hela????


Real kabisa mtu unasimama mbele ya kadamnasi na kudai Tanzania ni nchi masikini tena ati hujui kwamba umasikini wa nchi hii hujui unatokana na nini?? We utakuwa mgonjwa kuliko misukule yote ya Lumumba hadi laki si pesa.!!

Goooooooosssshhhhhhh!!!!

BACK TANGANYIKA

Nchi ina umaskini wa viongozi
 
Last edited by a moderator:
ubunge wa nini sasa wakati muda umeisha wa bunge la taifa.Mamlaka ya Rais wetu ni makubwa mno nayatumika kwa maslahi yake binafsi kuliko kuyatumia kwa maslahi mapana ya Taifa.Wabunge wateule wenye tija katika umri wa bunge hili ni Prof Mbawala na James Mbatia wengine labda maswala binafsi.
 
wa Miavuli', kawagawieni kila mkoa 1bn (bila shaka vijana mlizipata), na maamuzi mengine meeengi ya ajabu ajabu! Leo mnashangaa na kulalamika wkt mnajua hajawahi kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha ubongo? Kila mchuma janga hula na nduguze vijana wa Tz.
 
Back
Top Bottom