Rais Samia atakumbukwa kama Mtu wa maamuzi magumu na muasisi wa mageuzi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii wa kizazi kipya

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,053
49,737
Binafsi huwa namkubali sana huyu Rais na kutokana na msimamo wangu kuna watu wenye akili ndogo huwa wanajua labda Mimi ni chawa au nalipwa wakati wala hata sina kadi ya chama chake.

Iko hivi, nimebahatika kuwaona Marais wengi ukiacha Mwl. Nyerere ambae pia nimesoma na kusikiliza habari zake.

Sasa Kwa muda mfupi tuu aliokaa Madaraka Rais Samia amefanya maamuzi na Mageuzi makubwa sana na kuyasimamia bila kujalisha nani amemkera au nani anasema nini ilimradi tuu yeye anaamini ni kwa maslahi mapana ya Nchi.

Baadhi ya hayo maamuzi magumu na makubwa aliyofanya ni;

1. Maamuzi ya Kuagiza Chanjo za Uviko Katikati ya Propaganda za watu wa dini na yule Rais wa Wanyonge.
Licha ya makelele sijui kutukanwa nk lakini aliziba maskio akaagiza na Nchi ikawa intergrated tena kwenye Jumuiya ya Kimataifa.

2. Kuwahamisha Maasai Kutoka Ngorongoro.
Licha ya propaganda kibao za waliokuwa wananufaika na uwepo wao, upotoshaji na kutukanwa na kusema anauza Nchi Kwa Waarabu lakini hakurudi nyuma akijua kwamba dhamana ya kulinda Rasilimali za Nchi iko mikononi mwake.

3. Mageuzi ya Kisiasa.
Katikati ya Sukuma gang waliofura Kwa hasira Samia alionana na wakosoaji wa Utawala wa awamu ya 5, akawafingulia kuwa huru Kisiasa na akaenda hadi kwenye majukwaa yao kuhutubia. Alifungulia waliokuwa magerezani kuanzia Mashehe wa Uamsho hadi Wanachama wa upinzani, alifungulia Magazeti nk.

4. Mageuzi Makubwa ya Kiuchumi.
Alirithi Nchi yenye hali mbaya kiuchumi na Serikali ikiwa inapeleka pesa kwenye miradi mikubwa tuu huku sekta zingine zikiwa paralysed.Lakini ndani ya miaka 2 na nusu amefanikiwa kusonga mbele na miradi na kuanzisha mipya na kufufua sekta zingine zote za Uchumi kuanzia NHC Hadi Kilimo na Sasa Uwekezaji unamiminika. Matokeo ya haya Mageuzi ni utitiri wa miradi across sectors.

5. Kutangazia Umma kwamba Miradi yote Mikubwa ni Mikopo na yeye atakopa.
Hapa kulikuwa na propaganda nyingi na uongo ambao watu waliaminishwa sawa na ishu ya chanjo kwamba Kila kitu tunafanya Kwa pesa zetu wakati ni uongo wa mchana.Bila kupepesa macho Rais Samia alitamka wazi kwamba miradi yote mikubwa ni mikopo tena commercial.

Akasisitiza kwamba Serikali yake itakopa Ili kuharakisha ujenzi wa miradi na kufufua uchumi. Kukawa na Mjadala mkubwa mpaka Ndugai akataka kumpara Rais baada kuonjeshwa moto akazima hadi leo hii mambo inaenda. Deni la Serikali limepaa ingawa bado liko mbali na mstari wa Ukomo, Serikali inakopa na inalipa Madeni na maisha yanaenda.

6. Kuanzisha tozo ya Mafuta na Miamala Kwa ajili ya Barabara, Shule na Vituo vya Afya.
Huku Dunia ikiwa inaendelea na kupata athari za Uviko 19 na janga la Ukraine lililosababosha bei ya mafuta na bidhaa zingine kupaa,Rais Samia alisema hatuna Wajomba wa kujenga Nchi lazima tubanane wenyewe Kwa wenyewe.

Hapa alianzisha tozo za miamala na mafuta, licha ya kelele na Kila aina ya vitimbi hakurudi nyuma sana sana alipunguza tozo na kuleta ruzuku ya mafuta lakini Serikali ilikataa kufuta hizo matokeo yake Kwa mda mfupi alijenga zaidi ya Vituo vya Afya 1,000 Nchi nzima, maelfu ya vyumba vya madarasa na kukomesha Kilio Cha watu wa Vijijini kutokuwa na Barabara Kupitia TARURA, Bajeti imeongezewa mara dufu na Vijiji vinafikika na Uchumi unakua.

7. Sakata la DP World na Bandari.
Hili nalo bado liko moto sana kama la Ngorongoro.Wale waligeuza Bandari yetu shamba la bibi wanatumia Kila njia kupotosha kwamba anauza Nchi ila Rais amekaa Imara na sana sana ameiagiza Elimu zaidi na pia ku deal na wale wanaotaka kuhatarisha usalama wa Nchi Kwa sababu zao za kipuuzi na ambazo hazina mashiko. Hapa kwenye bandari atakomesha wizi na urasimu wa miaka Mingi Kwa maslahi ya wachache.

Hayo ni Kati ya masuala machache makubwa aliyoyafanyia Mageuzi na yamemlipa.

Mengine yaliyoko kwenye pipeline ni kufuta mashirika yasiyoleta faida, kufanya Mageuzi ya mitaala ya shule kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu, Mradi mkubwa wa gas (Ikumbukwe Jiwe alisema gas sio yetu imeuzwa),Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo nk..

Mwisho Pamoja na kufaulu mambo mengi ila kuna machache amefeli na aliongea Kupitia Bunge mfano kupunguza matumizi ya Serikali kwenye mafuta na ununuzi wa magari na vipuri kutoka bil.550 Kwa mwaka hadi Bilioni 50. Hapa Serikali ilitaka iwe inawapa maafisa magari na mafuta wajihudimie moja Kwa Moja. Toka limeongelewa Bungeni naona kukosa kimya maana nalo lilizusha gumzo ingawa ni wazo zuri.

My Take
Mungu akimpa huyu Rais uhai Hadi 2030 ataiacha Nchi ikiwa imepaa mbali sana kwenye Maendeleo. (Maneno machache vitendo Mingi).

Mungu mbariki Samia, wanaomchukia ndio kwanza wanamuimarisha na kumpa bahati zaidi ya kufanikiwa.
20230710_151831.jpg
20230710_151921.jpg
 
Back
Top Bottom