Kusafiri kwa lengo la kuimarisha uchumi wa Tanzania ni moja ya Kazi ngumu anayofanya Rais Samia

Abdalah Abdulrahman

JF-Expert Member
Aug 29, 2019
222
201
Uchumi wa Kidiplomasia ni uchumi ambao unatumia diplomasia kufanikisha malengo ya serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.Uchumi wa kidiplomasia unaongeza wawekezaji,uuzaji wa bidhaa nje,misaada,utalii,makubaliano ya kibiashara na mikopo nafuu.Ili malengo ya aina hii ya uchumi yaweze kufikiwa mahusino mazuri ndani ya nchi na kati ya nchi na nchi zingine ni ya msingi.Msingi wa kuimarisha mahusino mazuri ndani ya nchi ni pamoja na kutatua migogoro na kuimarisha mahusiano mazuri kwa wananchi wote bila kujali itikadi za vyama,dini kabila,jinsia au rangi zao.

Mahusinao mazuri kati ya serikali na vyama vya siasa,wafanyabiashara,wafanyakazi,na makundi mbalimali ya kijamii ni kichocheo kikubwa cha maendeleo endelevu.Kazi ya kuwaunganisha wananchi wa Tanzania imefikia hatua nzuri ambayo haikuwahi kufikiwa katika historia ya nchi hii tangia kupata uhuru.Wanasiasa na serikali wamekua wakijadili mambo na kukubalina kwa pamoja,kumekuwepo na mjadala wa siasa ya Tanzania na kikosi kazi ambacho kina wajumbe kutoka katika makundi yote ya kijamii kimewasilisha maoni yake kwa Mh Raisi.Vipo vikao mbalimbali kati ya serikali na vyama vya siasa,wadau wa maendeleo na makundi mbalimbali vinavyojenga kuimarisha mahusino mazuri.

Kwa upande wa pili,diplomasia ya uchumi inajengwa kwa kuweka mahusiano mazuri kati ya serikali moja na serikali nyingine.Mahusino haya kwa namna moja au nyingine yanahitaji viongozi hawa kukutana na kuongea pamoja na kuyafanyia maamuzi mambo mbalimbali pamoja.Safari zote ambazo amekua akisafiri Raisi Samia zimekua na manufaa makubwa kwa nchi.Hapa sitarudia manufaa ya safari bali nitaongelea ujasiri,uzalendo na ari aliyonayo Raisi samia katika kuwaletea Watanzania maendeleo licha ya kuwepo ugumu mkubwa katika kufanya safari za mara kwa mara za kikazi.Mambo haya nitayaeleza kwa kuonesha ugumu ambao msafiri anaupata kwa kusafiri ambao watu wachache wasiojua hilo wanalichukulia kama kusafiri ni starehe .

1. Kuna madhara yanayotokana na kusafiri

Kiwango cha mionzi ya kosmiki kinachomfikia binadamu huongezeka kutokana na kuongezeka kwa urefu(altitude) na latitudo pamoja na muda binadamu anaotumia kwenye mionzi. Hii ndio sababu ya mtu anayesafiri kwa ndege kutokana na umbali mkubwa kutoka usawa wa bahari kwa muda mrefu anapata kiwango kikubwa cha mionzi ukilinganisha na mtu anayesafiri na basi au chombo kingine kinachopita majini au ardhini. Inakadiriwa kuwa wahudumu wa ndege za safari ndefu hupata dozi ya mionzi kati ya 4-5mSv kwa mwaka, na kwa wale wa safari fupi inakadiriwa wanapata dozi kati ya 1-2 mSv kwa mwaka. Kiwango hiki ni juu ya kiwango anachopata mtu akifanya kipimo cha eksirei.Raisi wetu kutokana na mapenzi ya nchi yake na lengo la kuifungua nchi amesafiri Zaidi ya masaa X tangia aingie madarakani kama Raisi.

