Rais ametumia Moral authority sio legal authority

Rais ametumia Moral authority sio legal authority

Kwanza wewe mtoa mada unapaswa utujibu kama Makufuri alisena haya kama nani...je, alisema kama msemaji wa familia au msemaji wa hiyo michepuko ya Masaburi?
Mheshimiwa ameongelea Wake za Marehemu, na sio Michepuko. Ukiangalia kwa upande mwingine waweza kuta katika mahusiano hayo kulikuwepo na aina fulani ya urasimishaji, labda kulikuwa na ndoa za kimila, n.k. Mh Raisi amekuwa mkweli sana,hata ambapo pengine ukweli huwa unafichwa mara zote.
 
Rais amegonga pale ambapo ni shida sana wengi kutamka. Tatizo ni kubwa, wanaume wanaficha wenzi waliozaa nao, wanawake wa ndoa wanadai wao ndio wana haki, sheria zinanyima haki watoto ambao hawajulikani hata wakijitokeza (labda mtoto huyo awe na tajiri), makanisa hayawataki watoto wa nje, waislamu wanawaita wanaharamu, lakini kwa mila zetu mwanaume akizaa mtoto huyo ni wake, halali.
Kwa hiyo Magufuli alikuwa halali kwa mila zetu za Kiafrika. Ametufungulia njia ya kutambua watoto wetu mapema.
Halafu inakuwaje mtu ambaye hakuwepo wakati mtu anazaa na huyo mpenzi au mke wake lakini anakuwa kimbelembele kumkana mtoto anayejitokeza kuwa ni mtoto wa marehemu.
 
Sasa kama michepuko itakuwa ubaoewa bafasi kubwa namna hiyo, nini basi maana ya kuwa na ndoa. Je Masaburi alikuwa amefunga ndoa na hiyo michepuko? Je, kitendo kile cha rais kinaweka precedent gani hasa kuhusu uadilifu kwenye ndoa? Rais anashadidia michepuko, wakati vyombo vingine vya serikali vinakazana kudiscourage michepuko? Refer Baki njia kuu, michepuko sio dili?
 
Mambo ya familia ni ya familia, Haipaswi kuyaingilia, yanamalizwa katika vikao vya familia au mahakamani na siyo kwa presidential decree!

Wanaosema eti kwa kusema vile kaisaidia familia, kaisaidiaje familia?, kwamba kwa kuwa yeye kasema na kwa kuwa yeye ni mkuu basi familia itatii?

Siyo rahisi kihivyo!
Kwanza yeye magufuli ndiye kachochea migogoro kwa kuhalalisha uzinzi na kuwatambua watoto waliopatikana kwa uzinifu, na hii ndiyo tabia ya wanaCCM wote....wazinzi wakubwa!
 
Mkuu hapa NDOA ni moja tu...hao wengine ambao makufuri anaowapigia debe ni VIMADA tu. Lakini sishangai kwa kuwa watu wa CCM kuwa na vimada lukuki ni jambo la kawaida kabisa.
kweli mkuumpaka nawaza kwa sauti dar hapa ukiwa na mke mmoja kumtyunza ilivyo gharama uwe nao watano watoto ishirini kila mmoja atoe shida zake mkulu kabana dili. biashara haziende aisee lazima unyooshe
 
sijui kama ilikuwa sehemu sahihi japo naamini ndoa za namna ile huwa zinamikwaruzano sana hasa baba kama hajaweka mambo sawa
Huyu mtetezi wa Michepuko nahisi naye ana michepuko kwa hiyo anaandaa utaratibu wa Michepuko yake, kitu kibaya ni kupuuza mafundisho ya kanisa ambayo yeye pia amepitia sasa anajiona malaika
 
Unaweza kutuambia cheti cha ndoa kinathamani gani, lini mwenye thamani hiyo hutamalaki na kujipiga kifua akisifia ubora wake dhidi ya maungayembe!!!!!!
Fungua geti la ufahamu.
Usilete story za kwenye vipeperushi.
Rais amegonga oale ambapo ni shida sana wengi kutamka. Tatizo ni kubwa, wanaume wanaficha wenzi waliozaa nao, wanawake wa ndoa wanadai wao ndio wana haki, shria zinanyima haki watoto ambao hawajulikani hata wakijitokeza (labda mtoto huyo awe na tajiri), makanisa hayawataki watoto wa nje, waislamu wanawaita wanaharamu, lakini kwa mila zetu mwanaume akizaa mtoto huyo ni wake, halali.
Kwa hiyo Magufuli alikuwa halali kwa mila zetu za Kiafrika.
Halafu inakuwaje mtu ambaye hakuwepo wakati mtu anazaa na huyo mpenzi au mke wake lakini anakuwa kimbelembele kumkana mtoto anayejitokeza kuwa ni mtoto wa marehemu.
 
Hv magu kaongea uongo??

Na.km.sio je.kusema.ukweli nikuaibisha familia??

Nahisi wabongo tunatabia.ya kutaka kutoa sifa nzur kwa kila.marehem

Anyway
Watajua wenyewee
 
Usishangae siku za usoni akajitokeza mwanamke nwingine akidai na yeye ni miongoni mwa wake za marehemu
 
Kua na wake wa nne sio jambo la ajabu na pia nafikir hata hyo familia moja iliyotajwa inatambua kua kuna wenzao...
Hakuna sentence yenye kufunga kama kusema kua marehemu alikua na watoto wa tano na mke mmoja mind you imetamkwa mbele ya hadhara.
Kama ni ustaarabu mtoa risala Ange acknowledge uwepo wa hao wengne kwa sababu ni kwel wapo na sio kuficha.
Mh rais alikua sahih kuliweka waz ila labda namna ya kuliweka ndio inashida
 
Preemptive strike to save his own backyard.

Meseji nzito kwa "mji" wake mwenyewe!
 
Mkuu nimesoma nimeishia njiani baada ya kuona hii ni hoja ya kipuuzi sana. Kwanza wewe mtoa mada unapaswa utujibu kama Makufuri alisena haya kama nani...je, alisema kama msemaji wa familia au msemaji wa hiyo michepuko ya Masaburi?
Kama mwenye dhamana ya kulinda familia zote katika taifa hili kwa misingi maadili yataifa letu na sheria zetu
 
Kua na wake wa nne sio jambo la ajabu na pia nafikir hata hyo familia moja iliyotajwa inatambua kua kuna wenzao...
Hakuna sentence yenye kufunga kama kusema kua marehemu alikua na watoto wa tano na mke mmoja mind you imetamkwa mbele ya hadhara.
Kama ni ustaarabu mtoa risala Ange acknowledge uwepo wa hao wengne kwa sababu ni kwel wapo na sio kuficha.
Mh rais alikua sahih kuliweka waz ila labda namna ya kuliweka ndio inashida
Point sio "AJABU" bali uadilifu wa kiapo cha ndoa.
Unamshawishije mjukuu wake kuyaamini mafundisho ya kanisa ambayo babu yake hakuyafuata.

Mambo ya uani yaachwe uani na kushughulikiwa huko huko uani.

Tujihusishe na mambo ya hadhira hadharani.
 
Hivi ina maana marehemu alikuwa anamwambia siri zake zote? Anaijua Michepuko na watoto wa familia kuliko hata msemaji wa familia? Huu ni ulimbukeni wa madaraka
 
Back
Top Bottom