Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.

Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.

Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.

“Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na kushangiliwa.

“Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine.”

Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.

Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.

Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.

Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.

Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.

Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.

“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.

Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.

Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.

“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk Magufuli.

Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.

Chanzo:
Mwananchi

Huyo bulembo anafikiri hizo pesa anazolipwa sumaye ni fedha za ccm?mbona viongozi wengine hawatumii akili?hivi alipatikanaje kiongozi kama huyu hasiye jua kuwa Mshahara wa viongozi ni kutokana na kodi za watanzania woote bila kujali itikadi za kisiasa?
 
PIGA KELELE WEWEEEE ! Sinema ya Richmond imefika patamu kwa kikwete kumwaga mboga na lowassa amwage ugali
BAOBAO kwani kikwete kamtaja muhusika ni nani? nadhani ujiulize kwanini hamjamtaja jina?? na hii inatupa picha gani ukizingatia yeye ni rais wa nchi??
 
Huyu jk si alisema kuwa majangiri anawafahamu .Ni hatua gani amechukua mpaka sasa??.RICHMOND ni yake na asitufanye sisi wajinga.
 
Lowassa anatafuta sasa huruma aseme ameonewa. Swahiba wake JK hakuweza kumfunga lakini Magufuli hacheki na mtu. Ngojeni muone! Mnaosema mbona hajapelekwa mahakamani msiingie humu kulialia akipelekwa mahakamani!
Unayaamini haya? Wanasiasa hawaishi kushangaza ..."Kama hasipomtaja nitamtaja"! Miaka minane imepita na Watanzania wakiulizaswali hilo hilo; kwa nini sasa?
 
Hata Rais anaogopa kumtaja mhusika? Sasa kwa kuwa wanamrushia rungu yeye. Si achukue ushahidi azimwage makahakani. Jamani ushahidi uliopelekwa na Rais nani atashindwa kuufanyia kazi na kutupa uhalisi wa mhusika?
 
Mkuu,atawataja vipi wakati main character katika hizi MOVIE ZOTE NI YEYE MWENYEWE?

Inaweza hata ikawa sio yeye lkn nimarafiki zake anawajua so anatalk nao tu waache upuuzi....ndo yy aliyeshika dola anamaamuzi hayo......turudi mwaka huu uchaguzi kati ya EL na Magafuli nani anaonekana kuwa natabia kama za JK...bila shaka ni EL nayy pia hata ropokaropoka mambo.....
 
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
"Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe," alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.

Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.

Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa "ndiyo mzee" badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.

"Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi," alisema Bashe na kushangiliwa.

"Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine."

Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.

Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.

Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.

Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.

Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.

Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.

"...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi," alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang'anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.

Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.

Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.

"Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu," alisema Dk Magufuli.

Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.

Chanzo:
Mwananchi

Watanzania nchi nzuri ajabu!! Kuwa Rais wa hivi!! eti nitamtaja
Ninawafahamu wauza unga
Ninawafahamu majangili na kiongozi wao yuko arusha:
A whole president we have really survived in the last 10 years!!! Kwa ufahamisho anayetakiwa kuwajibika ni JK!! kwa kulea mauozo!!!!
 
Ndo kawaida ya Raisi wetu hapendi shari, kutaja taja watu hapendi..ndo Raisi wetu tuliomchagua 2005...Lkn upole wake licha yakuwa mchapakazi umeonesha watz wengi hawafurahishwi nao...lkn chakushangaza sasahivi wengi wanampigia debe EL, nayy pia nikama JK sio mwongeaji,mpole, haropokiropoki mambo......Tuchague Magufuli huyu yupo tofauti na EL na JK....husinambie ni serikali yake ndo inamfanya JK awe hivo, hapana yy ndo anamamlaka na wanamfuata yy....Sasa husinambie tabia ya EL mbowe au tundu lissu ataibadirisha....wataenenda vile EL halivyo....
 
Au jk kapiga nahau vile ili mjadala ukiwa mkal na chama chake kupoteza muelekeo ! Ambapo siku lowassa aki count attack mwamunyake akinukishe?
 
