Rais hapaswi kufanya kazi za kawaida za Rais akiwa nje ya nchi

Nimeona Chifu Hangaya (akiwa Glasgow, Scotland) amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NDC. Huu ni ukiukaji wa Katiba yetu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 47(1)(c) ya Katiba yetu, Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Na kwa mujibu wa Ibara ya 37(6)(b) ya Katiba hiyo hiyo, ili Rais ahesabike kuwa yuko nje ya nchi, lazima awe nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne.

Ingawa Ofisi ya Rais wa JMT yaweza kuwa mahali popote ndani ya mipaka ya JMT, katu haiwezi kuwa mahali popote tu duniani, kama Chifu Hangaya anavyotaka kuifanya. Ni lazima iwe ndani ya mipaka ya nchi yetu.

Vilevile, nchi haiwezi kuwa na Rais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Rais awapo nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne, Makamu wa Rais (au Waziri Mkuu, endapo Makamu wa Rais naye hayupo) ndiye Rais wa nchi kwa kipindi hicho (Kaimu Rais)! Periolakini
Unachotakiwa kujua, Rais anapoondoka nchini anamkaimisha VP, kwa maandishi na kuelekeza majukumu atakayoruhusiwa kuyafanya, Majukumu mengine hataruhusiwa kama Teuzi, utenguzi wa teuzi, uamirijeshi mkuu haukaimishwi na mambo mengine.hiyo ndiyo interpretation soma vizuri ibara ya 37(6) ya katiba
 
Soma vizuri Katiba. Kaimu Rais (au Kaimu yeyote yule) hawezi KUTENDA kitu kipya, hawezi kuteua hawezi kufukuza. Labda hiyo katiba mpya yenu iseme hivyo, Rais Tundu Lissu akiwa Belgium Kaimu Rais wake Peter Msifwa amteue Professor Assad awe Mkurugenz i wa NDC?

Nani amekuambia tunataka Kaimu Rais ateue au afukuze mtu?
 
Unachotakiwa kujua, Rais anapoondoka nchini anamkaimisha VP, kwa maandishi na kuelekeza majukumu atakayoruhusiwa kuyafanya, Majukumu mengine hataruhusiwa kama Teuzi, utenguzi wa teuzi, uamirijeshi mkuu haukaimishwi na mambo mengine.hiyo ndiyo interpretation soma vizuri ibara ya 37(6) ya katiba

Umeelewa kitu tunachokipinga?
 
Kaka,

Hili jambo ni zito tunahitaji msaada wa wazo la kila mtu. Hukusoma hoja ya mleta mada.

Mleta mada kajikita kwenye ibara ya 47 (1)(c) inayosema Rais akiwa hayupo ofsini Makamu anafsnya KAZI ZOTE ZA URAIS.

Wewe hujikiti na ibara hiyo unaleta masuaka ya barua ya kukaimisha ambayo huna uhakika kama kweli imeandika.

Hata ingeandikwa bado barua ya kukaimisha haizidi ibara hii ya 47 (1)(c) inayompa Philip Mpango urais wote yakishazidi masaa 24 Rais akiwa nje ya nchi.

Jikite kwenye ibara hii 47 (1)(c) aliyoiibua mtoa mada.

Kama sikosei Rais Nelson Mandela akiwa ziarani India aliwahi kufanya kosa la kumfuta uwaziri Winnie Mandela.

Ikaja kuonekana alifanya makosa aktungea amri ya kumfuta. Alivyorudi toka ziarani sasa akamfuta uwaziri hivyo Winnie Mandela akaacha kuwa waziri.

Labda tukuwekee hiyo ibara ya 47 (1)(c) uone inavyosema, inasema hivi,

"Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwandiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan-
atafanya KAZI ZOTE za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi."

Unachotakiwa kujua, Rais anapoondoka nchini anamkaimisha VP, kwa maandishi na kuelekeza majukumu atakayoruhusiwa kuyafanya, Majukumu mengine hataruhusiwa kama Teuzi, utenguzi wa teuzi, uamirijeshi mkuu haukaimishwi na mambo mengine.hiyo ndiyo interpretation soma vizuri ibara ya 37(6) ya katiba
 
Hawezi kuelewa.

Asome na hii ili aelewe,

Umeelewa kitu tunachokipinga?
 
Nimeona Chifu Hangaya (akiwa Glasgow, Scotland) amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NDC. Huu ni ukiukaji wa Katiba yetu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 47(1)(c) ya Katiba yetu, Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Na kwa mujibu wa Ibara ya 37(6)(b) ya Katiba hiyo hiyo, ili Rais ahesabike kuwa yuko nje ya nchi, lazima awe nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne.

