Mbunge Abood ameendelea na ziara zake za mtaa kwa mtaa

Oct 8, 2023
37
17
29/11/2023
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Dkt. Abdul Aziz M. Abood ameendelea na ziara yake ya kikazi kwenye Kata ya KINGO, MAFIGA, MWEMBESONGO, MJI MPYA NA MAFISA.

Huu ni mwendeleze wa ziara yake inayopita mtaa kwa mtaa lengo ikiwa ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu na kuwaambia wananchi wa Kata hizo juu ya kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kata ya KINGO Mhe Mbunge amezungumza na wananchi na kusikiliza kero zao, Vilevile Mhe Mbunge akiwa kata hii ya KINGO ametoa TOFALI 350 NA SARUJI MIFUKO 10 ili kumalizia ujenzi wa choo unaoendelea kwenye Shule ya Msingi MWELE.

Kata ya MAFIGA Mhe Mbunge amesikiliza kero za Wananchi na kuzungumza nao pia Mhe Mbunge akiwa Kata hii ya MAFIGA ametoa vifaa vya TEHAMA ikiwemo PROJECTA pamoja na LAPTOP kwaajili ya kufundishia, vilevile Mhe Mbunge ametoa mifuko ya SARUJI 100 Shule ya MAFIGA Secondary kwaajili ya ukarabati wa madarasa, pia Mhe Mbunge ametoa Mikeka kwaajili ya kukalia watoto wa Chekechea kwenye Shule ya Msingi MAFIGA (B).

Kata ya MWEMBESONGO Mhe Mbunge amezungumza na wananchi na kusikiliza kero zao, baadhi ya kero amezitatua. Pia Mhe Mbunge ametoa MADAWATI 5344wwwqq kwa Shule ya Msingi MSAMVU (B) ambayo ipo Kata ya Mwembesongo.

Kata ya MAFISA Mbunge amezungumza na wananchi, amesikiliza kero zao na kuzitatua. Sanjari na hayo Mhe Mbunge akiwa Kata hii ya MAFISA ametoa TOFALI 1,000 na MIFUKO ya SARUJI 20 ili kusapoti ujenzi wa ofisi ya CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) Kata hii ya MAFISA
IMG-20231129-WA0716.jpg
 
aje mtaa wa kihimbwa road forest kata ya boma
ajionee hari ya barabara muaka yote na ameshafatwa sana jeuri

toka enzi za diwani na meya nondo
ikafika mahala.wazee wakanza kugharamia wenyewe barabara

mzee mstaafu Mzee Mwalukasa kahaingikia sana kutumia hela yake na wengine waligomaga hata kuumunga badaye kina foya nao wamejaribu

hari ya barabara ni mbaya sana
 
Watu wa mji kasoro bahari humuona huyu mwamba kama semi god wao,wakipewa ma-bus chakavu ya kusindikiza msiba basi anaimbiwa mapambio kila uchwao.

Shujaa JPM aliwahi mchana live bila kupepesa macho kwa tabia yake mbovu ya kuua v-wonder na kufanya sehemu ya kufugia Mbuzi.
 
Back
Top Bottom