Rais ametumia Moral authority sio legal authority

Rais ametumia Moral authority sio legal authority

Mambo ya familia ni ya familia, Haipaswi kuyaingilia, yanamalizwa katika vikao vya familia au mahakamani na siyo kwa presidential decree!

Wanaosema eti kwa kusema vile kaisaidia familia, kaisaidiaje familia?, kwamba kwa kuwa yeye kasema na kwa kuwa yeye ni mkuu basi familia itatii?

Siyo rahisi kihivyo!

Familia zina siri zake, kuna kubambikiziwa watoto, kuna kuchepukiwa, kuna kupiga talaka kimyakimya

Sasa from no where mathalani mtu aje aseme namjua fulani na fulani nae ni mtoto wa marehemu, wakati labda mtoto yule si wako na ndiyo chanzo cha ugomvi wako katika mahusiano lakini hata hivyo umelifanya siri, hii inakuwa very insensitive kwa msemaji kuyasema hayo!
Hii haikuwa siri mkuu na pale walifanya unafki mkubwa maana hao wake wengine na watoto wengine walikuwa eneo la tukio wakiwa wamevaa sare na inajulikana hawa ni wajane, hawa ni watoto wa marehemu. Halafu kwenye Ulugy eti mke mmoja. NONSENSE!
 
Mkuu kwa heshima zote! Hicho unachosema siyo kweli isipokuwa amewatendea haki stahiki mbele ya Muumba.
Je ni uongo kuwa Marehemu alikuwa na Mke zaidi ya Mmoja?
Acheni maisha ya kinafiki. Ustaarabu gani ? Familia ipi imesononeka ile iyojichukulia hadhi ya kuwa watoto halali wa marehemu na wengine kuonekana vijakazi?

1. Hili jambo linahitaji busara kulitatua.
2. Inategemea marehemu mwenyewe aliiaminishaje familia yake enzi za uhai wake. Kama alisema alikuwa na mke mmoja si rahisi wanafamilia kuelewa kuwa alikuwa na wake wengi na watakuwa wake wengi hadi wangapi wa kuweza kuaminika kama marehemu hakuwataja mwenyewe?
3. Nilishashuhudia kifo cha ndugu ya rafiki yangu, ambaye alimwaminisha mkewe na watoto kwamba hakuwa na mke mwingine.
4 Lakini siku zilipokariabia kurudi kwa baba, ilibidi akiri mbele ya mkewe na ndugu waliokuwepo kuwa amekuwa akimdanganya muda wote wa ndoa yao, lakini haikuwa kweli.
5. Haikuwa rahisi kwa mke wake kuamini na alipokuwa anakaribia kukata roho aliomba radhi tena kwa mkewe na kuomba aambiwe kama amesamehewa. Mkewe kwa huzuni alisema: "Nimekusamehe".
6. Jambo la kujifunza ni kuwa wakweli na waaminifu kwa ndoa zetu ili tuweze kuepusha migogoro tunaporudi kwa baba.
 
Mi naona Rais alifanya vema maana tayari kulikuwa na ishara ya mtafaruku ktk familia
 
6. Jambo la kujifunza ni kuwa wakweli na waaminifu kwa ndoa zetu ili tuweze kuepusha migogoro tunaporudi kwa baba.


Na hapo ndipo Mhe.amemsadidia Marehemu na ndugu wengine kupata nafasi ya mapema zaidi ya kusameheana!
 
Mungu mwema. Mzee Yakobo katika waraka wake anatuasa akisema "Muwe wepesi wa kusikiliza, lakini si wepesi wa kusema"
 
incase case, kesi iko mahakamani, vipi hao desperate housewives wakipeleka record ya speech hii, vipi itawasaidia?
 
. Big Up Mheshimwa kwa kusema ukweli daima. Haipendezi kushiriki kumsindikiza mpendwa na muda huo uongo kusemwa mbele yako na upatapo muda wa kusema neno usiseme.
cjui ni kipi ambacho ni kigumu kulewa ndugu...wakristu wanatambua ndoa ya mke mmoja tu kulingana na taratibu zao lakin km nchi ina sheria na taratibu zinazohusu mambo ya ndoa na mirathi sasa mi sielew kwann unalazimisha polygamy iwe halali kwao!
 
UKIJIONDOA KTK MSAFARA UTAWEZA KUIELEWA DHAMIRA YA MANENO YA MH MAGUFULI KTK MSIBA WA MASABURI

Magoiga SN-Mwanza

Yeyote aliyezaliwa katika ndoa za mitaala atakuwa amemuelewa sana mh Rais na hususani ushauri wake kwa familia ya marehemu masaburi.

Watu wengi wamenifuata Inbox kutaka kujua ni nini mtazamo wangu kuhusu hili suala. Wengi wameonyesha kulalamika na kumlaumu Mh Rais kwa maneno yake aliyoyasema msibani. Kwa kuwa ni vigumu kumjibu kila mtu inbox kuhusu mtazamo wangu ktk hili, naomba nitumie fursa hii kukushirikisha ili tuweze kutafakari pamoja.

i) Kwanza kabla ya mazishi, ulizuka mvutano mkubwa sana kuhusiana na wapi mwili wa marehemu uhifadhiwe. Kila familia ilitaka mwili ufikie kwao. Mvutano ulikuwa mkubwa sana kila familia ikitaka japo mwili ukalale ktk familia yao mara moja mara moja kabla ya kuzikwa. Hivyo mwili wa Marehemu ulipitishwa kila familia. Je unalijua hilo??

ii) Kwanza Mh Rais aliongea yale maneno kama rafiki wa familia, aliyeijua vyema familia ya marehemu na kama mtu ambaye asingependa siku za usoni familia ile ikaingia ktk mgogoro mkubwa.

iii) Kuna mahala aliwaasa vijana/watoto wa marehemu kuwa, wakishikamana wataweza kuwaunganisha mama zao. Alisisitiza mshikamano maana alijua kuna shida mahala na inaweza kuleta shida siku za usoni.

iv) Ushauri unaotolewa mbele ya marehemu unaweza kuwasaidia sana watoto na familia inayobaki ktk kujitafakari pale panapohitaji kufanya hivyo.

