Rais Kikwete adanganywa tena

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,080
  • Asaini tangazo la serikali lililochakachuliwa


RAIS Jakaya Kikwete amedanganywa tena na baadhi ya watendaji wake, akasaini tangazo lililochakachuliwa. Septemba 5 mwaka huu, Kikwete alisaini tangazo la kusudio la uanzishaji wa wilaya mpya ya Butiama, lakini katika namna ya kushangaza, sasa inaonekana eneo la wilaya mpya ni Nyamisisi.

Hali hiyo inayotia fedheha kwa Rais wa nchi, imebainika juzi wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofika Butiama kuzuru kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pinda alilazimika kuwatuliza wakazi wa eneo hili waliotaka kujua sababu za msingi za Rais kubadili msimamo wake na kuhamishia makao mapya yaliyotakiwa kuwa Butiama na kuyapeleka Nyamisisi.

Pinda alikiri bayana kuwa Rais alisaini tangazo hilo akijua kuwa kilichoandikwa ni makao makuu kuwa Butiama bila kujua eneo lililoandikwa ni Nyamisisi.

"Hata kama kuna mtu alitaka makao makuu yawe Nyamisisi, kwa kweli haikupaswa hiyo Nyamisisi kuchomekwa hivyo. Hata mngeniuliza mimi makao makuu yawe wapi, ningesema lazima yawe Butiama tu," alisema Pinda na kushangiliwa.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema tangazo hilo lilikuwa na makosa kutokana na kutaja eneo la makao makuu tofauti na lile lililopendekezwa.
Pinda alisema mpango wa serikali ulikuwa ni makao makuu ya wilaya hiyo yawe katika kijiji cha Butiama ili kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Akijibu malalamiko ya wakazi wa Butiama, walioingia katika eneo la nyumba hiyo, wakimtaka atamke kuwa makao makuu yatakuwa Butiama, Pinda alisema:

"Hili la Butiama kwa kweli linaleta manenomaneno. Sisi serikalini tulidhani ukiwa na wilaya ya Butiama na makao makuu ni lazima yawe Butiama, ili tumuenzi Baba wa Taifa.

Hata hivyo, alisema pamoja na tangazo hilo kuchomekwa neno Nyamisisi, bado mtu aliyefanya hivyo hajafanikiwa, kwani tangazo hilo sio uamuzi wa mwisho wa kuhusu suala hilo.

Aliwataka wananchi wa Butiama kulichukulia tangazo hilo kuwa ni pendekezo tu ambalo wanapaswa kulitolea maoni yao kuhusu kulikubali au kulikataa na kwamba maamuzi ya mwisho kuhusu wapi yawe makao makuu ya wilaya hiyo yatatokana na maoni ya wananchi wenyewe.

Alisisitiza kuwa Butiama ikiwa wilaya sio tu huduma za msingi zitaboreshwa na kuwapa watu sababu ya kwenda wilayani hapo, bali pia itawapa sababu ya kwenda kuzuru nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa.

Pinda pia alimpa fursa mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, kutoa kauli yake kuhusu suala hilo, ambaye alisema yeye asingependa kuliingilia suala hilo.
"Hili suala halina tatizo, ninyi na wananchi wote mtakavyoamua ndivyo iwe hivyohivyo," alisema Mama Maria.
 

Wed

JF-Expert Member
Mar 7, 2011
315
266
Kwa wale tunaoijua vizuri CCM hatushangai kwani huu ndio utendaji wao. Hata ukienda kule bungeni, hawa vilaza huithinisha miswada bila hata ya kuisoma. Kwani mikataba yote mibovu tuliyoingizwa na CCM ilitokeaje ? Jamaa wanatia tu saini hata bila kuisoma ..... na hapa JK ndio kinara wao kwani anachofikiria tu kichani ni jinsi ya kumzidi Vasco de Gama kwa safari za nje ya nchi !
 

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
7,763
7,183
Du kazi kweli kweli huyu jamaa anaweza hata kutuuza wazima wazima very interesting au ndo alikuwa anawahi safari ya USA!
 

ebrah

JF-Expert Member
Oct 9, 2010
397
50
jamani JK wa watu alikuwa amepewa asign wakati anapanga nguo za safari ya washington, si unajua tena mcheche!
"but in reality this man bana hayupo serious"
 

Didia

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
719
258
[Pinda alikiri bayana kuwa Rais alisaini tangazo hilo akijua kuwa kilichoandikwa ni makao makuu kuwa Butiama bila kujua eneo lililoandikwa ni Nyamisisi.

"Hata kama kuna mtu alitaka makao makuu yawe Nyamisisi, kwa kweli haikupaswa hiyo Nyamisisi kuchomekwa hivyo. Hata mngeniuliza mimi makao makuu yawe wapi, ningesema lazima yawe Butiama tu," alisema Pinda na kushangiliwa]


Serikali hii inashangaza sana. Hivi inakuwaje Rais anadanganywa marakwamara na bira aibu wanadhihirisha wazi upuuzi huo? Au ni kile kinachoitwa unafiki wa pinda na J.K kutopenda kuonekana wabaya kwa wananchi huku wasaidizi wao wakibeba lawama? Hivi inakuwaje RAIS ana anguka tu sahihi bila kusoma hata Kichwa cha Dokezo husika?

Kumbe kosa la Dkt wa Muhimbili kumpasua mtu kichwa badala ya mkuu ilikuwa ni picha tosha jinsi serikali inavyofanya kazi.
Ama kweli vitu vinavyokwamisha maendeleo ya nchi hii ni vingi mno
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
225
Hampendi Baba wa Taifa hayati Julius Nyerere -- mnakumbuka ile ishu ya chuo cha jeshi cha Monduli? Mmewahi kumsikia hata siku moja JK akimtaja Nyerere kama 'Baba wa Taifa'?
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
Haya kama ni kweli basi hayabebeki? Kwani Rais akipelekewa kitu kusaini si kunakuwa na watu weledi wamekisoma na kukipitia na kujiridhisha au hao hao ndio wachakachuaji? Kama ni kweli basi hapa nategemea Rais achukue maamuzi mepesi ya kuwatimua wooote ambao hiyo karatasi iliyosainiwa ilipita mikononi mwao. Tukicheza kuna siku Rais atasainishwa karatasi ya kusema kwamba amejiuzulu bila yeye kujua!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

6 Reactions
Reply
Top Bottom