Ingawa Ofisi ya Rais wa JMT yaweza kuwa mahali popote ndani ya mipaka ya JMT, katu haiwezi kuwa mahali popote tu duniani, kama Chifu Hangaya anavyotaka kuifanya. Ni lazima iwe ndani ya mipaka ya nchi yetu.

Vilevile, nchi haiwezi kuwa na Rais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Rais awapo nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne, Makamu wa Rais (au Waziri Mkuu, endapo Makamu wa Rais naye hayupo) ndiye Rais wa nchi kwa kipindi hicho (Kaimu Rais)! Period.
Hivi Rais akiwa hayupo na Makamo akawa anafanya kazi za Urais, je Makamo anaweza kufanya uteuzi? Je Makamo anaweza kusaini hati ya kunyonga wafungwa waliohukumiwa kunyongwa? Je Makamo anaweza kutengua uteuzi?
 
Mwambieni Hangaya atulie nchini,hizi safari za kuzungumzia tabia nchi awaachie mataifa makubwa.
Kati ya matatizo lukuki ya nchi hilo wala halitusumbui
PS; Dar es Salam kuna mgao wa maji huku tunaambiwa tunawe na maji tiririka
Hangaya kaenda kule kuomba hela za wala rushwa, wala hakuna cha maana
 
Jibu ni NDIYO yaani sasa hivi Philip Mpango yaani makamu wa rais anaweza kufanya uteuzi, kutengua uteuzi, kusaini hati ya kunyonga na chochote anachofanya Rais Samia.

Isome vizuri ibara ya 47(1)(c) inayosema makamu anafanya KAZI ZOTE ZA URAIS na kwa kukurahisishia nimeinukuu hapa, inasema hivi,

"Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa
ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi."

Hivi Rais akiwa hayupo na Makamo akawa anafanya kazi za Urais, je Makamo anaweza kufanya uteuzi? Je Makamo anaweza kusaini hati ya kunyonga wafungwa waliohukumiwa kunyongwa? Je Makamo anaweza kutengua uteuzi?
 
Umesema mambo yafuatayo:-

1. Taifa haliwezi kuwa na maRais wawili kwa wakati mmoja.

2. Majukumu "yote" ya Urais yatafanywa na Makamu wa Rais endapo Rais atakua nje ya nchi kwa zaidi ya saa 24.

Kwa maelezo yako hayo hapo juu, maana yake kwa sasa Rais wa Tanzania ni Dr. Mpango (maana Mh. Samia hayupo nchini kwa zaidi ya saa 24).
Je, Mh. Samia yuko kule kama nani ? Jibu lako likiwa yupo kule kama Rais wa Tanzania, swali linalofuata ni je, kwa sasa Tanzania ina maRais wawili ?
Akijibu swali hili (Namba 1) Nenda kwa mganga. Swali hili halijibiki hata siku moja, ni mzigo wa misumari ndani ya gunia. Sana sana utaambulia matusi tu hapa.

Tatizo kajichanganya yeye mwenyewe, maana anasema: "Vilevile, nchi haiwezi kuwa na Rais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Rais awapo nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne, Makamu wa Rais (au Waziri Mkuu, endapo Makamu wa Rais naye hayupo) ndiye Rais wa nchi kwa kipindi hicho (Kaimu Rais)! Period." Piga ua, Kaimu Rais hawezi kuwa Rais, Kaimu mkurugenzi hawezi kuwa Mkurugenzi, Kaimu mwenye kiti hawezi kuwa mwenye kiti n.k. Siku zote hawa wahusika wataitwa vyeo vyao kwa kuanzia na NENO KAIMU.... hawezi kuwa Rais- bado atakuwa Makamu Rais

Hata siku moja ukawa na shida yako na Rais au mkurugenzi hayupo na kiti kikakaliwa na KAIMU.... Usikubali kusainiwa na Kaimu na akaandika cheo chake kama Rais au Mkurugenzi. Saini hiyo itakuwa batili/si halali. Lugha ya Taifa iko fasaha na wazi kabisa.
 
Hivi Rais akiwa hayupo na Makamo akawa anafanya kazi za Urais, je Makamo anaweza kufanya uteuzi? Je Makamo anaweza kusaini hati ya kunyonga wafungwa waliohukumiwa kunyongwa? Je Makamo anaweza kutengua uteuzi?
Jumbe aliweka watu kizuizini wakati Nyerere akiwa nje ya nchi, na watu wale wakaendelea kubaki kizuizini hata baada ya Nyerere kurudi!
 
Jibu ni NDIYO yaani sasa hivi Philip Mpango yaani makamu wa rais anaweza kufanya uteuzi, kutengua uteuzi, kusaini hati ya kunyonga na chochote anachofanya Rais Samia.

