Elections 2015 Rais Jakaya Kiwete ashitakiwa Mahakama ya Kimataifa ya ICC

gambalakobe

Member
Jul 1, 2015
55
125
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Anaandika Josephat Isango.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium Tower, wakili wa Chadema, John Mallya amesema Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.

Mallya alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia nakala za tuhuma dhidi ya Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika (AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue Uholanzi.

Kwa mujibu wa wakili huyo wa Chadema, barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah Safari.

Mashataka haya yanakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Rais Kikwete kuilamu Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC,

Hiyo ilikuwa ni siku tu moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, alikaririwa na vyombo vya habari vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo inatazama kwa umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Lowassa alilazimika kusema hayo katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Arusha na Mwanza, Lowassa akilitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.
 
STDVII

JF-Expert Member
Nov 24, 2014
1,585
1,500
Utatokwa povu sana. Safari hii jiandae kisaikolojia tu maana hamna namna nyingine isipokuwa ccm kuwa chama pinzani.

Mmezoea kuiba ndio maana mnasema hamna kulinda kura... Kura tutapiga na kuzilinda tutazilinda maana ni zetu

Kwa Hesabu gani? Wagombea Ubunge wenyewe wako 120 ukijitahidi utapata 25%
 
hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,318
2,000
Kuna siku niliandika uzi wa kuwalaumu viongozi wa ukawa na niliwaona ni kama viongozi walio lala
Lakini kwasasa nimewaona wameamka na wanakwenda vizuri na wametumia nafasi zao kama vile inavyo stahili kuwakomboa watanzania. kwahilo tunashukuru sana. najua ukawa inabahati sana ya kupendwa na watanzania tena bure na hii bahati naomba waitumie vizuri hata kama watatokea watu ambao wataendelea kukisaliti ukawa lakini atatokea shujaa mmoja au wawili wakuikomboa tanzania na sisi tukiwa nyuma yao na swala la ukombozi huwa halimuhusishi mtu mmoja tu hata wananchi nao inabidi wajitolee hata kulinda kura.
 
Lisa Rina

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
2,003
2,000
ICC sio solution ya matatizo ya ndani ya nchi, leo Kenya walichinjana baadae wakina Uhuru walipelekwa ICC lkn leo wamerudi wanaendelea na kazi. Vp wale waliokufa au kuumia kutokana na machafuko hayo nini wamepata au familia zao wamepata nini? Tambua nchi iliamua kujiunga kwa hiyari hivyo hivyo inaweza ikiamua kujitoa hakuna sehemu inaweza kulazimishwa mf. South Africa imeamua kujitoa pia Sudan, vp Omar Bashir sio tena Rais? Huyo anaendelea, Mallya usipotoshe watu wakapata madhara kwa kuwajengea kiburi wasiheshimu sheria za nchi husika.
Serikali inayo wajibu kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki pia Rais anaweza kutangaza hali ya hatari au kutoa amri itakayopelekea kurestore order, ndio maana vyombo vya ulinzi vina uwezo wa kutumia nguvu pale inapostahili. Acheni upotoshaji ICC haipo kwa ajili ya Watu walishindwa kufuata taratibu na sheria ya nchi husika. Haki yako ni kupiga kura kisha waachie mawakala na waangalizi wafanye kazi yao watakapomaliza matokeo yatabandikwa kituoni hivyo ni haki yako kuja kuyaona. Mipango yenu mibaya ambayo mnaipanga mkitaka kutumia "mob justice" kama cover ya kufanya uhalifu Serikali inaijua yote ndio maana imetoa agizo hilo ili wale wanaotaka kuleta fujo watambulike na wachukuliwe sheria stahiki. Hakuna haja ya kuwaletea wengine matatizo nenda mwenyewe ili ukileta fujo utambulike kweupe usipate utetezi kuwa ulifuata mkumbo.
Amani ya Tanzania kwanza, mengine baadae Mungu Ibariki Tanzania
Tanzania haina jeuri ya kujitoa coz wanajua kuna mirija kiana itazibwa na tunavopenda dezo...
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,310
2,000
Wameshajijuwa kuwa wameshindwa sasa wanatafuta huruma!

Hizzo mahakama na huko wanakopeleka malalamiko wana watu hapa hapaa nchini na wanaona ujinga wote unaofanywa na chadomo.

