• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Elections 2015 Rais Jakaya Kiwete ashitakiwa Mahakama ya Kimataifa ya ICC

gambalakobe

gambalakobe

Member
Joined
Jul 1, 2015
Messages
55
Points
125
gambalakobe

gambalakobe

Member
Joined Jul 1, 2015
55 125
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Anaandika Josephat Isango.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium Tower, wakili wa Chadema, John Mallya amesema Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.

Mallya alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia nakala za tuhuma dhidi ya Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika (AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue Uholanzi.

Kwa mujibu wa wakili huyo wa Chadema, barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah Safari.

Mashataka haya yanakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Rais Kikwete kuilamu Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC,

Hiyo ilikuwa ni siku tu moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, alikaririwa na vyombo vya habari vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo inatazama kwa umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Lowassa alilazimika kusema hayo katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Arusha na Mwanza, Lowassa akilitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.
 
USSR

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Messages
1,722
Points
2,000
USSR

USSR

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2015
1,722 2,000
kwikwikwi isango na macho kumchuzi akili zake na mallya hazina ishu kwa icc itakuwa mavi tu
 
Rweye

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Messages
16,389
Points
2,000
Rweye

Rweye

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2011
16,389 2,000
Nendeni huko ICU lakini nchi yetu hatuwapi iwe nyinyi ama hao ICU ...mmeshiñdwa kwenye kura sasa mnaanza kujitoa akiri, mnalo na kumbwela mbwela
 
Msarendo

Msarendo

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2011
Messages
9,508
Points
2,000
Msarendo

Msarendo

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2011
9,508 2,000
Nendeni huko ICU lakini nchi yetu hatuwapi iwe nyinyi ama hao ICU ...mmeshiñdwa kwenye kura sasa mnaanza kujitoa akiri, mnalo na kumbwela mbwela
na we we tutakuunganisha
 
Junior Lecturer

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Messages
831
Points
500
Junior Lecturer

Junior Lecturer

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2013
831 500
Mnaichezea amani kwenye tundu la choo?
 
the boss13

the boss13

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Messages
413
Points
225
the boss13

the boss13

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2013
413 225
Good move itapunguza kiherehere chake manake likitokea la kutokea icc imuhusu yey kama rais tunajua ana chama so akiongea Kama rais usieke uchama chama
 
mkono wa nyoka

mkono wa nyoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2015
Messages
334
Points
195
mkono wa nyoka

mkono wa nyoka

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2015
334 195
thanks sana mahakama ya icc lazma utulivu uwepo nchin maana vurugu hatutaki
 
Y

YONGOMA

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2015
Messages
276
Points
170
Y

YONGOMA

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2015
276 170
"DUNIA NI MGHUA, UKIJA MWE TOGHA UTAJA MWE YEGHEA". Ngoja naye akafaidi maisha nyuma ya nondo!
 
N

nguvila

Senior Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
121
Points
195
N

nguvila

Senior Member
Joined Jul 30, 2015
121 195
Kwa mataifa ya nje wanaweza muona kikwete km kiongozi alieiongoza Tz kwa weledi mkubwa,lkn kw upande wa wananchi wngi wa Tz kikwete amekuwa mwiba unaowachoma ndg zake watz.

Yako mambo mengi maovu yaliyofanywa eidha kwa amri yake au watendaji wake aliowajaza jeuri ya kufanya maovu hayo.

Mf.ktk kipindi chake tu matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliongezeka Mara dufu hii ni kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu

1.watu kupigwa wakati wakidai haki zao,eidha kwa maandamano au ktk vymbo vya hbr
2.mauwaji ya vikongwe na albino na kikwete hakuwahi fanya juhudi zzte kuwanusuru wala kukamatwa kwa wahusika zaidi ya kubambikizia watu kesi

Yako mengi mnaweza endelea Kutaja na mengine.
 
ISLETS

ISLETS

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Messages
8,185
Points
2,000
ISLETS

ISLETS

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2012
8,185 2,000
watanzania wengi ni wajinga wa kutupa.... eti tunaanza kushtakiana nje ya nchi si ujinga kabisa huu... hata wao ICC wanatushangaa kwa kweli...

mfia maji haachi kutapatapa
 
C

ChiefmTz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2008
Messages
2,798
Points
2,000
C

ChiefmTz

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2008
2,798 2,000
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Anaandika Josephat Isango.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium Tower, wakili wa Chadema, John Mallya amesema Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.

Mallya alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia nakala za tuhuma dhidi ya Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika (AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue Uholanzi.

Kwa mujibu wa wakili huyo wa Chadema, barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah Safari.

Mashataka haya yanakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Rais Kikwete kuilamu Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC,

Hiyo ilikuwa ni siku tu moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, alikaririwa na vyombo vya habari vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo inatazama kwa umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Lowassa alilazimika kusema hayo katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Arusha na Mwanza, Lowassa akilitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.
Mmeshampiga chini Tundu Lisu? Tamko kama hilo lilipaswa kutolewa na Tundu Lisu. Je ndo kusema nafasi yake imechukuliwa na mwenzao na wenye Chama?
 
Forum statistics

Threads 1,404,953
Members 531,857
Posts 34,472,748
Top