Raia wa Marekani kuchagua Rais kesho

Raia wa Marekani kuchagua Rais kesho

ni trump tu hakuna namna
Let's see
MCHAKATO WA UCHAGUZI WA RAIS WA MAREKANI;

Uchaguzi wa Rais wa marekani hutokea kila baada ya miaka minne, na hufanywa siku ya jumanne ya kwanza baada ya jumatatu ya kwanza ya mwezi November. Maana yake ni kuwa lazima ipite jumatatu ya kwanza ya mwezi November. Mwaka huu wa 2016, mwezi November ulianza jumanne (tar 1/11/2016), na kwa hiyo ikasubiriwa jumatatu ya kwanza ambayo ni tar 7/11/2016 kisha jumanne inayofuata ndio uchaguzi hufanyika.
Mchakato wa uchaguzi huanza na hatua za mwazo ambapo watu wenye nia ya kuwa Rais wa marekani hutangaza nia zao kwa umma wote, hii hufanyika mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi. Watu hao wenye nia wanaweza kutangaza vyama vyao vya siasa watakavyopenda kuviwakilisha au endapo watapenda kugombea binafsi.
Kisha katika majira ya joto ya mwaka hadi mwisho wa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, hutokea mijadala ya mwanzo ya ndani ya vyama na katika majukwaa ya kisiasa.
Mwezi Januari hadi Juni ya mwaka wa uchaguzi hutumiwa na vyama vya siasa kufanya kazi ya kuchuja na hatimaye kumpata kwa kuchagua mtu atakayebeba dhamana ya kuwakilisha katika ugombea wa urais. Septemba hadi Oktoba, wagombea hushiriki katika kampeni na midaharo ya wagombea. Suala la midaharo ya wagombea urasi katika marekani ni la lazima, na hulenga kuwapima wagombea katika kuwakilisha mawazo yao, utashi, ujuzi na uelewa wa mambo ya msingi ya nchi, kwa kuzingatia nafasi nyeti wanayotaka kuitumikia.
Ifikapo siku ya jumanne inayofuata baada ya jumatatu ya kwanza ya mwezi November, uchaguzi hufanyika. Januari ya tarehe 20 baada ya uchaguzi, mshindi huapishwa na kuanza kutumika ofisi. Ikiwa siku ya Januari 20 ni jumapili, basi shughuri za kumwapisha Rais hufanyika jumatatu ya Tarehe 21.

MATAKWA YA KIKATIBA KWA MGOMBEA WA URAIS

Mtu ataruhusiwa kuwa mgombea wa urais wa Marekanai endapo;
1. Atakuwa raia asili wa kuzaliwa Marekani
2. Awe na umri usiopungua miaka thelathini na mitano (35)
3. Ameishi Marekani kwa miaka isiyopungua kumi na mine (14) kabla ya kugombea urais.
Mtu yeyote mwenye vigezo hivyo anaruhusiwa kutangaza nia ya kugombea urais muda wowote, kisha kujisajili katika tume ya uchaguzi ya shirikisho (FEC) kwa ada ya dola elfu 5 (Tsh. Milioni 10)

KUPATIKANA KWA MSHINDI
Kwa mujibu wa katiba ya Marekani mshindi wa uchaguzi wa urais hupatikana kwa kushinda vijimbo vya uchaguzi (electoral college) na sio lazima kupata kura nyingi zaidi ya mwingine. Waasisi wa Taifa la marekani waliweka kanuni hizo ili kuondoa mkanganyiko katika uchaguzi wa Rais kutoka kwa watu na uchaguzi wa Rais unaofanywa na wawakilishi wa watu (congress).
ELECTORAL COLLEGE, ni vijimbo vidogodogo ndani jimbo moja kubwa (state) vinavyo wakilishwa na wawakilishi na maseneta. Wakati jimbo likiongozwa na Gavana, ndani ya jimbo hilo kuna ‘electoral colleges’ zinazoongozwa na wawakilishi (representatives) na maseneta ( senetors) ambao kwa ujumla huunda Bunge la marekani maarufu kama Congress. Kuna jumla ya electoral colleges 538 katika marekani nzima. Mgombea atakayeshinda kwa idadi ya electoral colleges 270, hutangazwa mshindi.

