Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

biblia ingekuwa haijafungwa kwamba m2 asiongeze wala kupunguza neno, ningeshauri maneno haya ya mnyika ambayo niya unabii yaongezwe ili watu ktk nyakati tofauti wayarudie rudie kuyasoma, maneno yenyewe ni haya,rais kikweta ni dhaifu,kwanini haya anayoyasema leo kwanini asiyasema miaka yote hiyo iliyopita!

mkuu unauhakika biblia haingezwi; unajidanganya sana
 
Kama hawa wahusika wakitajwa naomba ushahidi kokote.
1.Wauzaji wakuu Madawa ya kulevya nchini.
2.Waliosoma pesa za ESCROW kupitia stanbik bank.

Sina zaidi!
 
Majibu ya kikwete ni utoto na sio majibu ya rais. Wezi wako bandarini business partners wake akina home shopping center
 
CCM ni ukoo wa PANYA , MWENYEKITI MPAKA MAWAZIRI WEZI TU
 
Ndio hasara ya kuwa na mgombea fisadi,lazima ufisadi uwafuate.

Mambo mapya yapo na yamejaa,mahakama ya mafisadi hawa kuanzishwa soon baada ya Magufuli kuingia ikulu.

ulikuwa wapi tangu 2008? Kwanini hamkumchukulia hatua za kisheria tangu kipindi hicho? Hebu tafutaeni sababu za kutushawishi ni kwanini tusimpe Lowasa kura tuwape ninyi mnaowasamehe wezi wa mabilioni ya fedha na kuwasweka jela wezi wa kuku na simu za elfu kumi.
Nitafute nikufundishe jinsi ya kuwa fowarsee na kufikiri kwa faida.
Jambo lingine ni hili la washabiki wa ccm wenye akili ndogo kutaka kuongoza akili kubwa. Haiwezekani.
 
kweli hii nchi ya ajabu rais anajua muusika anashindwa kuchukua hatua za kisheria anaanza kuongea siasa za majukwaani ili kupata kura,tutaikataa CCM oct
 
raisi anamjua muhusika halafu anaongea majungu bila kuwa wazi

Laowassa hafai jamani tuache ushabiki
Tupe sababu kwanini Lowasa hafai???
Alishawahi kusema hajui owners wa Richmond na wahusika hawajui

As a commander in chief, aliaminika, sasa leo anakuja kisiasa zaidi

This kasshfa is not over

Richmond=Richard Monduli.Walifanya wizi wa kimkakati(Strategic theft) jinsi ya kupata ushahidi beyond no doubt ni ngumu.Na sheria zilivyo najua huzijui ila Fisadi EL baada ya kukaa kwa muda inaonekana wamemshauri kwamba ukitaka kulikwepa sema "Wakupeleke mahakamani" wakati kama ni kweli yeye siyo MWIZI kwanini HAUMIZWI NA UFISADI na RUSHWA KABISA,Kwanini anagawa sana PESA na Kwanini UHALALI WA UTAJIRI WAKE NI SIRI KUBWA.Aseme jinsi alivyopata ili na sisi tunaotafuta tufuate nyayo zake.NI MWIZI TU.....

Kwanini hayuko jela au hata mahakamani huyo mhusika, anatajwa kimajungu majungu tu ndio maana raia wameamua kupuuza tu.

Hilo lipo wazi lowasa mwizi sana mahakama ya mafisadi ikija ataisoma namba fisadi huyu.

Kama Amiri jeshi mkuu ndo yuko hivi!!basi na amalize muda wake naondoke.
Hapa mimi nina mashaka!! Nnachoshindwa kuelewa ni kwamba kama kweli rais anamfahamu kwanini kwa miaka yooooote 8 yko kimya wala hajachukua hatua zozote?????? why????? why??? au ndio udhaifu john mnyika aliousema bungeni??!! kwa mtazamo wangu kama rais anamjua muhusika na kakaa kimya kwa miaka 8 eti leo ndio anakuja na kusema muhusika ni fulani tena kwa kuficha ficha, Rais asiye na maamuzi hafai katika hii nchi na ndio maana hata wasemeje tunataka mabadiliko, tunamtaka Lowassa!!!
 
Mwenye Richmond hawezi kuwa Lowassa. Maana kwenye kampeni za 2010 Kikwete alimnadi Lowassa kuwa NI MTU SAFI.
 
