Rais Kikwete ateua wabunge wapya wawili

Rais Kikwete ateua wabunge wapya wawili

wapi juliana na mwampamba hawajakumbukwa basi angalau wapewe kuongoza mbio za mwenge kitaifa
 
kuendelea kula chakula wakati umeshiba eti kwa sababu tu kipo ni uzembe wa kufikiri kuna haja ya kutumia busara katika nafasi zetu. Eti kwa mujibu waa katiba wakati muda umeisha, it doesn't bring sense
 
Rais Kikwete amemteua Dr Grace Pujah na Bw Innocent Seba kuwa wabunge wapya katika bunge la Muungano kuanzia tar 20 Machi.

Kufuatia uteuzi huo, sasa JK amemaliza orodha wa wabunge wote kumi wa kuteuliwa kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Katiba.

===========

Hatari kwelikweli
 
Hii haijakaa sawa hata kidogo, huu ni uteuzi wa "kishkaji", hauna tija yoyote kwa taifa, ni kama vile kutafutiana ulaji tu, bunge limebakisha miezi minne, unateua watu kama si "kupeana" ni kitu gani?
 
March-Oct-2015 miezi nane watu wawili wanaondoka na Mafao ya 46,000,000x2= 92,000,000/= kwa kazi ipi hasa.
Ukiongeza na Mshahara na marupurupu 7,000,000x8= 56,000,000/=

Jumla kwa hiyo miezi nane watakuwa wamekwapua 148,000,000tsh.

Maisha Bora kwa Kila Mtanzania!
Bunge linavunjwa mwishoni mwa mwezi June na hili linaleta maswali zaidi. Wawili hao watahudhuria sana sana kikao kuanzia cha 9 cha mkutano wa 19 na vikao vyote vya mkutano wa 20, basi baada ya hapo wanapewa kiinua mgongo!!!! Jamani wanaojua zaidi hili somo watujuze!!!

Kweli, "wonders shall never end".
 
If this is true, then wacha watu waibe tu serikalini. If the president can do such a thing ili watu wapate kiinua mgongo, then wacha walio na nafasi ya kuiba waibe. Huu pia ni wizi kwa style yake kumteua mtu wakati bunge linaisha apate kiinua mgongo

Mkuu, kwa mamlaka aliyonayo rais jk ni kwamba sheria inamruhusu kufanya uteuzi wowote ule dakika chache kabla hajakabidhi kwa mrithi wake pale taifa. Ndo katiba inavyosema. Kwa hiyo hayo ni mamlaka yake. Ndo maana wananchi walitoa maoni kwa Warioba mambo hata yaangaliwe.
 
March-Oct-2015 miezi nane watu wawili wanaondoka na Mafao ya 46,000,000x2= 92,000,000/= kwa kazi ipi hasa.
Ukiongeza na Mshahara na marupurupu 7,000,000x8= 56,000,000/=

Jumla kwa hiyo miezi nane watakuwa wamekwapua 148,000,000tsh.

Maisha Bora kwa Kila Mtanzania!

Mkuu sio October ni July. Bunge linavunjwa.
 
He never been serious, au hana washauri au labda wanamuogopa.
Hizo hela zakugaramia Hawa wabunge kwa hiyo miezi 3 iliyo baki angechimba visima vingapi vya maji kwa watanzania wanaotaabika bila maji.

A very simple understanding! Sijui watanzania tulizaliwa na mwanamke gani tunakuwa namna hii.
 
haya ninmatumizi ya ofisi vibaya sasa bado kikao kimoja tu anateua wabunge kama sio kutumia madalaka vibaya
Ni mkutano mmoja wenye vikao ishirini au zaidi ndo umebakia baada ya huu wa 19 unaoendelea!
 
upuuzi kama huu ilibidi ukomeshwe na katiba mpya. Tukimuacha rais kuwa na mamlaka ya kuteua ni shida kweli. Utamteuaje mtu katika kipindi ambacho hata mbunge akifariki hakuna uchaguzi mdogo? Wasitake niamini rais analipa fadhira kwa watu wake au anakula 10% kwenye kinua mgongo chao. Upuuuzi uliopitiliza!!11
Huyo ndo raisi wetu mwana wane. Tulipewa pilau, kanga na nguo za kijani tukaona maisha bora ndo haya. Sasa ndo tunaanza kuamini kuwa mkulu ni dhaifu? Kimsingi wengine hatushangai sana maana tunamjua! Tukumbuke tu kuwa makini tusiingize ikulu mtu anayefanana na handsome boy huyu; a guy who's never serious with any serious matter. Ni shiiiida sana!
 
Mkuu, kwa mamlaka aliyonayo rais jk ni kwamba sheria inamruhusu kufanya uteuzi wowote ule dakika chache kabla hajakabidhi kwa mrithi wake pale taifa. Ndo katiba inavyosema. Kwa hiyo hayo ni mamlaka yake. Ndo maana wananchi walitoa maoni kwa Warioba mambo hata yaangaliwe.

Yote hayo tunayafahamu sana tena sana! Ila watu tuna akili tunaona something done in good faith and malicious one!
 
Tofauti na mbatia hawa wabunge walioteuliwa wamefanya nini la maana!!
 
Na hapa watasemwa washauri wake kwa ushauri wa kipotoshaji! Kweli??
 
Ukiona mpaka leo hujateuliwa na huyu dr..basi jua nyota yako ni ya busha.Ndio maana kuna watu ukitaja CCM tu povu linawatoka na sasa mara team Lowasa mara team Pinda mara Membe Mara .....malizia wote.Kumbe wanajua kuna ulaji wa bure hivi.Ngoja nitafute Team nzuri nami niingie.
 
Upuuzi mtupu,huku mishahara kimya mpaka ss.
A corrupt state!
Issue wala si hela sana ila logic. Je kutakuwa na tija gani ya ziada; kutakuwa na ongezeko la thamani ya bunge la kiasi gani kwa muda uliosalia. KWA HAKIKA MKUU JK KACHEMKA.
 
Back
Top Bottom