Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Hahah kikwete hana jipya miaka 10 serikalini. Alikua wapi. Anafucha maovu Leo ndo anataka aweke wazi. Mabadiliko lazimaa
 
Lowassa anatafuta sasa huruma aseme ameonewa. Swahiba wake JK hakuweza kumfunga lakini Magufuli hacheki na mtu. Ngojeni muone! Mnaosema mbona hajapelekwa mahakamani msiingie humu kulialia akipelekwa mahakamani!

Magufuli aanze na escrow kisha muuzaji wa nyumba za serikali
 
Sisi watanzania kweli ni vitoga, hivi huyu jamaa ametuongozaje mihula yote miwili? Kiongozi gani anamung'unya maneno.. Bure kabisa.
 
Huu ujinga unafanyika tanzania tuu Raisi anashindwa kumtaja mtuhumiwa wa richmond?
 
Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
"Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe," alisema Kikwete.
sasa kazi imewiva hakuna kukinusuru chama ila tunataka ukweli na wananchi tusipotezee hili kabisa. Maadam rais mwenyewe kaahidi kutaja mwenye Richmond ikiwa Tundu Lissu hakufanya hivyo, basi tuijenge hoja hii hadi ukweli upatikane na kazi inaanzia hapo. Ahadi ni deni msipuuze kabisa!
 
sasa kazi imewiva hakuna kukinusuru chama ila tunataka ukweli na wananchi tusipotezee hili kabisa. Maadam rais mwenyewe kaahidi kutaja mwenye Richmond ikiwa Tundu Lissu hakufanya hivyo, basi tuijenge hoja hii hadi ukweli upatikane na kazi inaanzia hapo. Ahadi ni deni msipuuze kabisa!

Kuwa na kumbukumbu mkuu alishaahidi kutaja mangapi. Yote ziliyeyuka kama bonge la barafu na alishasema hamjui mmliki wa Richmond.Kikwete aisee umeawafanya watanzania wote mazuzu na mazwazwa. We maliza muda wako utuachie nchi salama.
 
Tuacheni ushabiki lowasa hafai kabisaaaa nchi hii Malutheran na watu wa kaskazini wataifanya kama bucha vilee

Ukishafilisika sera na hoja unaanza kubwabwaja udini na ukanda hovyo kabisa.
 
Bei ya vyakula ilipanda ghafla kutoka 2005 na maisha ya mtanzania wa kawaida yamekuwa magumu kisa ni ufujwaji wa pesa nyingi za umma ambao umechangia kuaribu kabisa uchumi wa nchi. Sasa kwanini tunatega vitandawili? Niseme nisiseme? Nimtaje nisimtaje? Kashfa ya richmond ni uhalifu na mhusika au wahusika ni wahalifu. Sio tu watajwe bali pia wahaibishwe na wafungwe gerezani. Mheshimiwa Raisi tafadhali watanzania watafurahi kama utawatimizia hili!

Thubuuuutu
 
Back
Top Bottom