Raia wa Marekani kuchagua Rais kesho

Raia wa Marekani kuchagua Rais kesho

[emoji53] Nasubiria yaje matokeo ya tofauti kinyume na wengi
 
Naona wakina jay z, Alicia keys kama juma nature na shilole tu wamejazana kwenye majukwaa ya Democratic kama ya CCM [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naona wakina jay z, Alicia keys kama juma nature na shilole tu wamejazana kwenye majukwaa ya Democratic kama ya CCM [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23] [emoji23] yale yale
 
Kila mu Africa kifo cha kaddafi kimemgusa
Na aliyekuwa ktk mstali wa mbele ktk kifo chake ni Hillary clinton sasa iwejee Leo as really Africans unakaa kabisa na ku cherish Hillary???
Hatuko sawa sisi it's totally insanity over this matters walahi tena,imbeciles
Well said Mkuu! Sisi waafrika bure kabisa! Wanasema Oh republican wanapenda vita, wanampenda Obama vibaya sana, most of them wanakipenda chama cha Democratic lakini twende na facts
1. 1994 mauaji ya kibari Rwanda, Bill Clinton alikuwa Rais wa Marekani lakin hakufanya lolote kusaidia, lakini tunamtukuza
2. Obama alisema hapendi vita na hata akatoa majeshi Iraq lakin ona alilolifanya alienda Libya chini ya Hillary secretary of state kumuua Gadafi kisa ili waweze shinda uchaguzi wa 2012. Wakaingia Misri nadhani unaelewa alivyovurunda
3. Tunajifanya tunaupinga ushoga kwa nguvu zote but nani aliidhinisha ndoa za mashoga? tena kwa kupitia mlango wa nyuma Supreme court baada ya Cogress yenye republican wengi kukataa. Then Obama huyu huyu anakuja Kenya na kuwaambia waafrika ni muda wakukubali ndoa za jinsia moja
4. Ona yanayotokea Syria, Obama na maliberal wa europe wao wanaloliona ni kuwakaribisha wakimbizi kwenye nchi zao. Lengo lao ni kuongeza nguvu kazi kwenye nchi zao ndio maana wanawapa uraia. Huo si wizi wa raia wa nchi nyingine? Kwanini usiwasaidie kwa kuwapa ulinzi ndani ya nchi yao mpaka suluhu itakapopatikana?
Kuna mambo mengi hatuyajui kuhusu hawa Democratic but we just cheering as if they good people for us
 
Yessssss.Hillary for president

Unawezaje kusema watu wengi wamejiaminisha kuwa DT anashinda na hali hata wewe pia umejiaminisha kuwa HC utashinda.

Au umeaminishwa huko...!?

najua watu wengi wamejiaminisha kuwa trump atashinda ila nasema hivi kwa msisitizo!!!!!....
HILLARY CLINTON ndie mshindi kwa urais marekani nasema kwa kujiamini sifati mkumbo huyu mama nimemfatilia sana wakati wa kampeni yupo makini na anakubalikaaaaaaaaaaa anaepinga ushindi wake na aje apa TUPINGE........

HILLARY CLINTON OYEEEEEEE!!!!.
Kwani wameishapiga kura tayari? Zimehesabiwa?
 
Ni kama hapa Tanzania. Lipo gazeti la Tanzania Daima linasapoti Chadema wakati wa Uchaguzi. Au gazeti laUhuru linasapoti CCM.

Kama CCM ingekuwa inamiliki magazeti yote,yote yangesapoti CCM
Ndio ilivyo kule. Bill ni ukoo wa Rockefeller. Wanamiliki vyombo vyote vya habari. Main stream media yote inamsapoti Hillary.
Kwa hiyo wrote tunasubiri kwa hamu kubwa kuona kama Hillary atafanikiwa kuiba Uchaguzi.
Tunasikia Jeshi la Marekani limeshaambiwa litulie:Trump atashinda,lakini Hillary atakuwa Rais.
 
Raia wa Marekani kesho wanapiga kura ya kumchagua Rais atakayeliongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Katika uchaguzi huo Mgombea DONALD TRUMP wa chama cha Republican atachuana dhidi ya mgombea wa chama cha Democratic HILLARY CLINTON.

Mwaka huu kama ilivyo kwa kila baada ya miaka minne raia wa Taifa la Marekani wanaingia katika uchaguzi wa nafasi ya urais.

Nguvu zote zinazotumika kwa wananchi wa Marekani duniani kote kuhamasishwa kupiga kura mapema au kupiga kura kisha kutuma kwa njia ya posta lakini ukweli ni kwamba kura zao sio zinazoamua nani awe Rais bali kikundi cha watu ndio kinaamua, kikundi hicho kinaitwa Electoral college.

Kuelewa kuhusu electoral college inabidi kurudi kidogo katika historia ya taifa hili.

Marekani ina majimbo 50 na ukijumlisha na Washington DC katika muktadha wa mchakato wa uchaguzi yanahesabika kuwa 51.

Majimbo haya yanatofautiana kwa ukubwa na wingi wa watu.

