Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Laowassa hafai jamani tuache ushabiki

Lowassa hafai hata bure, Watanzania wengi wao ni wezi tu ndio maana wanamshabikia Lowassa. Akitokea kiongozi msafi na mwenye msimamo utaona kuna kundi la majizi linampinga vita. Magufuli ni kiongozi msafi na ni mtu mwenye msimamo dhabiti. CHAGUA MAGUFULI. #HapaKaziTu
 
Kumchaguwa mapadrock tutakuwa tumefanya kosa kubwa! Tunamtaka raisi ambaye hatafungamana na JK wala Mkapa ili tutoke kwenye minyororo hii ya kifisadi!
Kwa kuwa marais wastaafu wanakinga ya kuto shitakiwa basi waende zao ban wakiishi maisha yao kivyao na
wasifungamane kabisa na rais ajae!
Tunamtaka rais atakaye turudishia heshma ya taifa letu basiiii !
Wewe kweli kipofu haswa. Hivi wewe huyo mwizi anaweza kutuletea mabadiliko kweli?? Hapana jamani Lowassa hawezi kutuletea mabadiliko chanya, zaidi sana ataiharibu hii nchi mara elfu ya Kikwete. Mtu mwenye nia ya dhati kutuletea maadiliko hata ukimsikia tu jinsi anavyoongea ni JOHN POMBE MAGUFULI. Huyu MAGUFULI anaongea kutoka moyoni na mara nyingi sana mtu hutenda kile kilichopo moyoni mwake. #HapaKaziTu CHAGUA MAGUFULI
 
harakatinews hamumjui bulembo nyie? mtu aliyetumia mwamvuli wa soka kuingia siasa anajua nini kwenye siasa zaidi ya kujifanya mropokaji kusudi akumbukwe . Bulembo anadhani kuwa mshahara unatolewa na ccm (hii ndio athari ya kukosa elimu pana) anapaswa aelewe kuwa mshahara na marupurupu ya kiongozi mstaafu yapo kwa mujibu wa katiba na sio kwa pleasure ya ccm. hakuna mwenye uwezo wa kuzuia marupurupu hayo sanasana anajitafutia kuvuliwa kinga na kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi. ccm haina jipya na ndio maana shule za wazazi zinakufa kifo cha mende na miradi yao pia. akina bulembo kazi yao kujilipa posho na kuzunguka kupiga propaganda tu, hakuna ubunifu wowote unaolenga kuifufua jumuia ya wazazi. Bulembo anapaswa kujua kuwa tulianza na Mungu hata kama hapendi, tupo na Mungu japo hakubali na tutamaliza na Mungu apende asipende. vichinjio tunavyo na havinunuliki safari hii. mtakuja na pesa zenu tutazila na siku ya kupiga kura tunampigia Lowassa. na ole wenu mahali pengine tutawakamatisha kwa takukuru au tutaangalia namna bora ya kuwatia adabu
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.

Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.

Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.

“Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na kushangiliwa.

“Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine.”

Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.

Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.

Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.

Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.

Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.

Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.

“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.

Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.

Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.

“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk Magufuli.

Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.

Chanzo:
Mwananchi
 
kama jk alimfaham mwiz alikuwa wap sikuzote na alisubil nn na mpaka sasa anasubil nn kumkamata?, hiv kwel rais anaweza akakosa meno kwa mwiz kama anavyodai?,aache siasa nyepesi kama hzo na kwa kuwa amesema anamfaham ampeleke mahakaman tuone na c kulalamika jukwaan... ...nchi yetu tabu sana,rais analalamika,mawazir na mpaka mabaloz hakuna mweny msaada zaid,kilichopo wakae pemben na wengne waongoze nchi,c lazma ccm,r.i.p ccm kufa kabsa
 
Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.
Tundu Lissu Kaweka mtego ambao kwa upande wowote utapanic utunaswa.
 
