Rais amekwishasema "tuendelee kuchukua tahadhari lakini hakuna lockdown" Wizara ya afya mmesubiri nini kuhamasisha watu kuchukua tahadhari

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Bado naendelea kuwashangaa wizara ya afya, kiongozi wetu mkuu kila mara anasisitiza tuendelee kuchukua tahadhari.

Mara ya mwisho nimemsikia raisi wetu tarehe 19.02.2021 akirudia msemo huu, sasa sijui mnasubiri raisi ndiye afafanue tahadhari anazozisema ni zipi?

Rais ameendelea kusema mwaka jana tulifanya vizuri, ni matumaini yetu kuwa nyinyi wizara ya afya hamtamwangusha nyinyi na hamtawaangusha watanzania kwa kusisitiza tufanye yale yote tuliyoyafanya mwaka jana ili tuendeleze ushindi mkubwa tulioupata mwaka jana.

Lakini hiki kimya ninachokiona nyinyi ndiyo wizara ya afya mkizembea kama ambavyo kwa sasa mmepoa mnaweza kutusabashia kushindwa na tukashindwa kutembea vifua mbele kama tulivyofanya huko nyuma.
 
Kwani mkuu hizo tahadhari ni mpaka wizara au rais aseme?wewe kama wewe pamoja na familia yako hamuwezi kujiongeza?
 
Kwani mkuu hizo tahadhari ni mpaka wizara au rais aseme?wewe kama wewe pamoja na familia yako hamuwezi kujiongeza?
Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini Wanadamu walianzisha Serikali? Labda nikufahamishe kidogo historia.

Utawala katika jamii za wanadamu ulianzia ngazi ya familia, enzi hizo serikali hazipo.

kila familia ilikuwa na utawala wake na waligawana majukumu ngazi ya familia. Lakini kuna changamoto ambazo familia ilishindwa kuzikabili kivyake na ndipo zikaanzishwa tawala za kijamii kwa pamoja ambazo zilianza kama koo n.k

utawala wa kijamii umeboreshwa mpaka leo kufikia kuwa na sura ya kiserikali.

kusema changamoto hizi mtu huwezi kuzikabili wewe na familia yako kwanza ni kudhani serikali haina maana kuwepo, pili ni kuturudisha kwenye maisha ya zamani sana kabla ya kuunda utawala wa koo na kitakachofuata ni kuprove umuhimu wa serikali baada kila mtu kufanya vyake na ugonjwa ukatuzidia nguvu.

Lakini hii inaonyesha hulka ya uzembe na kama siyo mzembe ni jibu ni moja nalo ni mwenye dhamana ya hili ni nani na ni lazima awajibe ambaye mimi nimeona ni wizara ya afya
 
Raisi wa Tanzania akisema watu wote wanyoe nywele na kuwa na vipara hakuna wa kupinga. Watanzania wanaabudi mungu wawili Raisi na mungu muumba wa dunia. Nyerere apumzike mahala anapostahili.
 
Back
Top Bottom