Rais Kikwete adanganywa tena

Ndio maana tunasema serikali imekosa umakini ukianza na mkuu wa nchi,kazi kwelkwel
 
Anapenda kudanganywa kwake ni fahari sana anapodanganywa! yaani kweli hio document ilikua kubwa kiasi gani ashindwe kuipiga jicho au alikua busy kiasi gani hicho? ni uzembe wake tu na pengine waliofanya hivyo walishafanya mambo mengine kwa style hio hio na wakafanikiwa!
 
Hajadanganywa - Amefanya Makusudi!
AU ndio vile visa vyake na MWALIMU? Si kulikua na thread humu ndani ilikua inaelezea jinsi Teacher alivyomtimua dogo? Labda kuna kajiukweli flani hivi, ngoja tusubiri wataalamu wa uchambuzi waaamke!
 
...........Nimeangalia michango ya wanaJF waliochangia hii thread wamechoka na akili za raisi wao.Mimi sichangii maana nitasema maneno magumu halafu nipigwe ban.
 
"Hata kama kuna mtu alitaka makao makuu yawe Nyamisisi, kwa kweli haikupaswa hiyo Nyamisisi kuchomekwa hivyo. Hata mngeniuliza mimi makao makuu yawe wapi, ningesema lazima yawe Butiama tu," alisema Pinda na kushangiliwa.

Pinda pia alimpa fursa mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, kutoa kauli yake kuhusu suala hilo, ambaye alisema yeye asingependa kuliingilia suala hilo.

"Hili suala halina tatizo, ninyi na wananchi wote mtakavyoamua ndivyo iwe hivyohivyo," alisema Mama Maria
.
hapa ndio utaona tofauti kati ya mama mwenye hekima na busara na mama shughuli ubwabwa na ndembendembe!!
 
Huko Amerika anakoenda si ndiyo anatuuza kabisa maana hata lugha kidogo ni tofauti.Hivi ana wadanganyifu wangapi pale Ikulu? Kama mambo hayo madogo yanamshinda kiasi kwamba anaishi kwa kudanganywadanganywa kila siku, je mambo kama ya umeme atayaweza?
 
Ndiyo shida ya kusaini nyaraka ukiwa na haraka ya kwenda ughaibuni. Everything you do at a crisis.
 
Pinda alikiri bayana kuwa Rais alisaini tangazo hilo akijua kuwa kilichoandikwa ni makao makuu kuwa Butiama bila kujua eneo lililoandikwa ni Nyamisisi.

"Hata kama kuna mtu alitaka makao makuu yawe Nyamisisi, kwa kweli haikupaswa hiyo Nyamisisi kuchomekwa hivyo. Hata mngeniuliza mimi makao makuu yawe wapi, ningesema lazima yawe Butiama tu," alisema Pinda na kushangiliwa.

Namshukuru Mungu hapa Waziri Mkuu hakusema angekuwa angekuwa ameishamchukulia hatua mtu aliyeichomeka hiyo Nyamisis manake yanaweza yakawa yale yale ya DJ!!
 
Hayo ni makosa ya Raisi wetu kwa nn anadondoka signature bila kusoma kilichoandikwa ndani?. Mi nahis muda wa safari ulikuwa umekaribia akaamua kusign bila kusoma ila awahi airport.
 
Nimesikitishwa na kauli ya PM kusikitika, alitakiwa aagize aliyedanganya apatikane, ashughulikiwe na kutengua uamuzi wa makao makuu ya wilaya ya Butiama kuwa Nyamisisi.
 
Huyu jamaa alwlaways thinking kusafiri hana muda wa kukaa na na kusoma between the lines..
 
• Asaini tangazo la serikali lililochakachuliwa



Pinda alikiri bayana kuwa Rais alisaini tangazo hilo akijua kuwa kilichoandikwa ni makao makuu kuwa Butiama bila kujua eneo lililoandikwa ni Nyamisisi.

Ahaaa, tatizo la raisi wetu liko hapa,

Huwa hasomi "documents" anazopelekewa, yeye huwa anatia saini tu haraka haraka.

Na inaonekana jamaa walishamuona ni mvivu wa kusoma kwahiyo wameamua kupitia hapo hapo.

Walimchomekea kwenye sheria ya uchaguzi, akasaini baada ya Dr. na hili nalo la kuanzisha wilaya wanamchomekea? kwani ni refu kiasi gani hadi ashindwe kusoma kwanza.

Hii ni dalili ya kwa nini nchi hii ina mikataba feki mingi, watu wetu huwa hawasomi, wanasaini tu.
 
Sijawai ona serekali Kama hihi aiishi vituko hivi raisi kabla ajasaini hakuna washauri ? Na huyuPinda kila siku anasema angekuwa na uwezo angemuwajibisha aliye chomeka ilo Jina la Musisi badala ya Butiama yeye majukumu yake ni yapi?kila siku eye kulalamika tuuu
 
kila siku rais anadanganywa. hajasoma kwani huyu?ndo tatizo la kuchagua marais kisa mahandsome
 
alikuwa na haraka ya ku'sign ili awahi airport, alipiga saini akiwa mlangoni magogoni anatoka kuelekea uwanja wa ndege safarini america, hii habari ya uhakika kabisa kutoka chanzo cha magogoni.
 
Rais Kikwete amedanganywa tena mara ya 13 tangu aingie ikulu.

Hii ni rekodi yake ambayo itaduma pengine kwa miaka 50 ijayo au zaidi.Kwa mujibu wa gazeti la Tanzania daima la leo , Rais amesaini tangazo la serikali la kusudio la kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Butiama ambayo makao makuu yake yatakuwa Nyamisisi badala ya kuwa Butiama yenyewe kama ilivyokuwa imekubaliwa awali kati ya wananchi kama ilivyoahidiwa na Rais Kikwete.

Waziri mkuu Pinda alipokwenda Butiama kutembelea kaburi la Nyerere alikumbana na upinzani mkali kutoka wananchi alipokuwa ktk mkutano wa hadhara. Wananchi wengi hawakufurahishwa na hatua hiyo na wakamuuliza kwanini Rais amevunja ahadi yake aliyowaambia watu wa Butiama ya kuwapa wilaya ambayo makao makuu yake yangekuwa Butiama ili kumuenzi Baba wa Taifa?

Pinda alikiri kuwa Rais alisaini akijua kuwa makao makuu yatakuwa Butiama. Akaendelea, huyo aliyebadilisha tangazo la serikali atakuwa hajafanikiwa. Nawaomba ninyi wananchi mlichukulie hilo tangazo kama pendekezo, ili baadaye mtoe maoni yenu kuhusu makao makuu.

Pinda alikubaliana na wananchi tofauti na tangazo la serikali lililosainiwa na bosi wake, akasema, ukiniuliza mimi nitasema makao makuu yawe Butiama ili kumuenzi Nyerere.

My take:

Hivi JK huwa anasaini vitu asivyovisoma mwenyewe? Je, kama anakosa muda wa kusoma vitu vidogo kama tangazo anawezaje kutafakari na kuja suluhu ya matatizo ya nchi hii? Au yuko busy sana na safari za nje na zimemzidi sana

Source Tanzania daima.
 
Back
Top Bottom