nimeandika jinsi kikwete alivyoisafisha njia ya lowasa...lakini mmechomekea ujumbe huu juu ya ule wa kikwete amtaja muhusika wa richond..kwa mfumo huu hata nyie mnashindwa kuaminika...na ni mara nyingi topiki zinageuzwa jamani wanaofanya hivi wanaishushia heshima jamii forum..chombo ambacho kimekubalika sana

Ukiona hivyo ujue kuwa topic yako ni fupi mno na hajitoshelezi kujitegemea!
WAKATI MWINGINE MNAJITEKENYA WENYEWE NA KUCHEKA WENYEWE HUKU MKITARAJIA 'BATACHEKA TUUU!'
 
Wewe kweli kipofu haswa. Hivi wewe huyo mwizi anaweza kutuletea mabadiliko kweli?? Hapana jamani Lowassa hawezi kutuletea mabadiliko chanya, zaidi sana ataiharibu hii nchi mara elfu ya Kikwete. Mtu mwenye nia ya dhati kutuletea maadiliko hata ukimsikia tu jinsi anavyoongea ni JOHN POMBE MAGUFULI. Huyu MAGUFULI anaongea kutoka moyoni na mara nyingi sana mtu hutenda kile kilichopo moyoni mwake. #HapaKaziTu CHAGUA MAGUFULI

Magufuli anakwenda kuwa tv tu pale ikulu! remote atakuwa nayo JK na Mkapa ili waendelee kutuwekea channels wanazotaka wao! au kutopoteza muda ED ni bora zaidi kwa sasa kwa sababu yuko nje ya mfumo kandamizi wa CHAMA CHA MAJIZI
 
"CCM mkitaka #KURA yangu semeni ukweli nani anahusika na hizi tuhuma? na wahusika wamechukuliwa hatua gani?
-Katiba pendekezwa nani aliyaondoa maoni ya wananchi ambayo yalikuwepo kwenye rasimu ya Warioba?
-Mabehewa feki
-Kiwira
-Richmond
-Epa
-Escrow
-Epa
-Dowans
-IPTL
-NET GROUP SOLUTIONS
-Usafirishaji wa wanyama nje ya nchi mfano twiga alipandaje ndege?
-Biashara ya pembe za ndovu
-Biashara ya madawa ya kulevya
-Meremeta
-Mikataba ya gesi na mafuta
-Uuzwaji wa nyumba za serikali
Nahitaji majibu ya hayo maswali siyo porojo tuuu za kipumbavu, za kusema niseme au nisiseme!!!.Harafu Raid mzima bila hata aibu unasema eti utamtaja muhusika asipotaja TUNDU LISU!!!, Wewe ndo mkuu wa nchi na umetajwa kuwa ndo mhusika mkuu wa scandal ya Richmond , raid huna haja ya kutaja wewe agiza vyombo vyako vifanye Kazi.
 
Ndugu Ukitaka kujua 2005 tuliramba garasa huu ndo muda wake! Haiwezekani kiongozi wa nchi awe na kauli 3 tofauti (10yrs) katika scandal moja.
2010 Alisema kule monduli Ed kilichompata ni ajali ya kisiasa
2011 Alisema morogoro hamjui mwenye Richmond(dowans then Symbion)
2015 Anaondoka anamweleza Lisu mwenye Richmond(dowans or symbion) anatembea naye kwenye kampeni.
AJABU SANA MTU KAMA HUYU KUWA KIONGOZI TENA WA NCHI
Hata mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, Lowassa pia ni kigeu geu tena sana. Mfano mzuri soma hizi kauli zake alizotoa nyakati tofauti ndani ya miezi 4.
1. "Serikali ya Kikwete imefanya mambo mengi mazuri na mimi nikiteuliwa nitaanzia alipoishia yeye". Hapa alikuwa Arusha
2. "Rafiki yangu huyu ameharibu sana uchumi, bei ya sukari imepanda, bei ya mchele imepanda" Hapa ni baada tu ya kujiunga CHADEMA.
3. "Mimi sitaondoka CCM, asiyenitaka ndani ya CCM aondoke yeye".
4. "Mimi sina Plan B, wala sitegemei jina langu kukatwa, nani kakuambia jina langu litakatwa"?
5. CCM siyo baba yangu wala sio mama yangu.

