Rais Kikwete ateua wabunge wapya wawili

Rais Kikwete ateua wabunge wapya wawili

Ili nalo neno,ina maana wakimaliza hiyo miezi 5 watalipwa kiinua mgongo sawa na wenzao wenye miaka 5 ? au kuna formula itatumika? Kuna vikao vingapi vimebaki kabla ya Bunge kuvunjwa? Ni kwanini hakupewa Mpanju ambaye yaonekana ana strugle sana kupata nafasi hiyo?
 
Bunge linavunjwa mwishoni mwa mwezi June na hili linaleta maswali zaidi. Wawili hao watahudhuria sana sana kikao kuanzia cha 9 cha mkutano wa 19 na vikao vyote vya mkutano wa 20, basi baada ya hapo wanapewa kiinua mgongo!!!! Jamani wanaojua zaidi hili somo watujuze!!!

Kweli, "wonders shall never end".

''Kweli, JK "wonders does not have an end"


Haya ndiyo aliyoyaona Mwalimu JKambarage! Lakini haikutosha Kijana anayejitambua aliliona pia.

Narudia Mnyika historia itakukumbuka kwa kutokuwa mnafiki na maneno yako!
Maana wangukuwa hawa wasomi na Wabunge wengine uchwara angefuta maneno aliyoyasema Bungeni-huu ndio uwakilishi wa Watu.
 
Tusiingilie katiba...Rais ana mamlaka.
Hajavunja katiba.
Je angeteua wote kumi toka siku ya kwanza ya bunge ingekuwa vipi. Ameokoa ngapi kwa mnaojua mahesabu.
Tutii mamlaka iliyopo..
Tumejaa unafiki sana.
Wengine mnadai picha yake,ili iweje? Huu ni ubaguzi.
Angekuwa ana ubin wa mtoto wa kiongozi, ungesikia wanabebana!
Wengine mkisoma majina, mnakimbilia udini na kuyafananisha!
Tukubali sote tunaangamiza taifa kwa upumbavu wetu. Tuache ushabiki na porojo zisizo na mpango.
 
Tusiingilie katiba...Rais ana mamlaka.
Hajavunja katiba.
Je angeteua wote kumi toka siku ya kwanza ya bunge ingekuwa vipi. Ameokoa ngapi kwa mnaojua mahesabu.
Tutii mamlaka iliyopo..
Tumejaa unafiki sana.
Wengine mnadai picha yake,ili iweje? Huu ni ubaguzi.
Angekuwa ana ubin wa mtoto wa kiongozi, ungesikia wanabebana!
Wengine mkisoma majina, mnakimbilia udini na kuyafananisha!
Tukubali sote tunaangamiza taifa kwa upumbavu wetu. Tuache ushabiki na porojo zisizo na mpango.
Katiba inamruhusu, sawa. Busara je?
 
Kweli.....hayo ni matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za nchi....hivi huyu jamaa hana washauri???....TUNAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA YA KATIBA kupunguza madaraka kwa viongozi ambao hawajitambui......hata driver barabarani angekuwa anamgongo kila mpita njia kisa yuko sahihi kulingana na sheria za barabarani basi karibu watanzania wote tungekuwa vilema kama sio vifo vingi......Huyu jamaa ana waharibia wenzake kisa amemaliza muda wake
 
Hivi siyo kazi ya mpare kweli?? Na hivi ndo katiba mpya hairuhusu watu kushitakiwa wakimaliza madaraka yao, TUTAMKUMBUKA MZEE WARIOBA
 
ukistaajabu ya ngedere utaona ya fisi!!!
nani awahurumie waTZ maskini nani..
Tuache kujitoa kwenye ukweli ama tuendelee!!!
 
Leo mapema asubuhi mjini dodoma,bungeni wameapishwa wabunge wawili wa kuteuliwa na rais.its ok.

Swali langu ni je,katiba ya Tz inasema kama jimbo la uchaguzi litakuwa wazi miezi minane hakuna uchaguzi utakaofanyika,katika jimbo la mafinga magharibi (NYASA) kwa marehemu Capt.Komba.