Nimelisoma gazeti la mwananchi la leo nikacheka sana...na kila mwenye nguvu katika kufikiri ataungana na mimi. Yaani Raisi mwenye mamlaka yote ya kiutawala wakati akijibu hoja ya Mh Tundu lisu akiwa huko Kigoma alisema, eti tundu lisu anataka nimtaje muhusika wa Richmond wakati yupo na anatembea naye mikoani....hahahaha..samahanini imebidi nicheke kwanza tena kidogo.

Hivi kweli tuna raisi? na mtu wa aina hii eti anatupendekezea mtu alafu tumchague awe raisi! si maajabu haya! yaani tuendelee kupata maraisi wa aina hii "nonses" yaani JK alionyesha wazi kuwa wanamsingizia Lowasa na hata tu ujasiri wa kulitaja jina lake nafsi ilimsuta.

Kama watanzania waliokuwa wanamshabikia magufuli watendelea tena nitaamini kweli tanzania imelogwa na mchawi hatari sana....Kwangu mimi Kikwete ameniambia Lowasa ni msafi na amenidhihirishia kuwa walimsingizia kwa interest zao binafsi...

Ndugu Ukitaka kujua 2005 tuliramba garasa huu ndo muda wake! Haiwezekani kiongozi wa nchi awe na kauli 3 tofauti (10yrs) katika scandal moja.
2010 Alisema kule monduli Ed kilichompata ni ajali ya kisiasa
2011 Alisema morogoro hamjui mwenye Richmond(dowans then Symbion)
2015 Anaondoka anamweleza Lisu mwenye Richmond(dowans or symbion) anatembea naye kwenye kampeni.
AJABU SANA MTU KAMA HUYU KUWA KIONGOZI TENA WA NCHI
 
Kirikou Wa Kwanza

Naomba nikuulize swali, kama rais wa nchi anajua kuna mtu amehusika na richmond tena kwa miaka 8+ akakaa kimyaaa leo ndio anakuja na kumtaja tena kwa kuficha ficha , je sisi wananchi tumweleweje, dhaifuu????

kama kweli anaitakia mema hii nchi kwanini hakumchukulia hatua mwaka 2008???

Mkuu Upepo wa Pesa, kwa ufupi naweza nikakujibu kuwa kwa serikali ya awamu ya nne; uswahiba, ujanja ujanja na udhaifu wa Kikwete ndio umelifikisha taifa hapa!
 
Last edited by a moderator:
Bei ya vyakula ilipanda ghafla kutoka 2005 na maisha ya mtanzania wa kawaida yamekuwa magumu kisa ni ufujwaji wa pesa nyingi za umma ambao umechangia kuaribu kabisa uchumi wa nchi. Sasa kwanini tunatega vitandawili? Niseme nisiseme? Nimtaje nisimtaje? Kashfa ya richmond ni uhalifu na mhusika au wahusika ni wahalifu. Sio tu watajwe bali pia wahaibishwe na wafungwe gerezani. Mheshimiwa Raisi tafadhali watanzania watafurahi kama utawatimizia hili!
 
Ndo kawaida ya Raisi wetu hapendi shari, kutaja taja watu hapendi..ndo Raisi wetu tuliomchagua 2005...Lkn upole wake licha yakuwa mchapakazi umeonesha watz wengi hawafurahishwi nao...lkn chakushangaza sasahivi wengi wanampigia debe EL, nayy pia nikama JK sio mwongeaji,mpole, haropokiropoki mambo......Tuchague Magufuli huyu yupo tofauti na EL na JK....husinambie ni serikali yake ndo inamfanya JK awe hivo, hapana yy ndo anamamlaka na wanamfuata yy....Sasa husinambie tabia ya EL mbowe au tundu lissu ataibadirisha....wataenenda vile EL halivyo....

Kumchaguwa mapadrock tutakuwa tumefanya kosa kubwa! Tunamtaka raisi ambaye hatafungamana na JK wala Mkapa ili tutoke kwenye minyororo hii ya kifisadi!
Kwa kuwa marais wastaafu wanakinga ya kuto shitakiwa basi waende zao ban wakiishi maisha yao kivyao na
wasifungamane kabisa na rais ajae!
Tunamtaka rais atakaye turudishia heshma ya taifa letu basiiii !
 
Back
Top Bottom