Raia wa Marekani kuchagua Rais kesho

Raia wa Marekani kuchagua Rais kesho

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,635
Reaction score
62,526
Raia wa Marekani kesho wanapiga kura ya kumchagua Rais atakayeliongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Katika uchaguzi huo Mgombea DONALD TRUMP wa chama cha Republican atachuana dhidi ya mgombea wa chama cha Democratic HILLARY CLINTON.

Mwaka huu kama ilivyo kwa kila baada ya miaka minne raia wa Taifa la Marekani wanaingia katika uchaguzi wa nafasi ya urais.

Nguvu zote zinazotumika kwa wananchi wa Marekani duniani kote kuhamasishwa kupiga kura mapema au kupiga kura kisha kutuma kwa njia ya posta lakini ukweli ni kwamba kura zao sio zinazoamua nani awe Rais bali kikundi cha watu ndio kinaamua, kikundi hicho kinaitwa Electoral college.

Kuelewa kuhusu electoral college inabidi kurudi kidogo katika historia ya taifa hili.

Marekani ina majimbo 50 na ukijumlisha na Washington DC katika muktadha wa mchakato wa uchaguzi yanahesabika kuwa 51.

Majimbo haya yanatofautiana kwa ukubwa na wingi wa watu.

Katika kuleta uwiano na kuhakikisha Rais wa Marekani hajikiti katika majimbo yenye watu wengi pekee, waasisi wa taifa hili waliamua kuwe na wapigaji kura maalum wanaochaguliwa na vyama vyao ambapo wanatokana na ukubwa wa majimbo mfano WISCONSIN kura ni 10, jimbo la IOWA kura sita huku jimbo la California likiwa na kura 55.

Kwa hiyo kundi la watu 538 ndio wanaoamua nani awe rais wa Marekani kwahiyo wamarekani wanavyokwenda kupiga kura wanawapigia kura hawa wawakilishi wao ambao mara nyingi wanakuwa ni makada wa vyama vyao.

Baada ya wananchi wa Marekani kupiga kura jumanne tarehe 8 novemba , kura zao zinahesabiwa na mgombea mmoja atakayeongoza kura hizo maana yake ni kuwa chama hicho kitachukua kura zote za jimbo hilo. Hii inamaanisha kuwa mgombea ambaye atafanikiwa kufikisha kura 270 ndio atakuwa mshindi wa urais.

Pengine unaweza kujiuliza kwanini wagombea wengi hapa wanatumia nguvu nyingi kushawishi mashabiki wao kupiga kura katika majimbo mbalimbali?

hii ni kutokana kuwa kuna majimbo ambayo yamekuwa yakijulikana ni ya chama fulani lakini kuna majimbo ambayo yamekuwa yakibadilika badilika majimbo hayo yanaitwa swing states na ndiyo wagombea DONALD TRUMP na HILLARY CLINTON wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kushawishi wapiga kura kuzipata kura zao.

Kwa kifupi , wananchi wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ni kwa kuwa wanavyopiga kura wanachagua wawakilishi wao na wakishinda kuwa wengi maana yake ni kura nyingi na hivyo kushinda jimbo hilo , … na kura nyingi maana yake ni ushindi kwa mgombea wao ambaye licha ya ushindi wake kufahamika Novemba hii, atatangazwa rasmi Januari 20 ya mwaka 2017 kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi.
 
Land of opportunity

Nachowakubali usa bendera za vyama sio muhimu sana
Ila bendera ya ya taifa ndio muhimu zaidi

Tofauti na tanzania mkuu wa mkoa unakuta kavaa shati la ccm ofisin


Haha, me like this!...🙂
 
Hillary Diane Rodham au Hillary Clinton atashinda uchaguzi wa Marekani wa Tar 8/11/2016. Donald Trump atalalamika kuhujumiwa. Sina ushabiki wala upande katika siasa za nchi ya watu, lakini kwa muono wangu, Chama chenye mlengo wa kati-kushoto cha Democrats kitaendelea kuongoza kwa mara nyingine. Hilary Clinton, mwenye umri wa miaka 69, atakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Ikulu ya Marekani tangu nchi hiyo ipate Uhuru wake kutoka kwa Wakoloni wa kiingereza, mwaka 1776. Hilary Clinton na mme wake William Jefferson Clinton (Bill Clinton) wana mtoto mmoja tu, Chelsea Clinton mwenge umri wa miaka 36.


