Baada ya mazishi ndugu jamaa na marafiki wataitwa kwa ajili ya kikao cha ndani ya familia au koo huku M/Kiti wa mtaa akishirikishwa japo siyo lazima sana ila muhimu.
Muhtasari wa kikao utafafanua kinaga ubaga kuhusu Mali,Mke na Watoto wa marehemu, pamoja na kumchagua msimamizi wa Mirathi wataenda Mahakamani kufungua shauri la Mirathi. Mahakama kwa kushikirikiana na baraza la wazee litajiridhisha kuhusiana na mali, Mke/Wake/,Mtoto/Watoto wa marehemu na kuondoa sintofahamu yoyote iliyopo kwenye familia na kumtambua rasmi msimamizi wa mirathi.
Lakini haya yote yanakamilika baada ya mahakama kutoa muda(notice) ya siku 90 kwenye magazeti na ubao wa matangazo wa ofisi za Serikali ili kuwapa fursa wale wote wenye kila aina ya malalamiko dhidi ya shauri husika ili yashughulikiwe. Haya yote tumejiwekea sisi wenyewe Sheria, Taratibu na Kanuni. Mengine yataongezewa au kusahihishwa na wajuvi zaidi pale wanapoona panafaa kufanywa hivyo.
Hivyo basi, Ndg YULE hakuwa na sababu yoyote ile ya kuongea maneno yale yenye ukakasi na kumpunguzia credibility/PR yake? , Ndg YULE hakutumia busara na hekima kutatua kile anachofikiri ni tatizo!!, Ndg YULE anatakiwa ajitambue kuwa yeye ni Kiranja Mkuu hivyo si kiingiacho bali kimtokacho ndiyo Najisi, Ndg YULE afahamu kuwa "Utapimiwa kipimo kilekile unachowapimia wenzako".
Alamsiki!!