Elections 2015 Rais Jakaya Kiwete ashitakiwa Mahakama ya Kimataifa ya ICC

gambalakobe

Member
Jul 1, 2015
55
125
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Anaandika Josephat Isango.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium Tower, wakili wa Chadema, John Mallya amesema Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.

Mallya alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia nakala za tuhuma dhidi ya Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika (AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue Uholanzi.

Kwa mujibu wa wakili huyo wa Chadema, barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah Safari.

Mashataka haya yanakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Rais Kikwete kuilamu Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC,

Hiyo ilikuwa ni siku tu moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, alikaririwa na vyombo vya habari vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo inatazama kwa umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Lowassa alilazimika kusema hayo katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Arusha na Mwanza, Lowassa akilitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.
 
Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,644
1,225
watanzania wengi ni wajinga wa kutupa.... eti tunaanza kushtakiana nje ya nchi si ujinga kabisa huu... hata wao ICC wanatushangaa kwa kweli...

mfia maji haachi kutapatapa
bila shaka mkate wako wa kila siku unatoka ccm
 
rpg

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
3,513
1,225
Wameshajijuwa kuwa wameshindwa sasa wanatafuta huruma!

Hizzo mahakama na huko wanakopeleka malalamiko wana watu hapa hapaa nchini na wanaona ujinga wote unaofanywa na chadomo.

Kwanza inafaa washitakiwe wao kutuwekea mgomba urais ndondocha.

Lazima tuwawekee speed governor, kwa sababu mnataka kuvitumia vibaya vyombo vya usalama ili kupata bao la mkono. Mara mita mia mbia hakuna, mara simu zisitumike. Safari hii bao la mkono hata mkipigia chooni tutawachungulia tu, sijui mtamalizia au ndo mtajaa aibu!
 
The Intelligent

JF-Expert Member
Dec 27, 2013
2,465
1,500
watanzania wengi ni wajinga wa kutupa.... eti tunaanza kushtakiana nje ya nchi si ujinga kabisa huu... hata wao ICC wanatushangaa kwa kweli...

mfia maji haachi kutapatapa
Wewe unaona ni wapi sehemu mahususi kupeleka malalamiko kama hayo?
 
ISLETS

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
8,178
2,000
Unataka tukashitaki wapi Kisutu?
hakuna kosa hapo sasa mnaenda kushtaki nini...

eti kauli za vitisho kawatishia nini...?

ukipiga kura rudi kwenu... usilete vurugu wala msongamano usio wa lazima kwenye vituo vya kura.
 
ISLETS

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
8,178
2,000
Acha watushangaee tu kwani sisi ni wakwanzaa?
Nyinyi muagize polisi watupige risasi halaf sis tunyamazee?? Hiyo ni akili kweli?
yani ukifanya fujo utapigwa tu hiyo haina mjadala... tii sheria uone kama kuna polisi atakufuata.
 
ISLETS

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
8,178
2,000
Wewe ulitaka wakamshtaki kwenye mahakama gani ikiwa mahakama ya nchi yao haina nguvu kikatiba ya kumuwajibisha?
mkuu kwanza hapo hakuna kosa ni porojo tu za kutafuta huruma ya umoja wa mataifa kwenye huu uchaguzi.
hakuna vitisho alivyotoa, wao wanataka ili ccm ikishinda ionekane imeshinda kibabe sio kwa haki...
hakuna mtu mwenye akili timamu atakayetilia maanani hayo mashtaka.
 
The Intelligent

JF-Expert Member
Dec 27, 2013
2,465
1,500
mkuu kwanza hapo hakuna kosa ni porojo tu za kutafuta huruma ya umoja wa mataifa kwenye huu uchaguzi.
hakuna vitisho alivyotoa, wao wanataka ili ccm ikishinda ionekane imeshinda kibabe sio kwa haki...
hakuna mtu mwenye akili timamu atakayetilia maanani hayo mashtaka.
Kama ni porojo itajulikana tu. Waliopeleka malalamiko hayo sio vichaa, ni watu wazima wenye akili zao timamu. Mambo mengine yanahitaji muda tu kuthibitisha ukweli wake.
 
Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,882
2,000
[h=2]Tuesday, October 20, 2015[/h]

Mpekuzi blog

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium Tower, wakili wa Chadema, John Mallya alisema Rais Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.

Mallya alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia nakala za tuhuma dhidi ya Rais Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika (AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue Uholanzi.

Kwa mujibu wa wakili huyo wa Chadema, barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Rais Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah Safari.

Mashataka haya yanakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Rais Kikwete ailaumu Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC,

Hiyo ilikuwa ni siku moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, alikaririwa na vyombo vya habari vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo inatazama kwa umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Lowassa alilazimika kusema hayo katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Arusha na Mwanza kwa kulitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.

Chanzo Mpekuzi blog 

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,854
2,000
Mtapigwa tu. kama mnakaidi kufanya mikusanyiko isiyo halali baada ya kupiga kura hakika kipigo kitakuwa miguuni mwenu. JK yupo sahihi.
 
washwa washwa

JF-Expert Member
Jul 21, 2012
1,619
2,000
Mtapigwa tu. kama mnakaidi kufanya mikusanyiko isiyo halali baada ya kupiga kura hakika kipigo kitakuwa miguuni mwenu. JK yupo sahihi.
Naona na wewe utamsindikiza the Hague kwa kuwa hata Kenya kuna watangazaji wa redio walishtakiwa ICC kwa uchochezi
 
mjapan

Member
Oct 16, 2015
84
95
Mwenzenu Waziri Mkuu Pinda jana aliomba msamaha kupitia kanisa kwa kauli za wapigwe tu. Sasa ni The Haigh tu mkakutane na Fatu Bensouda baada ya hukumu Charles Taylor
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
28,235
2,000
CHADEMA wanazidi kuwa mabwege, hivi wanajua maana ya uhalifu wa kivita? Vita ipi hiyo?
Hapa ni eidha mleta mada umekurupuka kwa kutokuwaelewa wamesema nini au hao wanasheria wamekurupuka.
 
MADAM T

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
4,356
2,000
watanzania wengi ni wajinga wa kutupa.... eti tunaanza kushtakiana nje ya nchi si ujinga kabisa huu... hata wao ICC wanatushangaa kwa kweli...

mfia maji haachi kutapatapa
Wanakushangaa wewe!
 
luckyline

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
11,116
2,000
Kwikwikwikwikwikwi kweli akili hamna,,sasa hapa mmeshitaki au mmepeleka umbeya?? Mbona mnachuki sana na JK, amewafanya nini mkwere wa watu mbona yupo poa tu,, ikulu hii mbona mnaitafuta kwa nguvu sana wajameni??? Ikulu hatuendi kwa nguvu hiyo???
elimu ndogo na ujinga ulonao ndo unakusumbua pole mzazi wako kupoteza ada yake
 
Top Bottom