Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,398
- 2,990
Nimeona Chifu Hangaya (akiwa Glasgow, Scotland) amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NDC. Huu ni ukiukaji wa Katiba yetu.
Kwa mujibu wa Ibara ya 47(1)(c) ya Katiba yetu, Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi. Na kwa mujibu wa Ibara ya 37(6)(b) ya Katiba hiyo hiyo, ili Rais ahesabike kuwa yuko nje ya nchi, lazima awe nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne.
Ingawa Ofisi ya Rais wa JMT yaweza kuwa mahali popote ndani ya mipaka ya JMT, katu haiwezi kuwa mahali popote tu duniani, kama Chifu Hangaya anavyotaka kuifanya. Ni lazima iwe ndani ya mipaka ya nchi yetu.
Vilevile, nchi haiwezi kuwa na Rais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Rais awapo nje ya nchi kwa muda unaozidi saa ishirini na nne, Makamu wa Rais (au Waziri Mkuu, endapo Makamu wa Rais naye hayupo) ndiye Rais wa nchi kwa kipindi hicho (Kaimu Rais)! Period.