Rais Kikwete ateua wabunge wapya wawili

Rais Kikwete ateua wabunge wapya wawili

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,506
Rais Kikwete amemteua Dr Grace Pujah na Bw Innocent Seba kuwa wabunge wapya katika bunge la Muungano kuanzia tar 20 Machi.

Kufuatia uteuzi huo, sasa JK amemaliza orodha wa wabunge wote kumi wa kuteuliwa kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Katiba.

===========

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.

Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.

Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.

Wabunge ambao wameshateuliwa ni:


  • Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
  • Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
  • Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
  • Mhe. Janet Zebedayo Mbene
  • Mhe. Saada Salum Mkuya
  • Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
  • Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
  • Mhe. James Fransis Mbatia

Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi

Ikulu-Dar-Es-Salaam
 
Hakika leo ndo nathibitisha kwamba huyu jamaa ni Dhaifu kupita maelezo...!!!! Khaaaaaaaa

Sasa hiyo miezi mitano iliyosalia (Kikao kimoja cha Bunge) Watafanya kazi gani hawa wabunge? Yaani watu wafanye kazi miezi mitano tu then wapewe masurufu juu....!!!

Huwa nawashangaa sana wanaodai ati hii nchi ni masikini haina hele...!!!! Haina hela????


Real kabisa mtu unasimama mbele ya kadamnasi na kudai Tanzania ni nchi masikini tena ati hujui kwamba umasikini wa nchi hii hujui unatokana na nini?? We utakuwa mgonjwa kuliko misukule yote ya Lumumba hadi laki si pesa.!!

Goooooooosssshhhhhhh!!!!

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Angemchagua zito ktk kiti kimoja ili aapishwe mara mbili na achukue kiinua mgongo mara mbil na apate pesa za kuichangia act ili waciwe omba omba kama this time. Hahaaa mkuluuu haach viporo! Vijaze baba liziiii huu uuu uu hahaaaaa a
 
Bunge linakwisha wanateuliwa ili wapate kinua mgongo

If this is true, then wacha watu waibe tu serikalini. If the president can do such a thing ili watu wapate kiinua mgongo, then wacha walio na nafasi ya kuiba waibe. Huu pia ni wizi kwa style yake kumteua mtu wakati bunge linaisha apate kiinua mgongo
 
Back
Top Bottom