Isome vizuri ibara ya 47(1)(c) inayosema makamu anafanya KAZI ZOTE ZA URAIS na kwa kukurahisishia nimeinukuu hapa, inasema hivi,

"Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa
ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi."
Kuachiwa huko kumewekewa mipaka mzee vinginevyo Makamo anaweza kuchukua madaraka na Rais akakosa pa kwenda. Mipaka ipo na hawezi kufanya hayo!
 
Nimeona Chifu Hangaya (akiwa Glasgow, Scotland) amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NDC. Huu ni ukiukaji wa Katiba yetu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 47(1)(c) ya Katiba yetu, Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Na kwa mujibu wa Ibara ya 37(6)(b) ya Katiba hiyo hiyo, ili Rais ahesabike kuwa yuko nje ya nchi, lazima awe nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne.

Ingawa Ofisi ya Rais wa JMT yaweza kuwa mahali popote ndani ya mipaka ya JMT, katu haiwezi kuwa mahali popote tu duniani, kama Chifu Hangaya anavyotaka kuifanya. Ni lazima iwe ndani ya mipaka ya nchi yetu.

Vilevile, nchi haiwezi kuwa na Rais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Rais awapo nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne, Makamu wa Rais (au Waziri Mkuu, endapo Makamu wa Rais naye hayupo) ndiye Rais wa nchi kwa kipindi hicho (Kaimu Rais)! Period.
yeye anaona kafanya bonge la ubunifu.
 
Kaka Kichuguu, shikamoo,
Jumbe alikuwa sahihi japokuwa muhuri wa Rais hakuweka kwenye hiyo detention order.

Wale jamaa walipoenda mahakamani walishinda kwa kigezo kwamba detention order haikuwa na muhuri wa rais.

Inasemekana Nyerere alikuwa nasasfiri nao huo muhuri japo sina hakika na hilo.

All in all, ibara ya msingi hapa ni ile ya 47 (1)(c) ya katiba yetu ambayo Joseph Magata kwenye RAIA MWEMA aliitafsiri vizuri kama inavyoonekana article yake isome hapa

Jumbe aliweka watu kizuizini wakati Nyerere akiwa nje ya nchi, na watu wale wakaendelea kubaki kizuizini hata baada ya Nyerere kurudi!
 
Hakuna mipaka, ibara ya 47(1)(c) ya katiba iko wazi inasema Rais akisafiri nje ya nchi Makamu atafanya KAZI ZOTE za urais.

Soma makala hii ilifafanua

Kuachiwa huko kumewekewa mipaka mzee vinginevyo Makamo anaweza kuchukua madaraka na Rais akakosa pa kwenda. Mipaka ipo na hawezi kufanya hayo!
 
Mwambieni Hangaya atulie nchini,hizi safari za kuzungumzia tabia nchi awaachie mataifa makubwa.
Kati ya matatizo lukuki ya nchi hilo wala halitusumbui
PS; Dar es Salam kuna mgao wa maji huku tunaambiwa tunawe na maji tiririka
Mkuu swala la maji Basi limekua sugu Dodoma jiji Hali ya maji ni mbaya
 
Nimeona Chifu Hangaya (akiwa Glasgow, Scotland) amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NDC. Huu ni ukiukaji wa Katiba yetu.

Kwa mujibu wa Ibara ya 47(1)(c) ya Katiba yetu, Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Na kwa mujibu wa Ibara ya 37(6)(b) ya Katiba hiyo hiyo, ili Rais ahesabike kuwa yuko nje ya nchi, lazima awe nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne.

Ingawa Ofisi ya Rais wa JMT yaweza kuwa mahali popote ndani ya mipaka ya JMT, katu haiwezi kuwa mahali popote tu duniani, kama Chifu Hangaya anavyotaka kuifanya. Ni lazima iwe ndani ya mipaka ya nchi yetu.

Vilevile, nchi haiwezi kuwa na Rais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Rais awapo nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne, Makamu wa Rais (au Waziri Mkuu, endapo Makamu wa Rais naye hayupo) ndiye Rais wa nchi kwa kipindi hicho (Kaimu Rais)! Period.
Waziri mkuu hawezi kukaimu urais. Mlolongo ni rais, makamu wa rais, spika na jaji mkuu.
 
Ukikuta kikundi Cha watu 10 waulize ,Tania nchi Ni nini?
Hutapatata jibu wengi watakuwa wanafikili labda Serikali imewaletea mbegu mpya za korosho, Tumbaku ,Alizeti,pamba au Aina mpya ya bodaboda au bajaji.

Sisi tupambane na vyumba vya madalasa,vyoo umeme na maji,Tania nchi haituhusu zaidi ya Nchi zenye viwanda.
ndg ! Htr ukame Kenya na hata sisi mabadiliko ni makubwa
 
Back
Top Bottom