Rais anayetumia ndege na msafara wa watu 30 na anayesafiri kwa barabara na msafara wa Magari 50, ni yupi anabana Matumizi?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Leo Krav Maga nipo Kiuchumi (Kiubahili) zaidi hivyo nawataka Political and Economic Pundits wa JamiiForums hapa mnidadavulie Kiundani ili nijue nani anauharibu Uchumi na nani pengine ndiyo anaukuza Uchumi.

Na tafadhali mtakaokuja Kunichambulia (Kunidadavulia) hapa mnipe Gharama ya Mafuta ya Ndege in Miles ikiwa Angani na Tozo za Ndege kwa Kuruka mara kwa mara na mpaka Parking Fee huko inakotua kila mara.

Na wale mtakaokuja Kunidadavulia (Kunichambulia) kuhusu Gari za katika Misafara mnipe Gharama za Mafuta, Matengenezo ( Services ) zake na uharibifu wa Kimazingira katika njia ambazo pengine huwa zinapita.

Mwishoni mwenyewe Kimoyomoyo tu nitaihitimisha kati ya anayependa Kusafiri sana na Ndege na Yule anayependa Kusafiri na Gari nani ana Faida Kubwa ya Kubana Matumizi ya Pesa za Walipa Kodi wa Taifa husika ( siyo Tanzania ) na nianze Kumpongeza.
 
Naomba kurekebisha kwenye title yako, naomba uchunguze au ufanye utafiti vizuri kuhusu msafara wa shujaa na Samia. Shujaa alikuwa na msafara wa siyo chini ya gari 100+ plus helkopita juu, Jeshi na wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama. Pia msafara wake uliambatana na ugawaji wa hela barabarani bila kufuata sheria, haya ni matumizi mabaya ya hela za umma
 
Naomba kurekebisha kwenye title yako, naomba uchunguze au ufanye utafiti vizuri kuhusu msafara wa shujaa na Samia. Shujaa alikuwa na msafara wa siyo chini ya gari 100+ plus helkopita juu, Jeshi na wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama. Pia msafara wake uliambatana na ugawaji wa hela barabarani bila kufuata sheria, haya ni matumizi mabaya ya hela za umma
Yaan jamaa baada ya kusoma comments kaona aingie mitini baada ya kujiona kumbe hakuwaza vizuri maana alisha sahau hilo la helicopter pamoja na kikosi kikubwa cha jeshi na mitutu mikubwa na na kugawa mihela.
 
Kama atatumia Airbus safari ya lisaa limoja(1hr) atatumia 2,700ltres that means 900km/hr Yani safari yakutoka dar to mbeya estimation ya fuel cost ambayo ni aina ya ATF ndio inatumika haya ni mafuta ambayo ni kerosene form ila ni kwa ajili ya aviation (mafuta ya taa) kwa tz approximately cost ni tsh 1500per litre...hivo basi 2700×1500=4,050,00/=..

Akitumia Boeing atahitaji kutumia litres 5,600 per hour 900km/hr = 8,400,000/=.....atakaetumia magari 50 yenye engine zaidi ya size 3000(v8) safari ya kilometre 900 atatumia si chini ya mafuta ya 250,000 kwa mwendo wa kawaida m/speed 250,000 × 50 cars= 12,500,000/=.......wa magari atahitaji madereva 50 ambao watalipwa posho na maradhi, bado ulinzi ambao sijui wanakuwa wangapi na wanalipwa how much.....wa ndege kwa hao watu 30 nae atawalipa posho na maradhi pia sijajua Kama ndege ya raisi huwa inakuwa charged gharama za kutua na kuruka ikiwa ndani ya viwanja vya Tanzania.
 
Back
Top Bottom