Kiongozi yeyote mwenye kigeu geu hafai hata kidogo. Lowassa ni mtu mwenye kigeu geu hafai kuwa rais wa Tanzania. CHAGUA MAGUFULI. #HapaKaziTu
 
"CCM mkitaka #KURA yangu semeni ukweli nani anahusika na hizi tuhuma? na wahusika wamechukuliwa hatua gani?
-Katiba pendekezwa nani aliyaondoa maoni ya wananchi ambayo yalikuwepo kwenye rasimu ya Warioba?
-Mabehewa feki
-Kiwira
-Richmond
-Epa
-Escrow
-Epa
-Dowans
-IPTL
-NET GROUP SOLUTIONS
-Usafirishaji wa wanyama nje ya nchi mfano twiga alipandaje ndege?
-Biashara ya pembe za ndovu
-Biashara ya madawa ya kulevya
-Meremeta
-Mikataba ya gesi na mafuta
-Uuzwaji wa nyumba za serikali
Nahitaji majibu ya hayo maswali siyo porojo tuuu za kipumbavu, za kusema niseme au nisiseme!!!.Harafu Raid mzima bila hata aibu unasema eti utamtaja muhusika asipotaja TUNDU LISU!!!, Wewe ndo mkuu wa nchi na umetajwa kuwa ndo mhusika mkuu wa scandal ya Richmond , raid huna haja ya kutaja wewe agiza vyombo vyako vifanye Kazi.

Muhusika wa uchafu wote huo ni Lowassa na Friends of Lowassa na Team Lowassa.
 
Magufuli anakwenda kuwa tv tu pale ikulu! remote atakuwa nayo JK na Mkapa ili waendelee kutuwekea channels wanazotaka wao! au kutopoteza muda ED ni bora zaidi kwa sasa kwa sababu yuko nje ya mfumo kandamizi wa CHAMA CHA MAJIZI

Mkuu wewe ni hatarii,hahaahaa yani mzee pombe ni flat scren Lg samsum..hatariii
 
Richmond=Richard Monduli.Walifanya wizi wa kimkakati(Strategic theft) jinsi ya kupata ushahidi beyond no doubt ni ngumu.Na sheria zilivyo najua huzijui ila Fisadi EL baada ya kukaa kwa muda inaonekana wamemshauri kwamba ukitaka kulikwepa sema "Wakupeleke mahakamani" wakati kama ni kweli yeye siyo MWIZI kwanini HAUMIZWI NA UFISADI na RUSHWA KABISA,Kwanini anagawa sana PESA na Kwanini UHALALI WA UTAJIRI WAKE NI SIRI KUBWA.Aseme jinsi alivyopata ili na sisi tunaotafuta tufuate nyayo zake.NI MWIZI TU.....
KUMBUKENI TANZANIA TAJIRI SIO EL PEKEE WAPO WENGI HUSUSANI KWENYE HILI GARI MOSHI LA KIJANI,KUNA KASHFA NYINGI NA USHAHIDI UPO KATIKA MITANZANDO NA MABENK KWA MIAMALA MABLIMBALI ILA WATANZANIA HATUJAONA HATUA MADHUBUTI ZIKICHUKULIWA
UFISADI TANZANIA SIO RICHMOND T
1 .SCROL
2.kagoda
3.MEREMETA
4.EPA
;5.MABEHEWA FEKI
6.SUKARI
DREAM IS NO WHAT YOU SEE IN SLEEP BUT IS THAT THING WICH CAN NOT LET YOU SLEEP
KAMA WATANZANIA TUNATAKA TANZANIA YA AINA GANI?? TUNATAKA KUISHI VIPI? JE TUNATEGEMEA SYSTEM ILE ILIYO LETA MATATIZO INAWEZA TATUA MATATIZO YETU?? KILA MTU AFIKIRIE ALIPENDA NN KATIKA MAISHA YAKE NA KA ACHIEVE NN KAMA UMEFANIKIWA UMEPITA NJIA HALALI? KAMA HUJAFANIKIWA UNADHANI KWA NN HUJAFANIKIWA??
 
