Mlowo, Songwe: Makonda akataa kutumia jukwaa aliloandaliwa, ashuka haraka na kutumia gari lake kuzungumza na wananchi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu Watanzania,

Leo hii Mheshimiwa Paul Christian Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa ameacha gumzo mkoani Songwe katika wilaya ya Mbozi, mji mdogo wa Mlowo alipokuwa ameandaliwa jukwaa zuri na kubwa sana kwa ajili ya kufanya mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi kama ilivyo utamaduni wake.

Lakini kuna jambo ambalo limetokea ambalo kila mtu amebaki mdomo wazi na mwaswali kibao. Ilikuwa hivi baada ya Mheshimiwa kufika kulifanyika utaratibu wa haraka haraka wa utambulisho wa viongozi mbalimbali, ambapo baadaye aliitwa mbunge wa jimbo la Mbozi Mheshimiwa George Rainwell Mwenisongole halafu baadaye katibu wa mkoa akamkaribisha mwenyekiti wa CCM mkoa ili amkaribishe Mheshimiwa Makonda kuzungumza.

Lakini ghafla Mheshimiwa Makonda alitoka pale jukwaani kikomandoo bila watu wengi kujua japo mimi nilimuona akiwa yupo penye ngazi akishuka jukwaani na wasaidizi wake na mmoja akiwa ameshika maiki na kwenda kupanda kwenye gari iliyokuwa barabarani imepaki na kutokeza kichwa kwa juu kuwasalimu na kuanza kuzungumza na wananchi.

Kwanza watu walipigwa na butwaa kubwa sana, kwasababu anaposhuka jukwaani wengi hawakumuona na macho yao yalikuwa yameelekezwa eneo la jukwaani kwa mbele mahali ambapo ndipo ilitakiwa aende pale kwa ajili ya kuanza kutolea hotuba yake. Kiukweli watu wakapigwa na mshangao kuona sauti ikitokea nyuma yao juu ya gari akiwa kasimama kikomandoo na kwa ujasiri mkubwa sana.

Ambapo ameunguruma hapo kwa kishindo kikubwa sana kama Simba. Kiukweli ameacha gumzo katika wilaya ya mbozi. Mheshimiwa makonda anaijuwa siasa ni hakuna mfano.mheshimiwa anajuwa nini watanzania wanahitaji, anajuwa machungu wayapitiayo Watanzania na amejitoa na kujitolea kwelikweli kuwatumikia watanzania.

Kwa sasa yupo ndani ya mkoa wa Mbeya. Nitaendelea kuwaleteeni kila kinachojili katika mikutano yake Mheshimiwa Makonda ambaye ameteka hisia za watanzania na kugusa mioyo ya watanzania wanyonge. Mheshimiwa Makonda siyo mtu wa kawaida.

Ni mtu na nusu, ni Jabali wa siasa, ni kete ambayo Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan aliicheza kwa ustadi wa hali ya juu sana na ambayo imeleta matunda na matokeo chanya.

Meneja wa TANROADS mkoa wa Songwe amehenyeshwa kwa maswali ni hakuna mfano,amepigwa maswali mpaka jasho likamtoka na kubidi naibu waziri ujenzi kuja kutoa majibu.

Mkuu wa wilaya naye kaambiwa abaki pale pale kusikiliza kero za wananchi maana awali alisema wilaya ni shwari halafu baadaye ikaonekana kuna changamoto za watu waliokuja na mabango yenye kero mbalimbali, japo sijajua kama watu hao wamewahi kufika kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mbozi kupeleka kero zao,maana nimesikia mkuu wa wilaya akilalamika kuwa wengine wamefika na mabango yao lakini hawaijui wala hawajawahi kufika ofisi ya DC.

Ziara za Mheshimiwa Makonda zitawaondoa wengi sana kwenye nafasi zao, kutokana na kero nyingi anazokutana nazo huko apitako,zinazoonyesha kuwa wananchi wanakero ambazo wameshindwa kupatiwa majibu au kusaidiwa na viongozi walioko huko.

Ila mkuu wa wilaya ya Mbozi anajitahidi kufanya kazi na amekuwa akijitahidi sana kuwa karibu na wananchi na kusikiliza kero zao.amekuwa akikaa na kuzungumza na makundi mbalimbali na kutoa Elimu wa masuala mbalimbali pamoja na kusikiliza kero.hata kwa wananchi anajitahidi kufika ,hata kwenye michezo anashiriki vizuri tu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

IMG-20240201-WA0003.jpg
IMG-20240206-WA0027.jpg
 
Tuambie kwanini Makonda amekimbia jukwaani akaenda kuhutubia kwenye gari?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Mleta mada mjinga habari sensitive kama hiyo hakutakiwa kuleta humu ana agenda Gani angenyamaza Kuna shida Gani? Makonda aweza hutubia popote jukwaani,chini ardhini au kwenye gari

Mwashambwa Mleta mada Kwa hiyo umeleta humu ili iweje ? Lengo lako Nini?
 
Mleta mada mjinga habari sensitive kama hiyo hakutakiwa kuleta humu ana agenda Gani angenyamaza Kuna shida Gani? Makonda aweza hutubia popote jukwaani,chini ardhini au kwenye gari

Mwashambwa Mleta mada Kwa hiyo umeleta humu ili iweje ? Lengo lako Nini?
Yaani huyu dada anavyojigonga kwa Makonda sijui anafikiria atamuacha mkewe ili amuwowe yeye.
 
Mleta mada mjinga habari sensitive kama hiyo hakutakiwa kuleta humu ana agenda Gani angenyamaza Kuna shida Gani? Makonda aweza hutubia popote jukwaani,chini ardhini au kwenye gari

Mwashambwa Mleta mada Kwa hiyo umeleta humu ili iweje ? Lengo lako Nini?
Acha matusi kwani mkutano ya Mheshimiwa Makonda inafanyika gizani au hadharani? Kwamba kwa akili yako hiyo hiyo unafirikiri watu waliopo humu jukwaani wanatokea wapi? Si ndio hawa hawa waliopo mitaani na wanaohudhuria kwenye mikutano na matukio mbalimbali na kutuhabarisha kinachokuwa kinatokea?

Hujuwi ziara zake zinaambatana hata na waandishi wa habari ambao wanachukua matukio yote ,lakini pia hata wananchi wenyewe nao wananchukua matukio kupitia simu zao? Kwa akili yao ukizima na kusimamisha saa yako kwamba unafirikiri kuwa na kwa wengine saa zao zimesimama?
 
Back
Top Bottom