Paul Makonda awataka Viongozi wanaosubiri ziara ya Rais ndio watatue matatizo ya wananchi wajitafakari kama wanapaswa kuendelea kuwa viongozi

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,211
42,072
Katibu wa Itikadi naUenezi chama cha Mapinduzi (Paul Makonda) amewataka viongozi wa Umma na wa siasa kuacha mara moja tabia ya kusubiri ziara ya Viongozi wakuu wa Umma ndio waje kueleza mazuri na mipango au kutoa ufafanuzi wa mambo muhimu yanayo husu miradi ya jamii na utekelezwaji wake!

Paul Makonda amewataka viongozi wote wa Umma hasa wabunge na madiwani wa chama cha mapinduzi kuwafata wananchi na kwenda kuwatatulia kero zao na kuwasikiliza siyo mpaka wasubiri ziara ya Mh Rais au Waziri Mkuu ndiyo waende kugombania kipaza sauti kueleza wakati muda wa kueleza wanao mwingi !

Amesema kumezuka tabia ya wana CCM kukaa kimya tuu bila kuisemea serikali na chama kuhusu mazuri yaliyofanywa na kuwapa mwanywa watoa taarifa kutoa taarifa za uongo huku viongozi na wahusika wanaopaswa kusema na kutoa ufafanuzi wakiwa wamekaa kimya wakati wanalipwa na wengine waliomba kura kuwa viongozi wa nafasi mbali mbali ndani ya CCM.

Amesema ni wakati wa viongozi wa ngazi zote ndani ya CCM na serikali kuendelea kujitafakari kwakuwa mambo mengi yanafanywa na serikali lakini watu hawasemi wala kutoa ufafanuzi mpaka wasubiri ziara ya Rais….

Paul Makonda amehitimisha ziara yake kanda ya ziwa akiwataka viongozi wa serikali na chama kuwafata wananchi na kuwasikiliza!

Inasemekana kanda inayofuata ni kanda ya kaskazini mwa Tanzania au kusini…
 
Huyu Makonda huyu! Ni mtu safi sana, kwa nini watu wanaojiita wasomi sana hasa hapa TZ, huwa hawawezi sana kuongoza na kuleta mabadiriko ya kweli kwa wananchi?

Shida ipo kwenye elimu zao au ni uwoga usio na mantiki?

Wanataka kuongoza huku wakiogopa kanuni za kimataifa

Wamejaa hofu mpaka kwenye bongo zao, wanataka wabembeleze majizi kuepuka kufungiwa kuingia USA

Wengi wa wawasomi wetu ni washamba sana!
 
Huyu Makonda huyu! Ni mtu safi sana, kwa nini watu wanaojiita wasomi sana hasa hapa TZ, huwa hawawezi sana kuongoza na kuleta mabadiriko ya kweli kwa wananchi?

Shida ipo kwenye elimu zao au ni uwoga usio na mantiki?

Wanataka kuongoza huku wakiogopa kanuni za kimataifa

Wamejaa hofu mpaka kwenye bongo zao, wanataka wabembeleze majizi kuepuka kufungiwa kuingia USA

Wengi wa wawasomi wetu ni washamba sana!
Aiseee
 
Makonda ni sledge hammer au nyundo kubwa ya kunyoosha mambo ndani na nje ya chama tawala na wapinzani.
 
Kwa hilo namuunga mkono huyo DAB sijui wanakuwa wapi kueleza mazuri hayo ya serikali mpaka wafike viongozi wa kitaifa waanze kusema serikali imefanya hiki au kile au ina mpango huu au ule

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
KILA NIKIMTIZAMA PAUL MAKONDA.NDANI YAKE NAMWONA JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI.
kweli maana wote wauwaji. ile vita yake na wauza dawa za kulevya iliishia wapi vile ? mbona simsikii akiendelea nayo tena? vita yake na mashoga kina delicious je mbona haizungumzii tena? ile vita yake na waliotelekeza watoto je mbona ilikufa kibudu?
hahahaha mtu aliyefoji vyeti hawezi kuwa na akili timamu hata siku moja
nani alimpiga risasi TUNDU LISU?
 
Makonda ana nuka damu za raia wasio hatia
Hili limeshindwa kuthibitshwa na yoyote yule mbele ya Sheria
hivyo madai haya Yana muda mrefu si kweli,ni uzushi na upumbavu wa waleta hoja hizi mmoja wapo ni wewe ambae ubongo wako umejaa kamasi iliyochanganyika na utoko wa mbwa mwehu
 
Back
Top Bottom