Hata mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, Lowassa pia ni kigeu geu tena sana. Mfano mzuri soma hizi kauli zake alizotoa nyakati tofauti ndani ya miezi 4.
1. "Serikali ya Kikwete imefanya mambo mengi mazuri na mimi nikiteuliwa nitaanzia alipoishia yeye". Hapa alikuwa Arusha
2. "Rafiki yangu huyu ameharibu sana uchumi, bei ya sukari imepanda, bei ya mchele imepanda" Hapa ni baada tu ya kujiunga CHADEMA.
3. "Mimi sitaondoka CCM, asiyenitaka ndani ya CCM aondoke yeye".
4. "Mimi sina Plan B, wala sitegemei jina langu kukatwa, nani kakuambia jina langu litakatwa"?
5. CCM siyo baba yangu wala sio mama yangu.

Kiongozi yeyote mwenye kigeu geu hafai hata kidogo. Lowassa ni mtu mwenye kigeu geu hafai kuwa rais wa Tanzania. CHAGUA MAGUFULI. #HapaKaziTu

Acha ushabiki, ccm wangefuata utaratibu wa uchaguzi wa m/kiti wao yote yasingetokea. Nikweli kuna mazuri ambayo jk amefanya ila mabaya yake ndio njia ya mpinzani. Pia naomba nikuulize, jk alizingatia nini alipokuja na Sera ya 'maisha bora kwa kila mtanzania? Je kafaulu au kafeli?

Bila elimu hakuna maisha bora. Naomba upeni kura Lowassa.
 
Hata mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, Lowassa pia ni kigeu geu tena sana. Mfano mzuri soma hizi kauli zake alizotoa nyakati tofauti ndani ya miezi 4.
1. "Serikali ya Kikwete imefanya mambo mengi mazuri na mimi nikiteuliwa nitaanzia alipoishia yeye". Hapa alikuwa Arusha
2. "Rafiki yangu huyu ameharibu sana uchumi, bei ya sukari imepanda, bei ya mchele imepanda" Hapa ni baada tu ya kujiunga CHADEMA.
3. "Mimi sitaondoka CCM, asiyenitaka ndani ya CCM aondoke yeye".
4. "Mimi sina Plan B, wala sitegemei jina langu kukatwa, nani kakuambia jina langu litakatwa"?
5. CCM siyo baba yangu wala sio mama yangu.

Kiongozi yeyote mwenye kigeu geu hafai hata kidogo. Lowassa ni mtu mwenye kigeu geu hafai kuwa rais wa Tanzania. CHAGUA MAGUFULI. #HapaKaziTu
Sawa nikigeugeu pia lakini angalia mantiki ya ukigeugeu wa Ed na wa JK! Ed ana reason kahama chama,yuko upande tofauti sasa! Lazima mipigo yake iwe tofauti sasa si ile ya alikotoka! Nipe sababu nzito ya JK kugeuka geuka katika scandal hii ya richmond?
Lakini pia mambo aliogeuka Ed ni simple issues Richmond ni ZOMBI limutumaliza watanzania sasa tulipokuwa tunamalizwa na zombi hili halafu unamwona mkuu wa nchi haeleweki UNASHANGAA! toka usingizini wewe angalia mbere
 
Back
Top Bottom