Katika kuleta uwiano na kuhakikisha Rais wa Marekani hajikiti katika majimbo yenye watu wengi pekee, waasisi wa taifa hili waliamua kuwe na wapigaji kura maalum wanaochaguliwa na vyama vyao ambapo wanatokana na ukubwa wa majimbo mfano WISCONSIN kura ni 10, jimbo la IOWA kura sita huku jimbo la California likiwa na kura 55.

Kwa hiyo kundi la watu 538 ndio wanaoamua nani awe rais wa Marekani kwahiyo wamarekani wanavyokwenda kupiga kura wanawapigia kura hawa wawakilishi wao ambao mara nyingi wanakuwa ni makada wa vyama vyao.

Baada ya wananchi wa Marekani kupiga kura jumanne tarehe 8 novemba , kura zao zinahesabiwa na mgombea mmoja atakayeongoza kura hizo maana yake ni kuwa chama hicho kitachukua kura zote za jimbo hilo. Hii inamaanisha kuwa mgombea ambaye atafanikiwa kufikisha kura 270 ndio atakuwa mshindi wa urais.

Pengine unaweza kujiuliza kwanini wagombea wengi hapa wanatumia nguvu nyingi kushawishi mashabiki wao kupiga kura katika majimbo mbalimbali?

hii ni kutokana kuwa kuna majimbo ambayo yamekuwa yakijulikana ni ya chama fulani lakini kuna majimbo ambayo yamekuwa yakibadilika badilika majimbo hayo yanaitwa swing states na ndiyo wagombea DONALD TRUMP na HILLARY CLINTON wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kushawishi wapiga kura kuzipata kura zao.

Kwa kifupi , wananchi wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ni kwa kuwa wanavyopiga kura wanachagua wawakilishi wao na wakishinda kuwa wengi maana yake ni kura nyingi na hivyo kushinda jimbo hilo , … na kura nyingi maana yake ni ushindi kwa mgombea wao ambaye licha ya ushindi wake kufahamika Novemba hii, atatangazwa rasmi Januari 20 ya mwaka 2017 kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi.



Rekebisha kidogo! Mshindi atatangazwa mkesha wa tarehe 9/11/2016; Rais mpya ataapishwa tarehe 20/januari/2017;
 
Tukielekea uchaguzi mkuu wa Marekani si vibaya kupeana Elimu kidogo ya mfumo wa uchaguzi huko USA

Wakati wa uchaguzi mkuu wamarekani huenda vituoni kupiga kura za uraisi lakini majumuisho ya kura hizo ziitwazo *Popular Votes* huwa haziamui mshindi na badala yake Mshindi hupatikana kwa kura ziitwazwo Electoral College

Electoral College ndio bodi inayochagua Rausi na Makamu wa Raisi wa Marekani kwa kila miaka minne.Raia wa marekani hawachagui Raisi na Makamu wao moja kwa moja na badala yake huchagua Electors ambao hutoa ahadi ya kuchagua mgombea fulani watakayempendekeza

Swinging Votes
Haya ni majimbo 11 yenye nguvu na wapiga kura wengi ambayo ni Colorado,Florida Iowa,Michigan,Nevada, New Hampshire,Nirth Caroline,Ohio,Pennsylvania,Virginia na Wisconsin
Majimbo hayo mahesabu yake ya kura hujumuishwa na huchukuliwa mgombea aliyeshinda wastani kwa majimbo yote hayo(Average)

Kwa sasa kuna jumla ya wajumbe Electors 538 ambayo ni jumla ya Wawakilishi 435 na Senators 100 pamoja na Electors watatu iliyopewa Washington DC

Majimbo sita yenye wajumbe wengi wa Electoral ni
California (55)
Texas (38)
New York(29)
Florida (29)
Illinois (20) na
Pennsylvania (20)

Mpaka dakika hii masaa machache kufikia kilele cha uchaguzi wa USA bado ni ngumu kutabiri mshindi kwenye Taifa hili kubwa lenye muunganiko wa majimbo 50 na idadi ya raia 324,942,546
 
Asante... Sasa ebu jaribu kuelezea na utaratibu wa uchaguzi wa Tanzania...
 
Land of opportunity

Nachowakubali usa bendera za vyama sio muhimu sana
Ila bendera ya ya taifa ndio muhimu zaidi

Tofauti na tanzania mkuu wa mkoa unakuta kavaa shati la ccm ofisin

That's right.

In just a matter of hours it's going to be D-day while the world awaits with bated breath.

The greatest country on earth, the most significant nation in the history of mankind will go to the polls to elect its next leader.

I love America. The next best thing to heaven [if indeed there is one].

May the best candidate win.

USA baby
images
images
images
 
Kila mu Africa kifo cha kaddafi kimemgusa
Na aliyekuwa ktk mstali wa mbele ktk kifo chake ni Hillary clinton sasa iwejee Leo as really Africans unakaa kabisa na ku cherish Hillary???
Hatuko sawa sisi it's totally insanity over this matters walahi tena,imbeciles
Binafsi sikuguswa, niliona ni sawa kabisa. Lakini namkubali Trump.
 
Back
Top Bottom