Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Kikwete amtaja mhusika wa Richmond

Rais Jakaya Kikwete amesema anashangazwa na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani.

Kikwete aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.

Kadhalika, Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.

Richmond
Suala la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi wanaosababisha umaskini nchini.

Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.

Bashe alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.

“Umesema utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na kushangiliwa.

“Ni lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta biashara nyingine.”

Mgombea huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk Magufuli tofauti zimekwisha.

Bashe alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.

Hata hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya chama hicho.

Huku akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.

Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba hakijafanya chochote tangu uhuru.

Akiwahutubia wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya kitu.

“...Analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.

Magufuli na michango ya shule
Dk Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.

Alisema anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.

“Kuna mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,” alisema Dk Magufuli.

Akiwa Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.

Chanzo:
Mwananchi

Huyu jakaya nilianza kuwa na wasiwasi na kichwachake toka alivoanza kuanguka kwenye jukua kipindikile alipokua anaombakura,Ivi atawezaje kutumia cheo chake kumsweka ndani babu seya na watoto wake ndani alafu akamuacha mwizi mkubwa namnahiyo mpaka leo ndio amtaje?nina mashaka na kichwa chake.
 
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu kikwete amekiuka kanuni na sheria za NEC.

Ni kosa kuchochea au kuleta tafran ya aina yeyote, inayoegemea katika chama chochote nchini..

Yeye kama rais mstaafu anastahili kukaa akiombea amani ktk kipindi hiki tukielekea uchaguzi mkuu.

Kitendo cha kikwete kwenda kigoma na kuongelea Richmond ni ukosefu wa maadili na kosa hili ni kubwa sana kitaifa na kimataifa!

Hakupaswa kisheria kuingilia mambo haya kipindi hiki.. Alikuwa na muda wa kuongelea mikataba mibovu kama Richmond, Escow na gas.. Muda mrefu na hakufanya hivi!! Kwanini kipindi hiki ndo aanze kuongea jukwaani?! THIS IS NOT FAIR

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
sasa kazi imewiva hakuna kukinusuru chama ila tunataka ukweli na wananchi tusipotezee hili kabisa. Maadam rais mwenyewe kaahidi kutaja mwenye Richmond ikiwa Tundu Lissu hakufanya hivyo, basi tuijenge hoja hii hadi ukweli upatikane na kazi inaanzia hapo. Ahadi ni deni msipuuze kabisa!


Siamini kikwete ambaye amekuwa raisi wa ccm kwa miaka 10 atafanya hivyo. Sijawahi kuota ndoto Tz inaweza kua n araisi mpumbavu na juha wa kupindukia.

Siamini kwanza kama haya maneneo kayasema yeye na bado ajiite raisi wa nchi.

Ninashindwa kupata neno zuri la kumwita zaidi ya kuona anajiletea laana kubwa kwenye mabega yake.

Alikuwepo waakti wa ufisadi, akabunda kama bundi juu ya mti.

Lowasa akajiuzuru kuikoa serikali yake isianguke, akachekelea.

Hakuonyesha hata siku moja kujali wala kuchukua hatua dhidi ya ufirauni wa seriakli yake.

Alipoulizwa RICHMOND, Kikwete huyu huyu akasema hamfahamu mwenye richmond.

210 akasimama monduli akimnadi Lowasa kwamba ni mtu safi na kwamba wananchi wamchague.

Lowasa kamtaja yeye kuwa ndiye mwenye richmond, ndipo naye kaibuka toka shimoni kusema anamfahamu mwenye richmond.

Huyu mtu aitwaye kikwete, anapata wapi ujasiri wa kuwatukana Watanzania matusi makubwa hivi?

Lini kikwete atakuwa na hofu ya Mungu japo awe mkweli hata kidogo?

NInamba kuanzia sasa Divine Justice ishuke kwa Watanzania. Divine Justice ishughulike na huyu mtu mwongo aitwaye jakaya mrisho kikwete. Aliyotufanya yametosha.
 
Kuwa na kumbukumbu mkuu alishaahidi kutaja mangapi. Yote ziliyeyuka kama bonge la barafu na alishasema hamjui mmliki wa Richmond.Kikwete aisee umeawafanya watanzania wote mazuzu na mazwazwa. We maliza muda wako utuachie nchi salama.
Kwani jambo ukiwa hulijui leo, ni lazima usilijue na kesho pia? Inawezekana ni kweli hakuwa akijua huko nyuma, je kama baadaye ndio amekuja kujua nini kosa hapo? Tuwe logic kidogo
 
:mad2::mad2: chochea chochea :A S 41::A S 41: Chochea chochea :mad2::mad2:
 
Mwizi wa richmond ni kikwete kama anakataa amshitaki lowassa kama kweli ni mkweli

hawezi ataishia kujibu hivyo tu.aliyeenda marekani kukutana na kampuni ya richmond ni kikwete

nakuhakikishia kikwete hawezi kuthubutu hata siku moja.lowassa anamweshimu tu hakutaka kumwaabisha kikwete
 
Kwanza JK alisema hamjui mmiliki wa Richmond, leo hii anasema anamjua na atamtaja. JK ni mtupu kabisaa na anajiweka mahali pabaya. Kinga ikiisha anaweza shitakiwa kwa uhujumu uchumi
 
Mwizi wa richmond ni kikwete kama anakataa amshitaki lowassa kama kweli ni mkweli

hawezi ataishia kujibu hivyo tu.aliyeenda marekani kukutana na kampuni ya richmond ni kikwete

nakuhakikishia kikwete hawezi kuthubutu hata siku moja.lowassa anamweshimu tu hakutaka kumwaabisha kikwete

Lkn kwakuwa ameanza kuyachokoza mwenyewe basi ajiandae kwa lolote maana huyo lowasa nayeye kama binadamu anamwisho wa uvumilivu
 
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu kikwete amekiuka kanuni na sheria za NEC.

Ni kosa kuchochea au kuleta tafran ya aina yeyote, inayoegemea katika chama chochote nchini..

Yeye kama rais mstaafu anastahili kukaa akiombea amani ktk kipindi hiki tukielekea uchaguzi mkuu.

Kitendo cha kikwete kwenda kigoma na kuongelea Richmond ni ukosefu wa maadili na kosa hili ni kubwa sana kitaifa na kimataifa!

Hakupaswa kisheria kuingilia mambo haya kipindi hiki.. Alikuwa na muda wa kuongelea mikataba mibovu kama Richmond, Escow na gas.. Muda mrefu na hakufanya hivi!! Kwanini kipindi hiki ndo aanze kuongea jukwaani?! THIS IS NOT FAIR

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Unaweza kuitaja na kuinukuu kanuni na sheria hapa?
 
Back
Top Bottom