Nasikitika kutangaza kifo cha jambazi sugu aliyetambuliwa kwa jina CCM. Mazishi yanatarajiwa kufanyika tarehe 25 Oct. Watanzania wote mnaombwa kuhudhuria kwenye vituo vyenu vya kupigia kura ili tuweze kumsindikiza jambazi huyu kwenye safari yake ya mwisho. 2015 Lowasa#mabadiliko#
 
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.

Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.

Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.

“Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na kushangiliwa.

“Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine.”

Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.

Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.

Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.

Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.

Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.

Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.

“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.

Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.

Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.

“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk Magufuli.

Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.

Chanzo:
Mwananchi

naam! ni msimu mwingine watz kugeuzwa mazuzu na wanasiasa,hasa wanasiasa uchwara.
 
Kirikou Wa Kwanza
Kitu gani hukijaelewa hapo ndg yangu! Kama unafatilia Mwakyembe alimtaja Lowassa ndio muhusika wa Richmond na akatoa option mbili Lowassa kujizuru au kujadiliwa na bunge. Kama haitoshi JK pia kamtaja jana ingawa alimtaja kimafumbo, lakini tumemuelewa! Sasa ni zamu ya fisadi Lowassa kwa mdomo wake atuambie muhusika wa Richmond ni nani? Atuambie kwa ushahidi wa kuridhisha, Watanzania tunataka kujua kama sio yeye ni nani?
Naomba nikuulize swali, kama rais wa nchi anajua kuna mtu amehusika na richmond tena kwa miaka 8+ akakaa kimyaaa leo ndio anakuja na kumtaja tena kwa kuficha ficha , je sisi wananchi tumweleweje, dhaifuu????

kama kweli anaitakia mema hii nchi kwanini hakumchukulia hatua mwaka 2008???
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana kweli akawa anamuogopa!? Hapana sidhani.

Kwa sababu anajua akitaja cha moto atakiona.Maana 2010 alimpigia debe kwamba ni msafi sana,hakuna mtu safi kama Lowassa, na kwamba ile ilikuwa ajali ya KISIASA,leo AJALI ya KISIASA imekuwa TUHUMA za KISIASA???

Akinitajia nani yupo nyuma ya ESCROW leo hakika nampigia KURA Magufuli,vinginevyo rais ANYAMAZE sasa tumeshachoka na RICHMOND
 
raisi anamjua muhusika halafu anaongea majungu bila kuwa wazi
hao ni marafiki tangu wakiwa vijana. ni siasa tu zimewafanya watofautiane. kwa hiyo hata kutajana hadhari ni shida. ukitaka kunielewa angalia hotuba ya kikwete siku ya ufunguzi wa kampeni pale jangwani. alisema hatutaki rais aliye na utajiri usioeleweka kaupataje, lakini wananchi walipomuambia arudie jamaa alijifikiriiiiiiiya aka-nutrilize kidizaini fulani kwa kuingiza neno makandokando.
 
Kirikou Wa Kwanza

Naomba nikuulize swali, kama rais wa nchi anajua kuna mtu amehusika na richmond tena kwa miaka 8+ akakaa kimyaaa leo ndio anakuja na kumtaja tena kwa kuficha ficha , je sisi wananchi tumweleweje, dhaifuu????

kama kweli anaitakia mema hii nchi kwanini hakumchukulia hatua mwaka 2008???

Kwa akili yangu ndogo inaniambia kwamba RAIS wangu mpendwa ni muhusika wa moja kwa moja na KADHIA ya RICHMOND.

Aliposhindwa kutuambia nani muhusika mkuu wa ESCROW akadiriki kutetea wizi wa mabilioni ,ilinishangaza.Hakika watuambie kwanza nani muhusika mkuu wa ESCROW ACCOUNT na MAJANGILI wa MENO YA TEMBO kama atashindwa basi ninamsihi RAIS wangu Mpendwa sasa anyamaze.Ila ajue tunajuta kumfahamu
 
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.

Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.

Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.

“Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na kushangiliwa.

“Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine.”

Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.

Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.

Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.

Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.

Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.

Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.

“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.

Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.

Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.

“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk Magufuli.

Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.

Chanzo:
Mwananchi

Ajaribu kutoka adharani dunia itajua mengi nyuma ya pazia
 
PIGA KELELE WEWEEEE ! Sinema ya Richmond imefika patamu kwa kikwete kumwaga mboga na lowassa amwage ugali
 
Mbona jk analialia wakati dola kaishika yeye?na bado mijitu ipo tu inashabikia sisiemu wakati ina mwenyekiti dhaifu na kilaza asiyejua majukumu yake,

c ulimchagua mwenyewe 2010...sasahivi tunataka jembe magufuli...Jk anaondoka huyo
 
Back
Top Bottom