Kwanza inafaa washitakiwe wao kutuwekea mgomba urais ndondocha.
 
aretasludovick

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
6,357
2,000
Wameshajijuwa kuwa wameshindwa sasa wanatafuta huruma!

Hizzo mahakama na huko wanakopeleka malalamiko wana watu hapa hapaa nchini na wanaona ujinga wote unaofanywa na chadomo.

Kwanza inafaa washitakiwe wao kutuwekea mgomba urais ndondocha.
Mwaka huu itakuingia mpaka huko kunako :D na haya mabadiliko yatakubadilisha hadi tabia maana umezidi kuropoka kama nape, kikote na mkapa
 
monges

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
1,040
1,500
hapo kuna malalamiko yoyote. Hawa watu hawana mchezo watamwita uholanzi aanze kula kibano. hawatanii kabisa
Kinachofanyika ni urofa na upumbavu, chadema wanatumia mambo ya kitoto na wanakuwa kama hawakwenda shule, wenzetu wanajua kila kinacho endelea hapa nchini.
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
22,593
2,000
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium Tower, wakili wa Chadema, John Mallya amesema Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.
CHADEMA hawana wanasheria.Hicho walichopeleka ni malalamiko sio mashtaka.
 
GOD THE BOSS

Senior Member
Aug 4, 2015
145
170
nendeni huko icu lakini nchi yetu hatuwapi iwe nyinyi ama hao icu ...mmeshiñdwa kwenye kura sasa mnaanza kujitoa akiri, mnalo na kumbwela mbwela
ndio kawaida yako unafikiriaga kwa kutumia makalio j.pili ndio mwisho wenu fisiem na icc mtapelekwa wengi sn.
 
Bukama Batoko

JF-Expert Member
Apr 27, 2015
820
195
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Anaandika Josephat Isango.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium Tower, wakili wa Chadema, John Mallya amesema Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.

Mallya alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia nakala za tuhuma dhidi ya Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika (AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue Uholanzi.

Kwa mujibu wa wakili huyo wa Chadema, barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah Safari.

Mashataka haya yanakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Rais Kikwete kuilamu Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC,

Hiyo ilikuwa ni siku tu moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, alikaririwa na vyombo vya habari vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo inatazama kwa umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Lowassa alilazimika kusema hayo katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Arusha na Mwanza, Lowassa akilitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.

Ni mtu gani mwenye akili timamu asiyemjua J. Isango? Kazi yake ya msingi ni ipi? Muulizeni uchochezi kaacha lini? Je kiherere chake cha kutumia kalamu yake vibaya ni mara ya kwanza? Kwa sababu hajui yampasayo kutenda ila anaongozwa na jazba ambazo jibu lake ni kukurupuka. Muoneeni huruma J. Isango maana frastrutions zitammaliza. Hiyo ni mihemuko ya kauali ya mkosaji ili naye afurahishe genge. Watamuonaje mabwana zake kama anafanya kazi? Katumwa huyo kuharibu nchi yake.
 
gambalakobe,

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
13,672
2,000
ICC, fanyeni haraka plz...!!! Huyu ndio kinara wa wizi na kauli zake zitaleta vita Tanzania...!!! Aangaliwe kwa umakini mkubwa, sbb ANAITUMIA NEC na kufanya atakavyo, na wananchi hawamtaki, wala CCM hawaitaki kabisa..

So, ICC nyie kuleni sahani moja na mwenyekiti wa CCM, ndio huyo ataleta hatari sana, sbb naona anaiendesha NEC atakavyo, kama NEC ni CCM vile
 
mzee wa kismati

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
2,281
2,000
Kiongozi angekua kama Mbowe unachosema kingefanana, lakini CCM ni Waungwana umemuona JK anaaga kila mahali.

Lakini Chadema haiwezi kushinda Uchaguzi Kampeni zenyewe hovyo Kiongozi/Mgombea wenu hawezi kujieleza mpaka asemewe Wilaya na Majimbo mengi hajafika.

View attachment 300691

Pia kundi mlilolenga kuwapatia Kura ni walevi na hamjafanya Tafiti, huwezi kudai tu kwamba Vijana watawapigia Kura CDM, lazima uwachambue ni Vijana wa kundi gani miaka 18/25 au 25/35 au 35/45 ni kundi gani la Vijana.
35-45 sio vijana
 
Top Bottom