Rais Kikwete adanganywa tena

Rais Kikwete adanganywa tena

Anapenda kudanganywa kwake ni fahari sana anapodanganywa! yaani kweli hio document ilikua kubwa kiasi gani ashindwe kuipiga jicho au alikua busy kiasi gani hicho? ni uzembe wake tu na pengine waliofanya hivyo walishafanya mambo mengine kwa style hio hio na wakafanikiwa!

bora uwakumbushe. lakini si yeye, ni matokeo ya elimu ya kupewa na si ya kustruggle.
 
“Hili la Butiama kwa kweli linaleta manenomaneno. Sisi serikalini tulidhani ukiwa na wilaya ya Butiama na makao makuu ni lazima yawe Butiama, ili tumuenzi Baba wa Taifa.

Hata hivyo, alisema pamoja na tangazo hilo kuchomekwa neno Nyamisisi, bado mtu aliyefanya hivyo hajafanikiwa, kwani tangazo hilo sio uamuzi wa mwisho wa kuhusu suala hilo.

It defeats logic, kama ni hivyo basi huyu bwana anataka tuamini kuwa inawezekana hata wakuu wa mikoa na wilaya baadhi yao majina yamechomekwa
 
Haya kama ni kweli basi hayabebeki? Kwani Rais akipelekewa kitu kusaini si kunakuwa na watu weledi wamekisoma na kukipitia na kujiridhisha au hao hao ndio wachakachuaji? Kama ni kweli basi hapa nategemea Rais achukue maamuzi mepesi ya kuwatimua wooote ambao hiyo karatasi iliyosainiwa ilipita mikononi mwao. Tukicheza kuna siku Rais atasainishwa karatasi ya kusema kwamba amejiuzulu bila yeye kujua!

wote waliohusika wawajibishwe ipasavyo
 
nina uhakika pinda atakua kachemka, peoples power imemchanganya huko musoma
 
Wazee wetu wa zamani walikuwa hawajasoma walibadilishana na wazungu almasi kwa ushanga, leo hii ****** kipindi cha wasomi anabadilishana na mzungu almasi kwa net.
Teh teh teh teh teh teh teeeh
 
ni matokeo ya kujaza mashositi nyumbanyeupe wanaamua kumpaka waone kama anaweze ku-react.
 
kumbe kama maneno gani vile?
...........Nimeangalia michango ya wanaJF waliochangia hii thread wamechoka na akili za raisi wao.Mimi sichangii maana nitasema maneno magumu halafu nipigwe ban.
 
yeye huangalia sehemu ya kusign tu
 
mwaka jana CCM ingeweza kumpitishia bwana shimbuda kuwa mgombeaji mbadala ya kikwetwe naamini isingefanya haya madudu machafu kabisa kama rijitu hiri kazi kuzurura rikiombaomba na kopo la matonya mkononi. hovyo kabisa
 
P.HD yake ya chuo cha kata UDOM. Hakuwa na waalimu, computer wala vitabu. hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
mwaka jana CCM ingeweza kumpitishia bwana shimbuda kuwa mgombeaji mbadala ya kikwetwe naamini isingefanya haya madudu machafu kabisa kama rijitu hiri kazi kuzurura rikiombaomba na kopo la matonya mkononi. hovyo kabisa

Hizo anazoomba zinafikia walengwa? ni watu wangapi walipata mabilioni ya JK?
 
Kama haya ni kweli, basi kuna mambo mawili makubwa: 1. Kuna watu wanatumia maamuzi ya Rais kwa manufaa yao au kundi fulani binafsi bila Rais mwenyewe kujua, kwa kutumia nafasi zao. kwa maana hiyo basi, inatuonyesha wazi kabisa jinsi watendaji wetu wakuu ndani ya Serikali walivyopoteza maadili na haiba ya kushika nafasi hizo walizo nazo, kwa mantiki hiyo, kuja haja ya kupitisha fagizi na la chuma na kuwatimua wote na kuunda kundi la wafanyakazi waadilifu na wazalendo kwa nchi hii. 2. Inashangaza sana na kusikitisha kama Rais anaweza kusign kitu bila kusoma. Moja kwa moja inatuonyesha OMBWE la uongozi wa juu; hivyo basi ni vyema kuachia ngazi na kufanya yale mtu atakayoweza kama ni uwaziri wa mambo ya nje, au ukatibu mkuu au ukuu wa mkoa. Lakini kwa nafasi ya Rais, inasikitisha haya kutokea, na kwa mantiki hiyo, maisha ya watanzania takribani millioni 46 yamewekwa rehani. Je tunakubali haya Watanzania?
 
Inasikitisha sana na wanamfedhehesha sana muheshimiwa rais hili halikubaliki kama malaria,kwann wanafanyia hivyo baba yake riziwan?na yeye kwann anaendelea kukumbatia watendaji wa namna hii,fukuza wote ikulu tena na bakora juu,haki za binadamu zije baada ya hukumu,huu ni upotoshaji wa hali ya juu na avumiliki labda kwa baba riziwan pekee
 
Tutaamini vipi kama kadanganywa? Mtu mzima mwenye akili timamu anaweza kweli kusaini tangazo la kuanzisha wilaya bila kusoma walau jina la wilaya inayoanzishwa? Mbona aliweza kugundua kuwa aliyekuja kuchukua zawadi ya gari la wagonjwa aliyoahidi kwa wilaya moja huko Arusha hakutoka wilaya iliyolengwa? Je haiwezekani kuwa kimsingi anataka makao makuu yawe Nyamisisi lakini alisema Butiama kwa sababu alitaka kuonekana kuwa anamuenzi "Mzee Nyerere"?
 
Hivi Pinda hajajifunza tu kutoka kwenye sakata la Jairo?
 
Waziri mkuu anajitahidi kutupoza na kudanganya umma kwani yeye tumeshuhudia akisema na utekelezaji wake ni kinyume na kauli zake. Hivi nani zaidi kikwete au pinda? Ebu fikiri yaliyojili bungeni kuhusu jairo, udom hadi leo ahadi zake hazijatekelezwa hivi ana nafasi gani? Mbona kauli zake zinanichanganya? Au kuna serikali ngapi? Huwa anadai atamshauri rais. Mbona huwa haleti majibu ya kukubaliwa ushauri wake au kukataliwa? Uwaziri mkuu wake na maamuzi yake na kauli zake huwa hamshirikishi jk? Iweje rais kasaini yeye apinge na kutoa kauli tofauti? Je, kipi chenye uzito maneno au maandishi?
 
Back
Top Bottom