Dr Masaburi ni mkristo kisheria mke halali ni mmoja hao wengine ni hawara tuu
UMENENA....na hata asingekuwa Mkristo hata Muislam kama Mke ni yule ulofunga nae ndoa ya Kidini hao wengine kama hujafunga nao ndoa ni hawara tuu...hawakubaliki
Dr Masaburi ni mkristo kisheria mke halali ni mmoja hao wengine ni hawara tuu
labda kaisaidia familia yako kucheka ule udhalilishaji.Wala hakutek
Wala hakuteleza ila ameisaidia familia. Kama hao wake wapo na walihudhuria hafla hiyo, na watoto pia walikuwepo kwenye tukio hilo, mtu wa baki anawezaje kuwakana sasa, na kwa kutumia mamlaka gani, ambayo marehemu katika uhai wake hakuyatumia?.
Magu ameidhalilisha familia na amemuhukumu marehemu.katika hali ya kawaida ni kuwa kwenye misiba mingi madhambi au madhaifu ya marehemu huwa hayawekwi hadharani. hutokea pia hata maradhi yaliyosababisha kifo cha marehemu hayatangazwi.
fikiria kama familia ya marehemu wametangaza kuwa amefariki kwa shinikizo la damu,halafu ajitokeze mtu mwingine na aseme kuwa yeye ni rafiki wa marehemu na anajua kuwa amefariki kwa ukimwi!
hata kama ni ukweli lakini je,huo si udhalilishaji?
kwa christian yesKwa hiyo kuwa na Wake wawili au zaidi ni dhambi?
Dr Masaburi ni mkristo kisheria mke halali ni mmoja hao wengine ni hawara tuu
wacha unafiki wewe,
uko tayari kwenye kifo cha baba yako au mama yake mtu aje ashike mic nakutangaza madhambi ya marehemu??
Sikuungi mkono, kwenye msiba wa masaburi(RIP) ilionekana wazi kabisa kuwa kuna Makundi tofauti yalivaa sare tofauti, alichofanya jpm ni kuondoa umimi na ubinafsi wa baadhi ya wahusika na si kutaja dhambi za marehemuwacha unafiki wewe,
uko tayari kwenye kifo cha baba yako au mama yake mtu aje ashike mic nakutangaza madhambi ya marehemu??
mkonoMkitaka haya yasiwapate muache kuchepuka na muheshimu ndoa zenu, otherwise Magufuli kafungua njia na utakuwa mwendelezo. No more unafiki, kila mtoto ana haki kwa mzazi wake haijalishi alipatikana ndani ya ndoa or not. Hutaki haya yaikuye familia yako, heshimu ndoa yako.
Wananchi hivi kuficha ukweli ni hulka ama mila za sisi waafrika? Niseme tuu marehemu aliishi na wake hao aliowasema Raisi bila kificho na hata kanisa alilokuwa akipata huduma za kiimani lilijua. Kama alikuwa ni Mromani Katoliki...Basi kumbuka sakrementi ya kitubio ya kukili imani yake (mojawapo ni kukili amefanya kosa la kuoa mitala na kamba yeye katika sakramenti ya ndoa ameoa mke mmoja) na kama alifanya hivyo akiwa hospitali basi kulingana na misingi ya kanisa hilo huyo alistahili huduma zote za kiroho katika safari yake ya mwisho hapa duniani. Pili Raisi kama binadamu alizungumza kile ambacho marehemu alikiishi, sasa kama kati yetu tunataarifa kinzani kwamba marehemu hauishi maisha hayo basi na aseme kile kilicho sahihi (hapo utasema Raisi alikosea). Tatu, inawezekana islete mantiki sasa kwa mtazamo wa jumla kwa jamii juu ya alichokisema lakini kwa ustawi wa familia ni muhimu sana kusema kitu ambacho hata jamii nje ya familia wanakijua kuhusu maisha ya familia na wigo wake kwani itawasaidia wana familia kuzingatia ukweli kwamba wao si adui bali ni ndugu wa damu. Nne Raisi wetu Magufuli sio kiongozi wa kwanza kusema kiongozi fulani ana mitala (ameishi na wake zaidi ya mmoja kulingana na dini yake ya kikristo) Kumbukeni kwenye mkutano na waandishi wa habari mwaka 1995 Baba wa taifa hayati Mwl. J.K. Nyerere alisema nanukuu (" Kipindi hicho mwenzangu George Kahama alikuwa ameendelea ana wake wawili") na kiongozi huyu aliweza kusema vile kwasababu sio kwamba alikuwa kiongozi bali alikuwa Rafiki wa mlengwa na hivyo alikuwa na Moral authority ya kuzungumzia kiasi fulani maisha ya jamaa yake kwani yeye amekuwa sehemu ya maisha hayo kwani wameishi kama ndugu, rafiki na jamaa wa karibu. Kwa alilolifanya mheshimiwa Raisi kwa mtazamo wangu kama mwili wa marehemu ulipelekwa kila nyumba ya wake aliokuwa naishi nao na kwenye risala akatajwa mke na watoto wa nyumba moja hapo panatatizo ni bora kulisema ili jamii ikajua ukweli wa maisha ya marehemu.Dr Masaburi ni mkristo kisheria mke halali ni mmoja hao wengine ni hawara tuu
Iweje ambae hakuwepo awe na kimbelembele kumthibitisha?Rais amegonga pale ambapo ni shida sana wengi kutamka. Tatizo ni kubwa, wanaume wanaficha wenzi waliozaa nao, wanawake wa ndoa wanadai wao ndio wana haki, sheria zinanyima haki watoto ambao hawajulikani hata wakijitokeza (labda mtoto huyo awe na tajiri), makanisa hayawataki watoto wa nje, waislamu wanawaita wanaharamu, lakini kwa mila zetu mwanaume akizaa mtoto huyo ni wake, halali.
Kwa hiyo Magufuli alikuwa halali kwa mila zetu za Kiafrika. Ametufungulia njia ya kutambua watoto wetu mapema.
Halafu inakuwaje mtu ambaye hakuwepo wakati mtu anazaa na huyo mpenzi au mke wake lakini anakuwa kimbelembele kumkana mtoto anayejitokeza kuwa ni mtoto wa marehemu.
suala hapa ni kuwa kama familia yenyewe wameamua kuficha aibu ya marehemu ya kuwa na wake wengi ilhali yeye ni mkristo,je ilikuwa ni sahihi kwa mtu mwingine kukanusha na kuweka wazi mbele ya halaiki? kama ilikuwa ni kutaka kutoa ushauri kwa watoto si JPM angewaita faragha azunguze nao?
Dr Masaburi ni mkristo kisheria mke halali ni mmoja hao wengine ni hawara tuu