V) Sote tunajua, mzee wa familia anapofariki mambo mengi huenda kombo, familia huparaganyika kutokana na kugombania mali, mgawanyo usio sawa nk. Hususani ktk hizi ndoa za kimila

vi) Katika ndoa za mitaala Afrika, familia yenye financial power ndiyo inayohodhi kila kitu ikiwemo haki ya mazishi, usimamizi wa mirathi nk

MR RAIS ALIKOSEA AU ALIKUWA SAWA??

Hilo swali sina jibu lake maana kusema alikosea au alikuwa sawa inategemea sana uwezo binafsi wa mtu mmoja mmoja ktk kuitumia vyema akili yake kulitafakari suala hilo. Hivyo nitakachokifanya ili kulijibubswalinhilo, nitkuuliza mswali yenye mwongozo ili utumie muda wako kuyatafakari na kulijibu swali hilo kadiri ya uelewa wako

Akili ndogo hulalama badala ya kujihoji. Hivyo badala ya kubaki ukilalama ni vyema ujaribu kuyatafakari maswali haya ili uoate jibu iwapo Mh Rais alikuwa sawa au hakuwa sawa

i) Je ni kweli masaburi alikuwa na mke mmoja pekee?? Nini tafsiri ya Mke, na ndoa.

iii) Je ni kweli alikuwa na watoto 5 pekee?? Nini tafsiri ya watoto??

iv) Je ktk familia zetu za Kiafrika kuna wakati baadhi ya watoto hukosa stahiki zao pindi mzazi anapofariki?? Taja mazingira ambayo yamekuwa yalisababisha watoto na wajane kukosa stahiki zao

v) Kama alikuwa na watoto zaidi ya 20, na wake zaidi ya 4. Ila wanaotajwa ni mke mmoja na watoto 5. Unategemea kutakuwepo na amani ktk familia hiyo baada ya marehemu kuondoka?? Au tutegemee magazeti kuanza kuripotinkuhusu mgogoro wa kugombania mali za urithi nk?

#My_Take Kuna wakati mtu unahitaji kuondoka ktk msafara wa Nyumbu ukae pembeni ndipo unapoweza Kuyaona mambo ktk mtazamo tofauti 'in a different perspective'. Bika hivyo, utakiwa unawaza kinyumbu nyumbu kwa kutegemea akili ya anayeongiza msafara wenu
Acha kutetea utumbo.

Magufuli ana moral authority kwenye familia yake tu. kulikobakia ni Legal authority.

Familia si yake , yanini kuingilia mambo yake??? kiherehere cha nini??
 
Mteteeni ila kwa ukweli ameteleza na ameikwaza familia.
Familia iliokwazwa ni ipi sasa hapo kwa mtazamo wako? Ile iliotajwa kwenye risala au zile familia zilizofichwa kwenye risala!? Kwa mtazamo wangu labda wale 5 na mama Janet labda lakini wale 15 na mama zao 3 bila shaka watakua walitabasamu kumsikia rais akisema kile tulicho kisikia. Yaani mkuu uwe na mke zaidi ya mmoja ili hali ukijua dini au utaratibu wako hautaki, unataka siku ukifa hayo yasisemwe? No, Big No
 
suala hapa ni kuwa kama familia yenyewe wameamua kuficha aibu ya marehemu ya kuwa na wake wengi ilhali yeye ni mkristo,je ilikuwa ni sahihi kwa mtu mwingine kukanusha na kuweka wazi mbele ya halaiki? kama ilikuwa ni kutaka kutoa ushauri kwa watoto si JPM angewaita faragha azunguze nao?
Upotoshaji ukweli hadharani,unakabiliwa hapo hapo!
..period!
 
cjui ni kipi ambacho ni kigumu kulewa ndugu...wakristu wanatambua ndoa ya mke mmoja tu kulingana na taratibu zao lakin km nchi ina sheria na taratibu zinazohusu mambo ya ndoa na mirathi sasa mi sielew kwann unalazimisha polygamy iwe halali kwao!


Nimekulewa waliozoe kuishi kinafiki wataendelea kuwa hivyo huko nyumba ya pazia wakita Bwana Bwana! Huna haja kunijibu kama hujui na hoja kuwa Magufuli ni muongo na kama si muongo hoja yako ni mfu na unafiki. Kanisani watambue mke mmoja alafu mhusika yeye anatambua anawake zaidi ya mmoja na Sheria ya Nchi inaruhusu.


Kigumu unachoshindwa wewe kuelewa ni ukweli kuwa nyuma ya Pazia Marehemu pamoja na uchaji wake Kanisani kumbe alikuwa kinyume na Kanuni ya Kanisa ya kuwa na mke mmoja.
 
ana suport michepuko wakati huohuo,mashirika yanasema michepuko sio dili..yaan hapa nilipo,mbav zangu zinauma kwa vcheko.
 
Back
Top Bottom