MCHAKATO WA UCHAGUZI WA RAIS WA MAREKANI;

Uchaguzi wa Rais wa marekani hutokea kila baada ya miaka minne, na hufanywa siku ya jumanne ya kwanza baada ya jumatatu ya kwanza ya mwezi November. Maana yake ni kuwa lazima ipite jumatatu ya kwanza ya mwezi November. Mwaka huu wa 2016, mwezi November ulianza jumanne (tar 1/11/2016), na kwa hiyo ikasubiriwa jumatatu ya kwanza ambayo ni tar 7/11/2016 kisha jumanne inayofuata ndio uchaguzi hufanyika.
Mchakato wa uchaguzi huanza na hatua za mwazo ambapo watu wenye nia ya kuwa Rais wa marekani hutangaza nia zao kwa umma wote, hii hufanyika mwaka mmoja kabla ya mwaka wa uchaguzi. Watu hao wenye nia wanaweza kutangaza vyama vyao vya siasa watakavyopenda kuviwakilisha au endapo watapenda kugombea binafsi.
Kisha katika majira ya joto ya mwaka hadi mwisho wa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi, hutokea mijadala ya mwanzo ya ndani ya vyama na katika majukwaa ya kisiasa.
Mwezi Januari hadi Juni ya mwaka wa uchaguzi hutumiwa na vyama vya siasa kufanya kazi ya kuchuja na hatimaye kumpata kwa kuchagua mtu atakayebeba dhamana ya kuwakilisha katika ugombea wa urais. Septemba hadi Oktoba, wagombea hushiriki katika kampeni na midaharo ya wagombea. Suala la midaharo ya wagombea urasi katika marekani ni la lazima, na hulenga kuwapima wagombea katika kuwakilisha mawazo yao, utashi, ujuzi na uelewa wa mambo ya msingi ya nchi, kwa kuzingatia nafasi nyeti wanayotaka kuitumikia.
Ifikapo siku ya jumanne inayofuata baada ya jumatatu ya kwanza ya mwezi November, uchaguzi hufanyika. Januari ya tarehe 20 baada ya uchaguzi, mshindi huapishwa na kuanza kutumika ofisi. Ikiwa siku ya Januari 20 ni jumapili, basi shughuri za kumwapisha Rais hufanyika jumatatu ya Tarehe 21.

MATAKWA YA KIKATIBA KWA MGOMBEA WA URAIS

Mtu ataruhusiwa kuwa mgombea wa urais wa Marekanai endapo;
1. Atakuwa raia asili wa kuzaliwa Marekani
2. Awe na umri usiopungua miaka thelathini na mitano (35)
3. Ameishi Marekani kwa miaka isiyopungua kumi na mine (14) kabla ya kugombea urais.
Mtu yeyote mwenye vigezo hivyo anaruhusiwa kutangaza nia ya kugombea urais muda wowote, kisha kujisajili katika tume ya uchaguzi ya shirikisho (FEC) kwa ada ya dola elfu 5 (Tsh. Milioni 10)

KUPATIKANA KWA MSHINDI
Kwa mujibu wa katiba ya Marekani mshindi wa uchaguzi wa urais hupatikana kwa kushinda vijimbo vya uchaguzi (electoral college) na sio lazima kupata kura nyingi zaidi ya mwingine. Waasisi wa Taifa la marekani waliweka kanuni hizo ili kuondoa mkanganyiko katika uchaguzi wa Rais kutoka kwa watu na uchaguzi wa Rais unaofanywa na wawakilishi wa watu (congress).
ELECTORAL COLLEGE, ni vijimbo vidogodogo ndani jimbo moja kubwa (state) vinavyo wakilishwa na wawakilishi na maseneta. Wakati jimbo likiongozwa na Gavana, ndani ya jimbo hilo kuna ‘electoral colleges’ zinazoongozwa na wawakilishi (representatives) na maseneta ( senetors) ambao kwa ujumla huunda Bunge la marekani maarufu kama Congress. Kuna jumla ya electoral colleges 538 katika marekani nzima. Mgombea atakayeshinda kwa idadi ya electoral colleges 270, hutangazwa mshindi.

