Rais hajui kuzungumza na wananchi, ziara za njiani zisitishwe

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Naongea ukweli kutoka moyoni CCM mtanisamehe, Rais wetu hajui kuzungumza na raia barabarani, ni vyema ziara ya njiani zikanseliwe.

Rais hatatui changamoto unasimama njiani unaanza kuwaambia kurekodi filamu na tozo hiyo haisadii, wala sisi hatukusimamishi ili utwambie mambo ya filamu, sisi tunakusimamisha kukueleza kero na shida zetu tulizonazo eneo husika.

Ukisimama njiani tafadhali uliza wananchi wa pale wana shida gani, muite mkuu wa mkoa aeleze ataitatua lini au kwanini kashindwa kuitatua hilo ndio lengo la wananchi kusimama njiani,

Wananchi wanachangamoto sugu ambazo wakuu wa mikoa hawajawai kufanyia ziara, masoko yana shida, ushuru usio na tija, Rais simama omba hata Raia mmoja aelezee matatizo ya pale, muite mkuu wa mkoa umuhoji, Mweshmiwa Rais labda kwa taarifa tu ni kwamba hao wakuu wa mikoa hawafanyagi ziara wananchi hawajui wapate wapi msaada.

Nimeona leo hata pale Kwenye maonyesho wamekuomba ujenzi wa lami ya kilomita moja toka uwanjani hadi makumbusho ya bujora lakini hukuwajibu kitu.

siku nyingine tutakua hatuji maana kero zetu wakuu wa wilaya zimewashinda, mkuu wa mkoa kashindwa hata wewe Rais tunayekutegemea husemi chochote si bora vyavziara uviache tu tujikalie majumbani kwetu,

Naomba ziara za njiani zife ni kupotezea muda wananchi tu

Kama haiwezekani kusikiliza kero za wananchi eneo husika usiwe unasimama barabarani, kuumishana njaa tu
 
Atasema anayo staili yake ya uongozi hawezi kumuiga JPM Hayati. Ukiwauliza wananchi shida zao nyingine zitakuhitaji uchukue maanuzi ya papo kwa papo kama kumtumbua muhusika. Je anahuo uthubutu wa kufanya hivyo? Alishasema uongozi wake si wa kutumia miguvu! Tumsaidie kwa kuendelea kumuweka kwenye maombi Mh Rais.
 
Atasame anayo staili yake ya uongozi hawezi kumuiga JPM Hayati. Ukiwauliza wananchi shida zao nyingine zitakuhitaji uchukue maanuzi ya papo kwa papo kama kumtumbua muhusika. Je anauo uthubutu wa kufanya hivyo? Alishasema uongozi wake si wa kutumia maguvu! Tumsaidie kwa kuendelea kumuweka kwenye maombi Mh Rais.
basi haina haja ya ziara za njiani, kama Rais anaogopa kumtumbua mtu asiewajibika sasa anamsaada gani kwa nchi
 
basi haina haja ya ziara za njiani, kama Rais anaogopa kumtumbua mtu asiewajibika sasa anamsaada gani kwa nchi

Anapromote utalii kupitia royal tour na kuwakinga wananchi na vifo vya corona kupitia uhamasishaji wa chanjo na kuvaa barakoa. Nikumbushe majina ya Mawaziri wa utalli JMT na SMZ tafadhali.
 
Anafanya anayoyaweza tu ndugu yangu, hayo hawezi. Hata mimi niliwaza sana tangu aanze hiyo simama simama nikaona sioni jipya, hata yule makamu wake naye anajaribu bado anafeli anawaambia hiyo ni yako mkuu wa mkoa utashughulikia. Angalau waziri mkuu akisimama unaona kabisa anatembea kwenye hisia za wananchi ndio maana tunampenda.

Hao wengine wanapoteza muda bora wasingekuwa wanasimama. Waziri mkuu akisimama mahali unaona kabisa anafanya jambo la uhakika na anaondoka eneo hilo. Hao wengine hawajui kucheza mziki wa wananchi kwakweli
 
Tatizo mlizoeshwa tabia chafu na ya kishenzi kufokeana hadharani kama watoto wadogo na mliipenda tabia hiyo kwa sababu ujinga tu.
Mkuu kufokeana hadharani ni kweli sio sawa. Ila hawa wasaidizi wa raisi hamna kitu wanaweza kukusaidia amini Hilo.

Ukiwa na tatizo usiombe uende kwa mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa, utazungushwa hadi utakoma mwenyewe.

Ila Raisi ni mtu ambae wengi huwa wana Imani nae.

Pia hata hii njia ya kubembeleza nao pia ni mbaya, sisi waswahili kuna muda hatuhitaji kabisa kubembelezwa hasa kwenye kutekeleza wajibu wetu.

Onaa mfano Mkurugenzi kaiba mabati, alafu utegemee mkurugenzi huyohuyo atatue kero yako
 
Mkuu kufokeana hadharani ni kweli sio sawa. Ila hawa wasaidizi wa raisi hamna kitu wanaweza kukusaidia amini Hilo.

Ukiwa na tatizo usiombe uende kwa mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa, utazungushwa hadi utakoma mwenyewe.

Ila Raisi ni mtu ambae wengi huwa wana Imani nae.

Pia hata hii njia ya kubembeleza nao pia ni mbaya, sisi waswahili kuna muda hatuhitaji kabisa kubembelezwa hasa kwenye kutekeleza wajibu wetu.

Onaa mfano Mkurugenzi kaiba mabati, alafu utegemee mkurugenzi huyohuyo atatue kero yako
Uko sahihi 200%
 
Back
Top Bottom