UFAFANUZI

Raia wa Marekani anayeishi jimbo fulani anapopiga kura, kura hizo huenda kwa mgombea husika. Lakini baada ya kuhesabu kura, mgombea aliyeongoza katika jimbo hilo atajizolea kura zote ‘electoral colleges’ Kwa mfano; Jimbo la California lina idadi ya ‘electoral colleges’ 55. Kwa hiyo mgombea atakayeongoza kwa idadi ya kura za jumla katika jimbo la California, atajizolea kura 55 ambazo ni idadi ya ‘electoral colleges’. Na kura hizo 55 huitwa electoral votes. Kwa hiyo, endapo katika jimbo lingine, mfano New York yenye electoral colleges 29, kuwe na idadi kubwa ya watu kuliko ya California yenye electoral votes 55, maana yake, atakayeshinda California atatangazwa mshindi hata kama kura za jumla za New York ni nyjngi zaidi ya California, kwa sababu New York ina electoral colleges 29 tu.
JImbo la California ndio lenye idadi kubwa ya electoral votes 55 likifuatiwa na Texas lenye electoral vote 38. Ndio maana wagobea huumana meno huko California lenye Democrats wengi na Texas lenye Republicans Wengi. Majimbo mengine yenye idadi kubwa ya electoral votes ni New York (29), Florida (29), Pennsylvania(20), Illinois (20) na Ohio (18)
Lakini kama nilivyowasilisha awali, mshindi wa Urais ni lazima awe na angalau electoral votes 270, idadi ambayo ni zaidi ya nusu ya electoral colleges zote 538.
Nini kitatokea endapo mgombea hakufikisha electoral votes 270? Ingawa hutokea mara chache ambapo hakuna mgombea anayefikisha Electoral votes 270, ikitokea, basi idadi ya wagombea watatu waliopata idadi kubwa zaidi watapigiwa kura na wawakilishi wa electoral colleges ambao ni maseneta na wawakilishi wengine. Pia mchakato huohuo hutumika kuwachagua makamu wa Rais, lakini hapa wanaopigiwa kura ni wawili wenye idadi kubwa ya electoral votes na sio watatu kama kwenye urais . kwa maana hiyo, katika hali hii, inawezekana kukawa na Rais wa chama kingine na makamu wa urais wa chama kingine. Hii imewahi kutokea mara moja tu katika historia ya marekani, mwaka 1824, pale John Quincy Adams alipochaguliwa na baraza la wawakilishi kuwa rais wa awamu ya sita wa Marekani.
Kuongoza kwa idadi ya kura za jumla, lakini kushindwa uchaguzi hutokea. Imetokea mara nne katika historia ya Marekani, mara ya mwsho ikiwa mwaka 2000 ambapo George Bush wa Republican alishindwa kwa idadi ya kura lakini akashinda idadi ya electoral votes na kutangazwa mshind dhidi ya Al Gore wa Democrats. Katika uchaguzi huo, ingawa Al Gore alishinda katika jimbo la California lenye idadi ya electoral votes 55, na vilevile kushinda kwa idadi ya kura zote lakini alishindwa katika idadi ya jumla ya electoral votes.

View attachment 430664

Picha hii inaonesha majimbo ya marekani na idadi za electoral votes kwa kila jimbo.

View attachment 430665
VS



View attachment 430667
 
clinton kwasababu ananyege sana na urais lakini urais ataishia kuupigia punyeto.
 
That's right.

In just a matter of hours it's going to be D-day while the world awaits with bated breath.

The greatest country on earth, the most significant nation in the history of mankind will go to the polls to elect its next leader.

I love America. The next best thing to heaven [if indeed there is one].

May the best candidate win.

USA baby
images
images
images
Trump mbele kwa mbele
 
kumbe njia ya trump ni nyeupe hivi! trump ataongoza kwa electoral colleges votes dhidi ya clinton na kutangazwa mshindi,huyo mama atabaki na kura zake za wananchi
 
That's right.

In just a matter of hours it's going to be D-day while the world awaits with bated breath.

The greatest country on earth, the most significant nation in the history of mankind will go to the polls to elect its next leader.

I love America. The next best thing to heaven [if indeed there is one].

May the best candidate win.

USA baby
images
images
images

I hear you, broda! Let's go vote tomorrow![emoji3]
 
Muotaji kuwa Trumph ni Rais urud ukalale tena yawezkana hukumqliza ndoto yako
 
I hope CNN suffers for all the cheating and corruption
 
Binafsi naona chochote kinaweza kutokea, kinacho nishangaza zaidi licha ya mama huyo kupigiwa debe na watu wenye ushawishi mkubwa ukiongezea na vyombo vya habari (MSM) including Establishment Elite cha ajabu bado opinion polls lead inaonyesha Hillary ajazidiana sana na TRUMP, hii inakuwaje tena au inatoa picha gani kwamba baadhi ya Wamerika awana imani na Uongozi wa mwanamke au?

Nafikiri kambi ya Hillary imekwisha liona hilo ndiyo maana wanaonekana hawako over confident - leo kwa mfano nimeona bado wanaendelea kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi kumpigia kura Hillary - wanaendelea kumu-demonise TRUMP, sasa kama wana uhakika watashinda mbona wanaendelea kutumia nguvu nyingi, wakati TRUMP wala atumii nguvu nyingi kwenye kampein zake au kusema maneno mengi, hatumii watu Popular kumpigia debe akiwa jukwaani wala nini sijui!

Trump kuna kitu anajiamini licha ya vyombo vya habari kumpiga vita mara kwa mara lakini raia wa kawaida ambao ni wengi wanaotaka Taifa lao lirudi mikononi mwao kutoka kwenye mikono ya Establishment, kundi hilo la walala hoi ndilo linawatia wasi wasi kundi la Hillary.
 
Urais wa chama mpira anaweza kuupata lkn wa usa kama alivyo kuwa lowassa
 
Ili dunia inendelee kuwa salama Na America kuwa nchi mmoja napenda Bi Clinton achagulie kuwa rais Wa kwanza mwanamke Wa America

Binafsi simpendi bwana Trump!! kwanza ni mbaguzi Na Mimi si pendi ubaguzi!! yeye anakiburi cha pesa akifiri pesa ndo mungu!!


tupia hapa maoni yako au chaguo lako kati ya Bi Clinton Na Mr Trump
 
Back
Top Bottom