UFAFANUZI

Raia wa Marekani anayeishi jimbo fulani anapopiga kura, kura hizo huenda kwa mgombea husika. Lakini baada ya kuhesabu kura, mgombea aliyeongoza katika jimbo hilo atajizolea kura zote ‘electoral colleges’ Kwa mfano; Jimbo la California lina idadi ya ‘electoral colleges’ 55. Kwa hiyo mgombea atakayeongoza kwa idadi ya kura za jumla katika jimbo la California, atajizolea kura 55 ambazo ni idadi ya ‘electoral colleges’. Na kura hizo 55 huitwa electoral votes. Kwa hiyo, endapo katika jimbo lingine, mfano New York yenye electoral colleges 29, kuwe na idadi kubwa ya watu kuliko ya California yenye electoral votes 55, maana yake, atakayeshinda California atatangazwa mshindi hata kama kura za jumla za New York ni nyjngi zaidi ya California, kwa sababu New York ina electoral colleges 29 tu.
JImbo la California ndio lenye idadi kubwa ya electoral votes 55 likifuatiwa na Texas lenye electoral vote 38. Ndio maana wagobea huumana meno huko California lenye Democrats wengi na Texas lenye Republicans Wengi. Majimbo mengine yenye idadi kubwa ya electoral votes ni New York (29), Florida (29), Pennsylvania(20), Illinois (20) na Ohio (18)
Lakini kama nilivyowasilisha awali, mshindi wa Urais ni lazima awe na angalau electoral votes 270, idadi ambayo ni zaidi ya nusu ya electoral colleges zote 538.
Nini kitatokea endapo mgombea hakufikisha electoral votes 270? Ingawa hutokea mara chache ambapo hakuna mgombea anayefikisha Electoral votes 270, ikitokea, basi idadi ya wagombea watatu waliopata idadi kubwa zaidi watapigiwa kura na wawakilishi wa electoral colleges ambao ni maseneta na wawakilishi wengine. Pia mchakato huohuo hutumika kuwachagua makamu wa Rais, lakini hapa wanaopigiwa kura ni wawili wenye idadi kubwa ya electoral votes na sio watatu kama kwenye urais . kwa maana hiyo, katika hali hii, inawezekana kukawa na Rais wa chama kingine na makamu wa urais wa chama kingine. Hii imewahi kutokea mara moja tu katika historia ya marekani, mwaka 1824, pale John Quincy Adams alipochaguliwa na baraza la wawakilishi kuwa rais wa awamu ya sita wa Marekani.
Kuongoza kwa idadi ya kura za jumla, lakini kushindwa uchaguzi hutokea. Imetokea mara nne katika historia ya Marekani, mara ya mwsho ikiwa mwaka 2000 ambapo George Bush wa Republican alishindwa kwa idadi ya kura lakini akashinda idadi ya electoral votes na kutangazwa mshind dhidi ya Al Gore wa Democrats. Katika uchaguzi huo, ingawa Al Gore alishinda katika jimbo la California lenye idadi ya electoral votes 55, na vilevile kushinda kwa idadi ya kura zote lakini alishindwa katika idadi ya jumla ya electoral votes.

14910426_1285008301564404_9104998552605383776_n.jpg


Picha hii inaonesha majimbo ya marekani na idadi za electoral votes kwa kila jimbo.

Hillary Clinton.jpg


vs

Donald Trump.jpg
 
Naona unabii was baba T. B Joshua umekuingia vilivyo...
 
Hillary Diane Rodham au Hillary Clinton atashinda uchaguzi wa Marekani wa Tar 8/11/2016. Donald Trump atalalamika kuhujumiwa. Sina ushabiki wala upande katika siasa za nchi ya watu, lakini kwa muono wangu, Chama chenye mlengo wa kati-kushoto cha Democrats kitaendelea kuongoza kwa mara nyingine. Hilary Clinton, mwenye umri wa miaka 69, atakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Ikulu ya Marekani tangu nchi hiyo ipate Uhuru wake kutoka kwa Wakoloni wa kiingereza, mwaka 1776. Hilary Clinton na mme wake William Jefferson Clinton (Bill Clinton) wana mtoto mmoja tu, Chelsea Clinton mwenge umri wa miaka 36.
Itakuwa ni habari mbaya kwa Tanzania na Waafrika weusi Marekani.
 
Mimi na mtakatifu Trump ili are kuwanyoosha viongoxi wa Afrika
 
Nimefurahi kugundua kuwa tabia za wapinzani wa kisiasa duniani kote zina shabihiana, kulalamika kuibiwa au kuchakachuliwa kwa uchaguzi. Trump zee zima linalalamikia kuchezewa faulu na bibi.

Na washawasha!
 
Hakuna alichotabiri huyo anacheza na media zinavyosema tu. We uchaguzi umebaki siku 4 ndo unatabiri angetabiri mwanzo wa mwaka
[emoji12] Ko wew na yeye ndo wale wale... Uzi wako na wew Ungekuwa hata two months back,
 
Back
Top Bottom