2. Uchovu unaotokana na safari

Hata ukiwa unasafiria first class namna unayolala sio sawa na unavyolala ukiwa umelel katika kitanda cha nyumbani.Hewa unayotumia,na mkandamizo ndani ya ndege kwa muda unaosafiri haulingani na hali ya hewa unayo ivuta ukiwa nyumbani.Hivyo basi mazingira ya kusafiri ni magumu kwa aina yeyote ya usafiri.

3. Majanga yatokanayo na safari za anga.

Kwa nafasi aliyofikia Raisi ni wazi kuwa huko alipopitia katika nyadhifa mbalimbali alishawahi tembelea nchi nyingi duniani na pengine kukaa katika nchi hizo.Kwa watu ambao tumeshaishi nchi za watu wengine tunajua adha zilizopo kwenye hizi nchi.Ni wazi kuwa kama ni chaguo lake binafsi na kama kuna njia mbadala ya kutokusafiri na kuwafikia wawekezaji na kuimarisha uchumi wa kidiplomasia ni wazi kuwa asingetaka kusafiri kutokana na majanga yanayoweza kutokea kutokana na hivi vyombo.Hivyi ni vyombo ambavyo ametengeneza binadamuhivyo lolote liaweza kutokea,hivyo basi kujitoa kwa ajili ya watanzania sio jambo ambalo kila mtu anaweza kulifanya.

4. Mabadiliko ya Hali ya hewa.

Tunajua matatizo mbalimbali katika miili yetu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa,mafua,kutokupumua vema,joto la kupita kiasi au baridi kali,Mabadiliko ya hali ya hewa na ratiba ngumu za safari hizi ni miongoni mwa ugumu ambao anaupata mama yetu Raisi Samia

Mambo haya yote anayafanya mama kwa ujasiri na moyo mkubwa alionao wa kuwahudumia wananchi wa Tanzania.Tuendelee kumuunga mkono Raisi wetu na kumuombea aweze kututumikia mpaka 2030.
 
hivi mkuu mabalozi ambao wapo nchi za kigeni wa serikali yetu wana kazi gani huko.
 
Mkuu mbona wewe Bw. Ally hauuungi mkono juhudi za kuutakatisha mkaaa uwe king'aaaacho😂😂
😁 ni kupoteza mda tu ni sawa kumuogesha nguruwe .

hakuna kitakachobadilika na wala waislamu hawawezi kumuona msafi zaidi sana utapoteza maji yako na sabuni yako tu
 
Uchumi wa kileo andaa mazingira watu waje kwako sio wewe kila leo uko kwao huo sio uchumi mengine tutadanganya tu hadi soko la soya, parachichi akatafute Rais hapana mawaziri wako wapi, Bodi ya mazao mchanganyiko wako wapi au wamelala zao pale ubungo hawana habari na mtu
 
Kusafiri kila siku kuwafuata hao wanaoitwa wawekezaji haitasaidia kitu.

Zaidi watakuona hamnazo + ombaomba.

Hii ipo hata kwenye maisha ya watu wakawaida.

Kadiri unavyojipendekeza ndivyo watu wanakukataa zaidi.
 
Endela kujifungia usikutane na watu wenye biashara na pesa zao ukadhani utaondokana na umasikini. Sisi masikini tulifundishwa elimu mbaya sana ya kuwachukia matajiri na ndio inayotutafuna mpaka leo. Kasome Rich Dady Poor Dady
 
"Rich Day Poor Dady" ndiyo nini hiyo?

Title sahihi ya kitabu ni Rich Dad Poor Dad.

Haya sasa, umeanza kuharibu hapa kwanzo, utaweza kuhimili vishindo tukiendelea?

Acha kukurupuka mkuu, kaa nyumbani tulia. Fanya mambo yako kwa bidii. Acha kushobokea wanaume kisa wanapesa.

Kama ipo ipo tu.
 
Back
Top Bottom