Swali:je jk yuko sahihi kuteua miezi miezi saba kabla ya Uchaguzi mkuu?

Swali; Au ni technical appointmnt mahususi kwa ajili ya uchaguzi?


Only in Tanzania...
 
.....................................................
One of the cardinal principles of Economics is Opportunity Cost. Do the fast thing first, and those which can wait let them wait.....

Hebu tujaribu kufanya hesabu ndogo za kugawanya na kuzidisha za darasa la tano. Ni hivi, wabunge wawili walioteuliwa watalipwa mishahara ya miezi mitano bure maana hatutegemei jipya watakalolifanya huko bungeni. Mshahara kwa mbunge mmoja ni Mil.11 mara miezi mitano watakayofanya kazi ni jumla ya Sh.Mil 55 kwa kila mmoja. Kwa wote wawili ni Mil.110.

Wabunge hawa walioteuliwa leo watalipwa kiinua mgongo kwa viwango vya wabunge wa kawaida Sh.Mil.90 kila mmoja ifikapo tar.31 mwezi July mwaka huu. Kwa wote wawili ni Mil.180.

Taarifa ya Ikulu inasema uteuzi wao unaanza tarehe 20, hivyo basi kuanzia tar.21 wataanza kulipwa posho za vikao vya bunge kwa siku 10 zilizobakia kwenye bunge hili linaloendelea. Posho ya siku moja ni Sh.330,000/= kwa siku kumi ni Mil.3 na laki 3.

Kwenye bunge la bajeti Watalipwa posho ya 330,000/= kwa siku. Bunge hilo litatumia jumla ya siku 60. Hivyo mbunge mmoja atalipwa Mil.19 na laki 8, kwa muda wote wa bunge la bajeti. Kwa wote wawili watalipwa mil.39 na laki 6.

Wabunge hawa "watakopeshwa" magari ya kifahari ya kutembelea. Yani kama walikua wakitumia usafiri wa umma, kuanzia tar.20 March wameambiwa stop. Watapanda Mashangingi yanayokadiriwa kugharimu Mil.120 kwa moja, kwa wote wawili ni Mil.240.

Kwa ujumla makadirio ya gharama zote za wabunge hawa wawili kwa miezi mitano tu watakayofanya kazi watatumia jumla ya Shilingi Milioni 573 na laki 2.

Pesa hizi zinatosha kulipia mikopo ya elimu ya juu kwa semester moja kwa wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza Chuo kikuu cha St.Augustine, au Chuo Kikuu Dodoma kwa wanafunzi wanaosoma Social Science.

Pia pesa hizi zingeweza kujenga maabara za kisasa katika shule 12 Tanzania. Zingeweza kulipa mishahara ya waalimu (daraja la pili) 1,432 wa shule mbalimbali za sekondari nchini. Pia fedha hizi zingeweza kutolewa kama mkopo kwa vijana wanaohitimu vyuo vya Elimu ya juu nchini na kukosa ajira. Jumla ya vijana 573 wangenufaika kwa mkopo wa Mil.1 kila mmoja.

Lakini cha ajabu pesa zote hizi zitatumiwa na wabunge wawili tu tena kwa kipindi cha miezi mitano tu, with no expectation of return. Hatutegemei wabunge hawa watafanya lolote jipya huko bungeni litakalogharimu hizo Mil.573 watakazotumia.

Kwa lugha rahisi ni kuwa hatutegemei output ya wabunge hawa izidi input. Hakuna mbunge yeyote atakayeweza kutoa hoja zitakazo-value hizo Mil.573 watakazotumia, hata wakisaidiwa na huyo aliyewateua.

Sasa nimejiuliza, hivi katika mazingira haya ambayo hatuna rasilimali za kutosha kulinganisha na mahitaji tuliyonayo, je kulikua na ulazima wowote wa kuteua wabunge hao?

Tunahitaji pesa za kujenga maabara, kujenga shule, kulipia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mikopo, kulipa mishahara, kununua madawa etc. Lakini tumeacha vyote hivyo tumetoa kipaumbele kwa wabunge tena wa kuteuliwa.

Tafakari......😱😱
 
Back
Top Bottom