Rais Jakaya Kiwete ashitakiwa Mahakama ya Kimataifa ya ICC

gambalakobe

gambalakobe

Member
Joined
Jul 1, 2015
Messages
55
Points
125
gambalakobe

gambalakobe

Member
Joined Jul 1, 2015
55 125
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemshitaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete. Anaandika Josephat Isango.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana ukumbi wa Kisenga uliopo Millenium Tower, wakili wa Chadema, John Mallya amesema Kikwete ameshitakiwa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mahakama ya kihalifu Uholanzi kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya kutisha wananchi kuelekea uchaguzi mkuu.

Mallya alisema kuwa Mashitaka hayo yameelekezwa Umoja wa Mataifa lakini pia nakala za tuhuma dhidi ya Kikwete zimepelekwa pia Umoja wa Afrika (AU) na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo The Hegue Uholanzi.

Kwa mujibu wa wakili huyo wa Chadema, barua hiyo ya tuhuma dhidi ya Kikwete imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Abdallah Safari.

Mashataka haya yanakuja ikiwa ni miezi miwili tangu Rais Kikwete kuilamu Mahakama hiyo ya kihalifu kwa kusema kuwa viongozi wa Afrika hawafurahii kwa namna ambavyo mahakama hiyo inavyofanya kazi zake kwa kuwashughulikia zaidi viongozi wa mataifa ya Afrika.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa 16 wa Umoja wa Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini mwa Afrika-SADC,

Hiyo ilikuwa ni siku tu moja baada ya ICC kueleza kwamba inafuatilia mwenendo wa uchaguzi nchini Tanzania.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, alikaririwa na vyombo vya habari vya Aljazeera na Gambia Today akisema kuwa Mahakama hiyo inatazama kwa umakini mkubwa yanayotokea Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu kama ilivyofanya katika nchi za Kenya, Ivory Coast na Congo na kwamba itachukua hatua za haraka kama kutakuwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Kauli hiyo ya Bensouda ilitanguliwa na ile iliyotolewa na mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

Lowassa alilazimika kusema hayo katika ziara ya kutafuta wadhamini katika mikoa ya Arusha na Mwanza, Lowassa akilitahadharisha Jeshi la Polisi juu ya uwepo wa Mahakama ya ICC kutokana na kitendo chake cha kutumia nguvu dhidi ya wapinzani kwa kuupiga mabomu msafara wake.
 
Superbrand

Superbrand

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2013
Messages
508
Points
225
Superbrand

Superbrand

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2013
508 225
Ndo maana Mh mbowe kwenye mkutano alisema hawana akili
 
luckyline

luckyline

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2014
Messages
10,261
Points
2,000
luckyline

luckyline

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2014
10,261 2,000
Umekosa cha kuandika
Rudi shulen mwalim wako wa uraia akakufundishe kazi kubwa moja ya mahakama ya ICC
Usidanganye watu
tukwambie kwamba rais wa nchi hii hana kashfa hata moja ya uhalifu wa kivita.
unajua maana ya neno uchochezi? Acha kukurupuka dogo
 
njiwa

njiwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2009
Messages
11,718
Points
2,000
njiwa

njiwa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2009
11,718 2,000
Hahahaha.. Yaani kuna watu wanachekesha hata huko icc watawashangaa
 
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2012
Messages
3,812
Points
1,225
Dr.Mo

Dr.Mo

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2012
3,812 1,225
Kinachofanyika ni urofa na upumbavu, chadema wanatumia mambo ya kitoto na wanakuwa kama hawakwenda shule, wenzetu wanajua kila kinacho endelea hapa nchini.
Upo mzima kweli.? Umeandika nini hapa.?!
 
Alure

Alure

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2014
Messages
1,107
Points
2,000
Alure

Alure

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2014
1,107 2,000
Ashitakiwe tu maana hamna namna, huyu jamaa anataka kutuletea machafuko kwenye nchi yetu
Tena yakitokea machafuko afungwe maana maneno yake yatakuwa ni chachu ya machafuko
 

Forum statistics

Threads 1,304,903
Members 501,587
Posts 31,531,248
Top